Pinda awaomba radhi Wakatoliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda awaomba radhi Wakatoliki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 4, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Na Sammy Kisika, Sumbawanga

  WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda amewaomba radhi viongozi wa dini hasa Kanisa Katoliki kutokana na kitendo cha baadhi ya wafuasi na wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia kauli zinazokinzana na imani zao wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita.

  Bw. Pinda ambaye pia Mjumbe wa halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM, aliomba radhi hiyo katika kikao baina yake na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na baadhi ya wazee maarufu wa mjini hapa jana, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Libori mjini Sumbawanga.

  "Najua tulimkwaza Mhashamu Baba Askofu (Damian Kyaruzi), tumekejeli imani ya dini yake, tunaomba radhi. Mimi naomba radhi kwa niaba ya CCM na serikali. Si hapa tu (Sumbawanga) lakini ni maeneo mengi nchini kama vile majimbo ya uchaguzi ya Hai na Same ambapo baadhi ya wagombea katika kuomba kura ya ndiyo, walilazimika kutumia baadhi ya maneno yanayotumika katika Injili.

  "Uchaguzi mkuu uliopita haukuwa laini kama ilivyotarajiwa na kutazamiwa, lakini badala yake ulikuwa na changamoto nyingi ikiwemo tofauti za kimtizamo na kiimani, hivyo kwa yale yaliyojitokeza ya baadhi ya waliokuwa wagombea kugusa imani za dini za watu, halikuwa lengo lao kufanya hivyo na tunaomba mtusamehe kwa yote yaliyojitokeza na kukwaza imani za dini zenu," alisema Bw. Pinda.

  Kauli hiyo ya Bw. Pinda imekuja wakati Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga likiwa limewasimamisha na kuwatenga baadhi ya waumini kwa kukashifu Utatu Mtakatifu kwa kuufananisha na kaulimbiu ya mafiga matatu, yaani rais, mbunge na diwani; wakifananishwa na Mungu, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu wakati wa kampeni.

  Vile vile waumini hao ambao ni wafuasi wa CCM wanadaiwa kukashifu alama ya kanisa, msalaba, kwa kuuzika wakati wa kushangilia ushindi wa mgombea wao.

  Wakati Bw. Pinda akikiri makosa hayo na kuomba radhi, baadhi ya viongozi wa CCM mkoani humo wamekuwa wakissitiza kuwa waumini hao wametengwa kutokana na kushabikia chama hicho na mgombea wake wa Ubunge, na hivyo kutofautiana na mgombea wa CHADEMA wanayedai alikuwa anaungwa mkono na kanisa hilo.

  Akitoa maoni ya jumla ya uchaguzi huo, Bw. Pinda alisema kuwa kutokana hali iliyojitokeza, CCM na Serikali yake imepata fundisho, na hivyo kuomba katika chaguzi zijazo viongozi wa dini, serikali na vyama vya siasa wakae pamoja na kuweka angalizo ili wagombea wajiepushe na kukejeli imani za dini za watu wengine.

  Waziri Mkuu aliwasihi viongozi hao wa dini nchini nzima kuanza ukurasa mpya na kutumia muda mrefu kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo.

  Akizungumzia suala la rushwa, alikiri kukithiri kwa vitendo hivyo katika uchaguzi mkuu uliopita na kuongeza kuwa ipo haja ya kuangali upya mfumo wa uchaguzi kuanzia ndani ya CCM ambayo inajiandaa kwa uchaguzi wa viongozi wake mapema mwakani, ili kuhakikisha hautatoa mianya ya rushwa.

  Aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini na wazee kukemea kwa nguvu zote vitendo vya rushwa.

  "rushwa ni rushwa tu, hakuna haja ya kusema kuna rushwa ndogo hata mtu anapotaka kutimiza haja zake fulani kwa kutoa kitu kidogo bado ni rushwa. Pia kwa mgombea anapotoa doti ya khanga ili apigiwe kura hilo ni tatizo, hivyo naiomba CCM ibadilike, najua ni jambo gumu lakini lazima tupigane nalo kikamilifu. Wagombea nao taabu tu, hasa kwenye chama, safari hii tujirekebishe," alisema Pinda.

  Akitoa neno la shukrani, Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Tanzania mkoa wa Rukwa, Mchungaji Israel Moshi alisema kuwa madhehebu ya dini yamesamehe, na kuwataka viongozi kusameheana kwa kuwa wote ni binadamu.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Hivi Pinda haoni umuhimu kwanza wa kuwashauri waliokashifu ukatoliki kuwa mstari wa mbele kuomba radhi ili wasamehewe........badala ya wao kujificha kwenye kivuli cha CCM na cha Waziri Mkuu?

  Isitoshe wahusika wamekuwa wakiendelea kutoa kauli za kuukejli uongozi wa kanisa..............sasa lipi kanisa lifuate.....................Pinda au hao wakorofi wachache ambao wameamua kumpa kaisari yale ya Bwana?
   
 3. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  samehe saba mara sabini lakini ccm nilaima ife kwanza ndiyo iweze kusamehewa baada ya kufufuka
   
 4. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...... ni lazima ife kwanza....
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Maoni yangu nayatunza bado juu ya hili kama kijisehemu fulani tu ya serikali ndiyo imeweza kulitambua.
   
