Pigo la UKAWA linalofuata ni kujiondoa rasmi CUF

Pigo la UKAWA linalofuata ni kujiondoa rasmi CUF

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
22,476
Reaction score
21,046
Mark my word kilichobakia muungano wa CUF na chadema ndani ya UKAWA ni mtu mmoja tu basi ,tena amebakia kiroho ila kisheria ni CHADEMA,tamko rasmi la kutokumuunga mkono rasmi Lowassa linakuja linapikwa liko njiani ,hii inatokana na ukiukwaji wa makubaliano wa hali ya juu wa CHADEMA kuendelea kung'ang'ania majimbo ambayo mwanzo walikubaliana waachiwe CUF na NCCR Mageuzi,pili kutokuwa na msaada wowote wa kampeni kutoka kwa mmiliki mpya wa CHADEMA yaani Lowassa.

Hofu imetanda zaidi vyama hivyo kutokujiweza kisiasa baada ya uchaguzi ,kwani uwakilishi wao wa ubunge na kukosekana kwa uwakilishi wa Rais kunainyima fursa ya kutokupewa nafasi ya kuteuliwa wabunge wa viti maalum bungeni ambayo kimsingi CHADEMA lazima wateuliwe wengi na kusababisha vyama vya CUF na NCCR kukosa Ruzuku ya kuendeshea vyama vyao.

Hongera sana Agent mkuu wa CCM Mbowe kwa kuua upinzani Tanzania ,its only a matter of time.
 
Hivyo vyama vinavyounda ukawa havipaswi kupewa nchi! yaani umoja ambao haupo smart sijui wanaweza kudeal vipi na kagame, au uhuru! kama just mbowe mwenye certificate ya form iv tu anawaghiribu sioni ni jinsi gani kagame au museven or kenyata wakiwatapeli wanaweza kutoka!
UKAWA ni wa kuogopwa kama ukoma!
 
tena wajitoa ndio watakuwa wametusaidia:
a)ununuzi wa wana cuf utakuwa hauna impact kwa ukawa directly au indirectly
b)tutakuwa na kazi ndogo ya kuwanadi wana cuf wenye misimamo badala ya hao mamluki
c)ata akijitoa lowasa,ccm out
 
Mtatunga sn lkn jioni hii mbowe na twaha wa cuf waliokuwa kwenye shrh za idi na wako pmj
 
