Pinda aingia mitini, ashindwa kukutana na wahadhiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda aingia mitini, ashindwa kukutana na wahadhiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 16, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Pinda aingia mitini, ashindwa kukutana na wahadhiri
  • Wanafunzi Kitivo cha Elimu wamteka DC

  na Danson Kaijage, Dodoma


  [​IMG] WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ameshindwa kumaliza kiu ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa madai kuwa hakuwa vizuri kiafya.
  Taarifa iliyotolewa kwa wahadhiri hao na Waziri wa Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema kuwa Pinda alishindwa kukutana na wahadhiri hao kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
  Dk. Kawambwa alisema pamoja na wahadhiri hao kuwa na kiu ya kutaka kukutana na Pinda ili kutatuliwa matatizo yao, lakini alishindwa kuonana nao kutokana na kuumwa.
  Aidha, katika ratiba yake, Pinda alitakiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya chuoni hapo, ambayo yamekuwa yakionekana kuwa ni kero kubwa, ikiwa ni pamoja na kuangalia miundombinu ya maji, hali ya mabweni na wanafunzi kushindwa kupatiwa fedha za mikopo kwa wakati.
  Katika msafara huo, wanafunzi wa Kitivo cha Elimu chuoni hapo waliteka msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, John Tupa, kwa saa tatu, ikiwa ni hatua ya kutaka kumshinikiza Waziri Pinda kuweza kuongea na wanafunzi hao.
  Kutokana na hatua hiyo, wanafunzi hao walitoa upepo gari la mkuu wa wilaya, jambo lililosababisha kushindwa kuambatana na msafara wa Pinda kwa wakati.
  Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa wataalamu wahadhiri katika chuo hicho, Paulo Louisulie, alisema wamekubaliana na maombi ya Pinda kwa kumtuma Waziri wa Elimu kuhusu kushindwa kwake kuonana na wahadhiri hao.
  Mwenyekiti huyo pia alidai kuwa pamoja na kutoweza kuongea nao lakini wanamsubiri kwa kesho (leo) na wanachotegemea zaidi ni kuona jinsi gani wataweza kufikia muafaka juu ya madai yao .
  Wahadhiri hao walidai kuwa hata wakikutana na Pinda hawataweza kuingia madarasani hadi walipwe fedha zao.
  “Kwa sasa tunashughulikia haki yetu na si maneno yasiyo na msingi, ambayo yatatushawishi kuingia madarasani,” alisema.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa viongozi mbona hivi...............................hata AG alikwepa kongamano la katiba mpya akidai anaumwa....................
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Pale ni maji marefu mkuu kashaona hawezi ndo maana kakimbia!
   
 4. l

  lazaro New Member

  #4
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sio kucheleshewa pesa za mikopo tu bali bodi ya mkopo imetuzulumu pesa za field mwaka jana kwa kigezo cha kutodaiwa baadae kitu ambacho ni ufisadi ,piatatizo la maji ni kbwa zaidi mpaka infika wiki maji hayatoki na kuna vyoo vya kuflash wanafunzi wanatumia muda mrefu kutafuta maji badadla ya kuingia madarasani na kusoma,hudma mbovu za afya inafika kipindi mpaka wanachuo wanalazimika kukodi magari kupeleka mgojwa hospitalini,tena cha kuhuzunisha zaidi hakuna vipimo dhabiti katika hospital za chuo ingawa wanafunzi wanatozwa Tshs LAKI MOJA YA MATIBABU.pia wanachuo cha dodoma pamojana wahadhiri hawamtaki prof mlacha kwa kile kinachodaiwa kuwa ni chanzo cha migogoro yote katika chuo cha dodoma maana anatafuna pesa za wanachuo kwa kuwalazimisha walipe pesa nying kuliko kawaida yake na kukataa kuzirudisha pindi wanachuo wanapozidai pesa zao
   
 5. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Aliogopa kulia tena mbele ya wahadhiri na wanafunzi...
   
 6. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Si angefika tu alie,ana machozi ya karibu huyu pm,,,,,,,,,,,
   
 7. B

  Baba Tina Senior Member

  #7
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Leo ameenda na kikao na wahadhiri kinaendelea sasa nasikia kiko hot sana.
   
 8. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sasa kama alikuwa anaumwa ameenda Dodoma kufanya nini? Hii ni kuchezea pesa zetu tu.
   
Loading...