 6. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HabariLeo hawajaomba radhi lakini maana ndiyo walikuwa wachochezi wakuu wa mgogoro huu
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  there are some who are being played fool out there! I doubt sencerity ya hii kuomba radhi kwa mwanasiasa! Siyo kwa sababu tu kura zimeshapigwa na mshindi kasherehekea? Uchaguzi mwingine ukifika, tabia hiyo hiyo! Wanahitaji wokovu wa kwelisio hii.
   
 8. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Hakuna kuwasamehe, hao jamaa ni wajinga na walifanya hivyo makusudi hakuna haja ya kuwasamehe kabisa kama mbwai na iwe mbwai tuu haiwezekani kushangilia ushindi kwa kuzika msalaba wa masiha wetu huo ni mpango wa wazi kabisa wa wapinga kristo.

  No no no no msamaha na adhabu yao kuu ni kutowapa kura hata moja chama chao na hao wapinga kristo
   
 9. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Chonde chonde wana Sumbawanga, msamehe Pinda lakini si mbunge na rais wake! Waje wenyewe na kuomba radhi,waifungie pia jarida la habariLeo,ndo wananchi tutaona kuwa wanahitaji msamaha.

  Mwisho wa mwaka ktk ukumbi mmoja hapa DSM JK karudia yale yale, anauliza wasanii na waliohudhuria, nlisikia anasema "sisi tuna maandiko matakatifu kama ya nani? Marko, Yohana?!" Watu wakajibu "Philip". JK akacheka kama kawaida yake, akarudia kwa kejeli "Ya Philip Marmo, sio?" akasema tena "Ndio, ya Marmo ndo yetu CCM".

  Jaman sikuamini! Nilitamani nizime Tv. Kama kuna mtu aliyeona anaweza kudhibitisha hii laana pale ukumbini, kama sikosei ni Diamond Jubilee!

  Narudia kusema Msamehe Pinda lakini si JK, si mbunge wao, si madiwani wala wale waliotengwa! Ni ombi langu kwa Kanisa Katoliki!
   
 10. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,195
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  As Pinda kama ulihusika na kejeli hiyo ima uliwatuma haki hiyo ya kuomba msamaha unayo Kinyume cha Maelezo hayo bado bado ni propaganda tu! .....ATAKAYE MKUFURU ROHO WTAKATIFU HANA WA KUMSAMEHE;!
   
 11. O

  Omumura JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kanisa limesisitiza wanaopaswa kuomba radhi ni waumini wenyewe na haikubaliki hata kidogo eti kumtuma
  Pinda ndio awaombee msamaha, Pinda nae kama ana akili asikatikie nyege zisizo za kwake.Hao jamaa waliji
  ona wamefika na hasa walipokuwa wanalitumia gazeti la Habari Leo kama ngao na chombo cha propaganda
  ili kuupotosha umma juu ya kilichokuwa kikiendelea!Ni lazima watubu!!!
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,224
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Nadhani msamaha wangeomba wahusika wenyewe, ili kuonesha uzito na kujutia walichokifanya. Kwa nini Pinda awe ndo "Shock Absorber" ya kubeba kila chafu la serikali na sisiemu?
   
 13. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Msamaha unaoombwa kwa Kanisa Katoliki si wa kuongea mbele ya wazee au waandishi wa habari. Ni msamaha ambao unafanyika katika ibada au misa maalum ambapo kila muumini aliyefanya kosa kubwa kama hilo la kumkashifu roho wa Bwana anapita na kula kiapo cha kumkana shetani na mambo yake yote.

  Sana sana Pinda angewaombea msamaha kwa Mungu huku akimuomba Mungu awape ujasiri wa kukiri makosa na kufanya kitubio.
   
 14. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,062
  Likes Received: 3,928
  Trophy Points: 280
  kwani walifanya nini? na kanisa katolini ni nini? si dini kama dini zingine tu? kitendo gani cha ajabu walifanya haswa?
   
 15. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani Pinda kaomba msamaha kwa niaba ya CCM na serikali tu. Wale watu moja moja waliotoa kashfa na hatimaye kufungiwa na kanisa wanaendelea na adhabu zao hadi watakapoomba msamaha na kutubu kibinafsi.
   
 16. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kamuulize Pinda..............walicho fanyaaaaaaaaaaa
   
 17. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, umeshindwa hata kuisoma habari? Mbona inaeleweka hata kwa mtu ambaye hakuwahi kusikia lolote?
   
 18. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  As always absorbing the shocks of his CCM members shits!
   
 19. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Imeandikwa kisasi ni kwa BWANA wa Majeshi si kwetu. Tena imeandikwa usiposemehe hauwezi kusamehewa. Futa kauli yako kama wewe ni Mkristo.
   
 20. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu vipi tena umesahau jazba walizonazo watu wa pande hile wanasikia jina la kanisa katoliki,ukristu.Hawezi kusoma habari yote kwa sababu kichwa cha habari teyari kilishamchukiza!poleni sana watu wa aina hii kwa kuwa ukristu ulikuweo,upo na utaendelea kuwepo,hakuna anayeweza kuutokomeza!!
   
Loading...