Tatizo ni zaidi ya overloading. Tatizo ni viwango vya barabara zetu. Ujenzi wa Highways ni tofauti na ujenzi wa barabara za mitaani ambazo zina viwango vya magazi yasiyo zidi tani 5-10. La msingi hapa ni kuhakikisha wakandarasi wanachaguliwa wenye viwango vya hali ya juu katika ujenzi wa barabara zetu. lakini pia, wanainchi tuko wapi? iweje tukubari kupewa barabara chini ya kiwango? Na huyo waziri au mwakirishi wake anapokwenda kufanya ufunguzi wa hizo barabara, huwa wanajua wanachokubali kukipokea? Ndugu wa Tanzania wenzangu. Tufike maali tutambue kuwa, pesa inayoutumika katika ujenzi wa barabara hizi ni zetu walipa kodi. Basi, kama haturiziki na viwango, tusikubali hizi barabara zifunguliwe na sisi tukiangalia tuu. WATANZANI TUACHE KUONGEA BILA VITENDO. TUACHE KULALAMIKA WAKATI KATIBA INATUPA HAKI YA KUFANYA CITIZEN ARREST...
Mimi ni Mhandisi (Engineer) naomba niwaeleweshe nini kinaendelea ktk barabara zetu tunazozijenga kwa gharama kubwa:
1. Barabara ina design yake ya kuhimili mzigo (pavement design)hivyo basi uzito wa magari hutakiwa kuzingatia uwezo wa barabar yenyewe ndo maana kukawa na mizani
2. Ujenzi wa barabara zetu hufuata maanadalizi, maadili na taratibu zote za kihandisi, ndiyo maan utaona barabara ikishakamilika kujengwa huwekwa katika kipindi cha uangalizi/matizamio kisichopongua miaka miwili, ikitokea barabara ikaharibika basi mhandisi mshauri na mkandarasi watawajibika kurudia ujenzi wa barabara husika kwa gharama zao, mfano ni ile barabara ya Kilwa. Hivyo ni vigumu sana kujenga baraba chini ya kiwango.
3.Nchi zilizoendelea hujenga barabara zake na tena zenye ubora kuliko zetu (Asphalt Concrete) ni tabaka la lami zuri kabisa. Katika barabara zao uzito ni mdogo ukilinganisha na sisi, mfano Marekani ni tani 36.2, Uingereza tani 40, Ujerumani tani 40, Ufarasa tani 40, Urusi tani 38, lakini kwa Tanzania ni tani 56 ambacho ni kiwango kikubwa sana.
4. Kuna utafiti umefanyika hapa Tanzania na umeweka wazi kuwa barabara zetu zinaharibiwa na wafanya biashara wasioitakia mema nchi kwa kuwa wanatumia tairi zijulikanazo " Super Single Tires" ambazo ni adui mkubwa sana kwa uharibifu wa barabara, simple physics, Pressure between two surfaces "the smaller the area the greater the pressure" malori mengi sana wa hao wafanyabiashara yana hizo tairi na bado yanazidisha uzito wewe unategemea nini kwa barabara iliyojengwa kuhimili Dual Tires (Tairi mbili kwa pamoja). Hapo barabar zitatoboka na ndicho hicho mnachokishuhudia ktk picha, na bado yatatokea madhara makubwa kuliko unavyoona kama serikali itaendelea kuwakikingia kifua wafanyabiashara waroho kuzidisha uzito.
5. Hitimisho, Serikali itafakari upya kuzuia kuwadhibiti wasafirishaji (Transporters) kwa kutumia sheria namba 30 ya mwaka 1973 ya usalama barabarani. La sivyo barabara tunazozijenga si lolote zitakwisha harahaka sana na wala tusisingizie eti zimejengwa kwa viwango duni- never!!!