Pinda ashindwa kupelekea madaktari wanajeshi ktk hospitali za DSM

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
katika kuthibitisha ukosefu wa umakini ndani ya serikali, mchana huu mwandishi wa Clouds Redio ameripoti kuwa wagonjwa katika hospitali ya Muhimbili hawakupata huduma yeyote ikiwemo kushuhudia zaidi ya ambulance 7 zikileta wagonjwa toka hospitali mbali mbali na kulazimika kuondoka na wagonjwa wao kutokana na kukosekana kwa huduma katika hospitali hiyo. Hii inashiria kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameshinde kutekeleza ahadi yake kupelekea madajatari toka JWTZ na JKt akama alivyoahidi jana wakati akitoa kauli za dharau dhidi ya madakatari wanaogoma.

My take: Tukumbuke kiini cha mgogoro huu ni madakatari walioko mafunzoni yaani interns katika hospitali ya Muhimbili kunyanyaswa na uongozi wa Wizara ya Afya hivyo kutakiwa Waziri Dr Haji Mponda, Katibu Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Ngd Deo Mtasiwa kuondolewa mara moja kwa kuishawishi serikalim kuchukua hatua za kionevu dhidi ya madakatari hao waliokuw akatika mafunzo. Ni kwanini Serikali inakubali watanzania wafe katika kuwalinda wazembe watatu?

Ni imani yangu watatu hao wakiondolea hata leo madakatari walioko katika mgomo watakuwa tayari kuzungumza na serikali kuhusu madaia yao.
 
wanachofanya ni kama kuondoa pesa mfuko wa kulia na kuhamishia kushoto... hukuwa kisahau kwamba the bottom line imeshakuwa depleted

hospitali za jeshi nao watakosa huduma
 
katika kuthibitisha ukosefu wa umakini ndani ya serikali, mchana huu mwandishi wa Clouds Redio ameripoti kuwa wagonjwa katika hospitali ya Muhimbili hawakupata huduma yeyote ikiwemo kushuhudia zaidi ya ambulance 7 zikileta wagonjwa toka hospitali mbali mbali na kulazimika kuondoka na wagonjwa wao kutokana na kukosekana kwa huduma katika hospitali hiyo. Hii inashiria kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameshinde kutekeleza ahadi yake kupelekea madajatari toka JWTZ na JKt akama alivyoahidi jana wakati akitoa kauli za dharau dhidi ya madakatari wanaogoma.

My take: Tukumbuke kiini cha mgogoro huu ni madakatari walioko mafunzoni yaani interns katika hospitali ya Muhimbili kunyanyaswa na uongozi wa Wizara ya Afya hivyo kutakiwa Waziri Dr Haji Mponda, Katibu Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Ngd Deo Mtasiwa kuondolewa mara moja kwa kuishawishi serikalim kuchukua hatua za kionevu dhidi ya madakatari hao waliokuw akatika mafunzo. Ni kwanini Serikali inakubali watanzania wafe katika kuwalinda wazembe watatu?

Ni imani yangu watatu hao wakiondolea hata leo madakatari walioko katika mgomo watakuwa tayari kuzungumza na serikali kuhusu madaia yao.
mkuu bora umeturudisha kwenye hoja ya msingi, maana PM yeye anaongea tu kuwa anaweza kureplace doctors wote wakati serikari hiyo hiyo imeshindwa kupeleka hata madawa kutoka MSD lakini haisiti kuja na ahadi kubwa within 24hrs!!!

Kama kuna mtu anayeweza kutathmini hasara iliyosababishwa na mgomo mpaka sasa ndio atajua kuwa kuondoka kwa Mh. Mponda, Nyoni, Mtasiwa nk ilikuwa ni nafuu sana kwa taifa.

Namshauri PM (japo mimi ni mtu mdogo sana na siwezi hata kumkaribia) aache porojo na ku-victimize viongozi wa mgomo badala yake ashughulikie madai kama ni ya kweli na kama sio ya kweli basi atwambie maana yeye ni juzi tu wakati wenzie wanaenda Apollo India yeye alienda London kucheck afya yake!

Mi nadhani suluhisho ni kuwatimua viongozi wa wizara ya afya kwanza wakiongozwa na Blandina ndipo mgogoro huu utakapoisha maana she is the source of all the troubles we see in the MOH
 
k

... Ni kwanini Serikali inakubali watanzania wafe ...?

