BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,845
Washughulikie kwanza waliokwishajulikana badala ya kudai wakikamatwa nchi italipuka
Posted Date::5/28/2008
Pinda aomba msaada kukabili mafisadi
Na Kizitto Noya
Mwananchi
SERIKALI imeiomba jamii kuipa ushirikiano kuwabaini wala rushwa na wahujumu uchumi, kwa kuwa wamekuwa kikwazo cha maendeleo nchini.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa pamoja na uchumi wa nchi kukua kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni, ufisadi umekuwa ukihujumu uchumi na kuongeza kiwango cha umaskini nchini.
Pinda alisema hayo wakati akifungua Jukwaa la Nne la Sekta ya Nishati, lililoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema tangu kuanzishwa kwa sera ya Urekebishaji na Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma na Mageuzi ya Kiuchumi yaliyoruhusu mfumo wa soko huria, mapato ya serikali yameongezeka kutoka Sh25bilioni kwa mwezi mwaka 1995 hadi Sh280 bilioni kwa mwezi mwaka huu.
Alisema pia thamani ya uuzaji wa bidhaa nchi za nje imeongezeka kutoka dola za Marekani 851.3milioni mwaka 2001, hadi dola 3.5 bilioni mwaka jana. Kwa mujibu wa Pinda pamoja na ongezeko hilo uchumi wa Tanzania unahujumiwa rushwa na wizi wa rasilimali za umma vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wa serikali na wananchi wa kawaida.
Wito wangu kwa wananchi wote wakiwemo wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (tanesco), ni kushirikiana na serikali kubaini wahalifu ambao wamekuwa wakisababisha hasara kubwa.
Serikali itachukua hatua kali za kisheria kupambana na wote wataopatikanma wakihujumu miundombinu muhimu,?alisema Pinda. Waziri Pinda aliwataka wafanyabiashara nchini kuwekeza katika uzalishaji wa umeme ili kukabiliana na tatizo la upatikana wa nishati hiyo kwa kuwa na vyanzo mbadala.
Alisema kwa upande wake, serikali inayafanyia kazi mapendekezo ya wadau, kuhusu kuigawa Tanesco ili liwe na kampuni tatu zitakazojitegemea, pamoja na kuanzisha mamlaka za kusimamia biashara katika sekta ya nisahti na maji mijini na vijijni.