Pikipiki kali na imara sana 2026 ni Haojue express na Tvs 125

jay-millions

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2015
Posts
4,475
Reaction score
11,470
Kama unahitaji pikipiki kwa usafiri binafsi au kubeba abiria chukua Haojue Express Plus au TVS 125
Na ukihitaji pikipiki ya kubebea mizigo shambani chukua Haojue 125 Mninga utafurahia usafiri wako, nimependekeza hizo kwasababu zifuatazo
1. Ni rahisi kuuza hata ukiwa umeitumia kwa mda mrefu
2. Ulaji mdogo wa Mafuta
3. Upatikanaji mzuri wa spea hadi vijijini
4. Mafundi everywhere
5. Bei yake ni rafiki 3M
Screenshot_20260222_200138_Instagram.jpg
 
Hii pikipiki vijijini inakubalika mno. Magunia ya mpunga inabeba wakulima wanaipenda. Mwenyewe nilienda na jamaa shambani kwake kuna maji mengi ila hii ikapita nikainyooshea mikono. Nilikuwa nashangaa wanapakia magunia wanapita nayo kwenye matope.

Nadhani Haojue wakileta dirt bike muundo kama Yamaha DT series watauza maana Sinoray haijawa na review nzuri sana na Yamaha ina bei wengi hawamudu. Hongli inajitahidi kidogo kwenye dirt bikes.
 
Kuna watu wanabebea kg 400-500 za mchele. Hapa ifakara na mangula. Hoajue ni nyoko.
 
Boss nyanda za juu kusini mnyama ni kinglion tu,hakuna cha sinoray,sanlg,tvs wala haoujue... Kwanza haoujue huku kwetu ni mayai sana hazimudu kabisa mazingira haya
 
  • Thanks
Reactions: Lax

Kinglion ina nguvu ila inachakaa mapema na kelele nyingi kwa injini, ina vibration na value for resale baada ya matumizi ni ndogo ukilinganisha na haojue mninga
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Boss nyanda za juu kusini mnyama ni kinglion tu,hakuna cha sinoray,sanlg,tvs wala haoujue... Kwanza haoujue huku kwetu ni mayai sana hazimudu kabisa mazingira haya
Mnanunua haojue ipi?
 
Back
Top Bottom