Pinda ashindwa kupelekea madaktari wanajeshi ktk hospitali za DSM

Huu mlundikano wa maDaktari hospitali za Dar unatokana na nini. Tarafa ninayotoka kuna kituo kikubwa tu cha afya tangu miaka ya mwanzo ya 80. Hajawahi kuletwa Daktari pale! Nimeshangaa kusikia Amana ina Madaktari zaidi 30 mbali na Interns wa kila mwaka.
 
Unamaanisha sababu ya msingi ya mgomo wenu "interns" ni uongozi wa Wizara ya Afya (Dr Haji Mponda, Katibu Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Ngd Deo Mtasiwa)!! Mbona Mh. Waziri Mkuu aliposoma na kuyatolea maelezo madai ya hao interns inaonesha msingi mkuu wa mgomo ni madai ya mshahara mnono na posho nono kama za wabunge wa bunge la Tanzania!

Wamelichukilia pupa susla zima la afya na uhai wa watu!
 
Hivi kwa haraka haraka mnadhani niwangapi wanapoteza maosha kwa sababu ya malumbano haya. Hebu mwenye taarifa atujuze!
 
Tuache ushabiki na chuki za kudumu kwa serikali ya CCM na JMK. Tupate ufafanuzi wa yafuatayo:
-Kwa nini Madaktari wetu walikataa kuonana na Waziri Mkuu wetu?
-Kulihitajika kundi zima la madaktari kumsikiliza Waziri Mkuu alichotaka kuwaambia?
-Madaktari hawa hata kwa umri wao ukilinganisha na wa WM Pinda wakashindwa kumheshimu wamsikilize tu hata kama wasingekubaliana naye?
-Matatizo ya Madaktari wetu hayapo kwenye taaluma na ajira zingine?
[QUOTE
]Serikali rudisheni JKT. Wengi wa madaktari hawa kwa umri wao wameyakosa malezi ya J
K
T.

[/QUOTE]Kwani hao akina Lowassa na JK waliopita JKT wamelisaidia nini taifa hili?
 
Neno ubinadamu lisiwe ngao ya kunyanyasa madaktari. Wao pia wana familia zao zinazowategemea na hawawezi kuewakabidhi kifurushi kinachoitwa "ubinadamu" ili kutatua matatizo yao wanachohitaji ni haki zao halali zitimizwe ili wakidhi mahitaji yao. Ubinadamu haulipi ada wala kodi ya nyumba.

Mbona yule daktari aliyemuudumia mgonjwa kwenye flight XXXX over atlantic kwa masaa 5 hakulipwa na airline? udaktari ni wito pia. Warejee viapo vyao.
 
wewe ni mgonjwa au la wewe ni Gamba,unasemaje?hiyo mizigo iliyoko huko wizara ya afya huioni?na kinachofanya Nyoni aonekane kama ndio mmiliki wa wizara ya afya ni nini?na hao mawaziri wanafanya nini hapo,huyo mganga mkuu juzi tu katoka kufanya madudu ya Reagents za HIV bado havijapoa kalizua jingine na bado mnakinga kifua,kwanini huangalii chanzo cha tatizo?

vyovyote kichaa chako kitakavyokutuma ... I am just a disillusioned citizen/baada ya kujionea hali halisi (kwenye moja ya mahospitali). Tembeleeni mahospitali muone watu wanavyotaabika ndiyo mtoe comments zenu.
 
Mbona yule daktari aliyemuudumia mgonjwa kwenye flight XXXX over atlantic kwa masaa 5 hakulipwa na airline? udaktari ni wito pia. Warejee viapo vyao.

wakati wanarejea viapo vyao na wewe urejee ufisadi wako na wa wenzio!
 
Back
Top Bottom