Nani anakubali watanzania wafe? Kama ni hukumu, basi huwa kuna hukumu 1st hand murder & 2nd hand murder. Hapa nadhani 1st-hand murders ni nyinyi madaktari msiowahudumia hao wagonjwa na 2nd-hand murders ni hao wengine. Wekeni ubinadamu mbele ..
 
mkuu bora umeturudisha kwenye hoja ya msingi, maana PM yeye anaongea tu kuwa anaweza kureplace doctors wote wakati serikari hiyo hiyo imeshindwa kupeleka hata madawa kutoka MSD lakini haisiti kuja na ahadi kubwa within 24hrs!!!

Kama kuna mtu anayeweza kutathmini hasara iliyosababishwa na mgomo mpaka sasa ndio atajua kuwa kuondoka kwa Mh. Mponda, Nyoni, Mtasiwa nk ilikuwa ni nafuu sana kwa taifa.

Namshauri PM (japo mimi ni mtu mdogo sana na siwezi hata kumkaribia) aache porojo na ku-victimize viongozi wa mgomo badala yake ashughulikie madai kama ni ya kweli na kama sio ya kweli basi atwambie maana yeye ni juzi tu wakati wenzie wanaenda Apollo India yeye alienda London kucheck afya yake!

Hakuna suala la udogo au ukubwa hapa mtu ukiwa kiazi ni kiazi tu kwa mfano hapa PM ni kiazi wa hakuna kuogopa PM ni Kiazi
 
pinda ana weakness ya kutumia feelings zaidi ktk maamuzi kuliko hali halisi!
 
Kusema tunamadaktari wa kutosha Jeshini ni sawa na kusema Jeshi letu lina ndege kibao za kivita zinazoweza kuruka wakati wowote.

Hii inaitwa Wishful Thinking.

Tatizo la watu kaa Pinda ni kutumiwa kama ya Ndani jeshini kuna MA na RMA kibao ambao wenyewe wanawaita Madaktari.
Jamaa kaletewa idadi kwa ununda wake wa kushindwa kudadisi hoja kadhanimadkari jeshini ni kibao huyo kaenda kuropoka kwenye vyombo ya habari.

Hivi hao madaktari wa jeshi wakitolewa huko jeshini na kuletwa Muhimbili ni nani atahudumia katika hospitali za jeshi walizoziacha bila madakitari??

Ni siasa zinazo mtuma kuropoka au ni ubabe wa kijima?
 
Najiuliza hao madaktari kutoka jeshini huwa wapo tu hawana kazi?what i know wanatumika ktk hospitali za huko/jeshini. Sasa ukiwaondoa what next?na ni wengi kiasi hiko? kauli nadhani ilitoka kwa jazba

Madaktari wa jeshi wanafanya kazi wakati wa vita tu..muda mwingine wanakuwa wanakula na MEREMETA. Ni wakati wao wa kulipa fadhila. Huko jeshini wataenda kuimport madaktari wengine tokea China...labda wanathani itakuwa cheap labour kama walivyozoea.
 
pinda ana weakness ya kutumia feelings zaidi ktk maamuzi kuliko hali halisi!

Well analysed, hii ni best assessment kuhusu akili na uwezo wa Pinda katika sentensi moja. Hilo nilitambua wakati wa issue ya kuuawa kwa Tanzanians wenye albinism.
 
Madaktari wa jeshi wanafanya kazi wakati wa vita tu..muda mwingine wanakuwa wanakula na MEREMETA. Ni wakati wao wa kulipa fadhila. Huko jeshini wataenda kuimport madaktari wengine tokea China...labda wanathani itakuwa cheap labour kama walivyozoea.
na kwa akili za viongozi wetu hili suala sio la ajabu kutokea mkuu!
 
kauli za wanasiasa tu, kuvuka mto kwa kutumia godoro, aibu kwake pm

busara ya mtu ni jinsi anavyopambana na mitihani ya kimaisha akiiweza ataonyesha busara zake akishindwa ataonyesha udhaifu wake, je huyu pm yupo kundi lipi?
 
Pinda Amepinda. Amepiga muziki kumbe hakuna mchezaji na mwenyewe hajui kucheza.

Hao watu watatu waondoshwe ili kulinusuru Taifa. yaani pinda anafikiria kufukuza kazi Madaktari wote badala ya kufukuza Kazi watu watatu.

Ama kweli kazi imemshinda na ame-pinda kweli!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
kumbuka Pinda alivyosema Bungeni issue ya maandamano ya CDM kuhusu Lema,hee huyu Lema anaoneka ni mtu wa fujofujo hivi,ni hisia tu bila kuwa na uhakika ndo yanayoigharimu sirikali yetu wakioma viongozi kama hawa .Wao wanjua tu watakuwa hapo milele ,Nyie subiri tu Ndumba ,Rungu,FFU na nini na nini haziwezi kuzima Hoja zenye Nguvu
 
Back
Top Bottom