Kwa wengi wasiojua facts and figures katika sekta za Nishati na Madini, huyu Prof. Muhongo alionekana kama vile ametoa facts na figures za hali ya juu kwenye mdahalo uliofanyika Chuo KIkuu DSM, kumbe ni ubabishaji mtupu. Malalamiko kuwa wazawa wana viwanja vingi kwenye utafutaji wa madini na ambavyo havifikii hata asilimia 10 ya viwanja vyote vilivyopo ni kichekesho kitupu. Aidha, ukubwa wa kiwanja si hoja ili mradi viwanja hivyo vimepatikana kihalali na kwa kufuata sheria. Inaonekanakana kwa Profes huyu kwamba mzawa akipata fursa ya kushiriki kwenye kuendeleza rasilimali zilizop nchini, hiyo inamuudhi sana na ndiyo maana akadiriki katukana Wazalendo kuwa kazi yao ya msingi ni kutengeneza juice na maandazi kwa ajili ya wageni. Matarajio ya Watanzania kutoka kiongozi wa wizara nyeti kama hii yalikuwa ni kumsadia na kumjenga mwekezaji mzalendo aweze kushiriki kikamilifu katika fursa za kuendeleza rasilimali zetu. Tulichoambulia kwa Pofesa huyu ambaye anajigamba ndiye msomi wa hali ya juu kuliko wasomi wengine nchini? ni matusi, kejeli na kauli za ubabashaji. Labda nidokeze kwa kifupi fusra ambazo makampuni yetu hapa nchini yanaweza kushiriki katika utafutaji na uendelezajiwa sekta ya mafuta na gesi: (a)Kushiriki moja kwa moja kama wabia katika shughuli za kutafuta mafuta. Tayari wako wazalendo ambao wameonesha mwamko wa kushiriki katika fursa hizi. (b) kutoa huduma za kifedha na bima; (c) Kutoa huduma za kitaalamu kwa makampuni ya nje; (d) Kutoa huduma za usafirishaji (Logistics); (e)Kutoa huduma za ulinzi; (f) Kutoa huduma za burudani, malazi na vyakula; (g) Kutoa huduma za nyigine za kiufundi kama vile tathmini za mazingira, kijamii, hali ya hewa na nyinginezo. Hayo ni baadhi tu ya maeneo mengi ambayo wazalendo wanaweza wakahamasishwa kushiriki. Cha ajabu huyu Profesa na uongozi wa Wizara hawayaoni haya bali waona kazi ya Watanzania ni kutengeneza juice. Haya ni matusi na kielelezo dhahiri kuwa huyu siyo kiongozi bali ni mzigo mkubwa sana kwa Taifa. Inasikitisha sana mtu anapomliganisha huyo Pofesana na Waziri Mkuu. ni kichekesho cha hali ya juu.Mzee wa facts and figures ni moto wa kuotea mbali .... Kwa mdahalo wa last week ata ungefanyika Kwenye office ya Dr Mengi jamaa angeibuka kidedea.... prof: Muhongo ni mtu makini wa siyo wa kubeza kirahisi rahisi