Hivi ukimtukana PM si unaweza kupelekwa Keko? Huyu jamaa naye anaweza kuishia kutukanwa. Wamepewa majina na Dr. Slaa, wameshindwa kuchukua hatua mpaka wengine wanakufa/wanatoroka bila kuhojiwa.
Anataka wananchi tumsaidie nini tena?
Alisema kwa upande wake, serikali inayafanyia kazi mapendekezo ya wadau, kuhusu kuigawa Tanesco ili liwe na kampuni tatu zitakazojitegemea, pamoja na kuanzisha mamlaka za kusimamia biashara katika sekta ya nisahti na maji mijini na vijijni.[/size][/color]
Kwanza atusaidie kuwapeleka keko EL na wenzie ambao tuna ushahidi wao mkononi. Naye siku hizi naona kapinda na anaturudisha kwenye enzi zilezile za maneno bila matendo. Kila leo wananchi tunaombwa tusaidie bila hatua kuchukuliwa sasa wacha sisi tushughulike kivyetu na tuone jinsi tunavyoweza kuwashughulikia hawa mafisadi. Subiri tu ilo siku watajua kuwa Umma wa watizedi umekasirika.
Washughulikie kwanza waliokwishajulikana badala ya kudai wakikamatwa nchi italipuka
Posted Date::5/28/2008
Pinda aomba msaada kukabili mafisadi
Na Kizitto Noya
Mwananchi
SERIKALI imeiomba jamii kuipa ushirikiano kuwabaini wala rushwa na wahujumu uchumi, kwa kuwa wamekuwa kikwazo cha maendeleo nchini.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa pamoja na uchumi wa nchi kukua kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni, ufisadi umekuwa ukihujumu uchumi na kuongeza kiwango cha umaskini nchini.
Wito wangu kwa wananchi wote wakiwemo wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (tanesco), ni kushirikiana na serikali kubaini wahalifu ambao wamekuwa wakisababisha hasara kubwa.
Serikali itachukua hatua kali za kisheria kupambana na wote wataopatikanma wakihujumu miundombinu muhimu,?alisema Pinda.