Viongozi wakuu wa umoja wa katiba ya
wananachi UKAWA wakiongozwa na
mwenyekiti wa chama cha Democrasia na
maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE
pamoja na makamu mwenyekiti wa
CHADEMA Profesa SAFARI na kaimu
mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF
ambaye pia ni mbunge wa bunge la Africa
mashariki Mh TWALHA TASLIMA leo jioni
wamehudhuria Baraza la kuu la idd
lililoamndaliwa na Taasisi za kiislam
Tanzania shughuli iliyofanyika katika hotel
ya LAMADA Jijini Dar es salaam.
Katika shughuli hiyo ambayo iliambatana na
dua mbalimbali pamoja na hotuba za
viongozi mbalimbali pia walialikwa
wagombea urais wa vyama vyote Tanzania
lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kufika
huku mgombea wa UKAWA akiwakilishwa na
Mh FREMAN MBOWE.
Mh mbowe alipata nafasi ya kutoa Hotuba
fupi ambayo iliwagusa mamia ya waislam
ambao walikuwa katika shughuli hiyo na
hapa nimekunukulia baadhi ya mambo
ambayo mbowe aliyazungumza na kushtua
wengi
1-Nashukuru sana kwa ukaribisho wa
shughuli hi,mgombea wetu ndugu EDWARD
LOWASA alitamani kuwa nasi jioni hii lakini
kutokana na ratiba ya kampeni kubana
imebidi aunganishe kwenda kwenye
kampeni za kesho huko manyara-- MH
MBOWE
2-Swala la mashekh ambao wapo jela bila
hukumu yoyote,tulisema siku ya ufunguzi
wa kampeni na tunaendelea kusema kuwa
tumewaagiza wanasheria wa chama chetu
kufwatilia kwa makini na kuona nini hasa
kimetokea kwao kama kuna mahali
kunahitajika msaada wa kisheria tupo tayari
kulishuhulikia hilo kwani sisi lengo letu ni
kurudisha umoja na mshikamano Tanzania.
-- MH MBOWE
3-Zimebaki siku takribani 30 sasa kabla ya
watanzania kufanya maamuzi halisi,ni muda
wa maamuzi ndugu watanzania. -- MH
MBOWE
4-TANESCO imefilisika na watanzania wengi
hawajui hili,sasa shirika la umeme halina
hata sent na wameamua kufanya mgao wa
kimya kimya lakini ukweli ni kwamba huu
mgao ni mkubwa sana huko tuendako kwa
sababu hawana hela na wanaficha
ukweli,kuna mgao mkali sana sasa wa kimya
kimya na utaendelea kuwa mkali kadiri siku
zinavyokwenda. -- MH MBOWE
5-Kuna wizi mkubwa sana wa mafuta
Tanzania na kuna baadhi ya watu wakubwa
wanauratibu wizi huo,Tanzania ina akiba ya
mafuta hadi mwezi wa 11 lakini serikali
imetoa hati ya kuingiza mafuta nchini
ambapo baadhi ya wahusika ni familia ya
Rais KIKWETE. -- MH MBOWE
6-Serikali yetu ya awamu ya tano sio serikali
ya visasi kama inavyodhaniwa,ila ni serikali
ya kuwarudisha watanzania pamoja kwa
maridhiano,na maelewano,ila kuna watu
itabidi washughulikiwe kwa mijibu wa
sheria kutokana na kuligharimu taifa hao
tutafanya hivyo. -- MH MBOWE
7-Tume ya uchaguzi ya miezi miwili iliyopita
sio tume ya sasa,mwenyekiti yupo ila
watendaji wengi wameondolewa bila sababu
za msingi. -- MH MBOWE
8-Mtendaji mmoja mkuu wa tume juzi
tumepata taarifa kuwa ameondolewa na
kupelekwa kusikojulikana na amerudhishwa
na kutakiwa kukabidhi ofisi mara moja. --
MH MBOWE
9-Tume ya sasa inaongozwa na wanajeshi na
usalama wa taifa,mimi mbowe ndio nasema
kama kuna mtu anabisha waje wanikamate
leo,hatuwezi kuvumiliana kiasi hiki ni
wakati wa kuwekana wazi ili watanzania
wafanye jambo wanalolitaka. -- MH MBOWE
10-Nasema hivi hatutakubai hujuma hizi
ambazo zinaendelea sasa tutasema hadi
mwisho. -- MH MBOWE
11-Mwisho kabisa nasema hivi ni wajibu
wetu kutafuta kura,kupiga kura na kulinda
kura hivyo ndugu zangu waislam nawaomba
tushirikiane katika hili,ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA-- MH MBOWE
Share
 
Ccm msihangaike mkatoa roho bure. Mlishaanzisha propaganda ya naibu katibu mkuu wa cuf kuongea na press leo lakini ikawa uongo. Unavyosema cuf haisaidiwi kampeni je wameanza kushiriki uchaguzi leo? Na ni wapi chadema wameng'ang'ania jimbo?...Kama mabadiliko yanakuja yatakuja tu hata mfanyeje. Mmeshaambiwa Yesu na Mtume walipingwa sana lakini leo dini zao zipo
 
Hawawezi kujitoa kwasababu hata hivo viti walivonavyo watavipoteza kama wakijitoa nadhani umeona jinsi lowassa alivyowasafisha huko kina kundambwanda bado mbagala na kigamboni ,segerea na atakwenda temeke, nje ya umoja hawataweza game la ma ccm
 
Watanzania ni watu waoga wa challange. Kila kitu wanaona ni pigo na matatizo. Hizo ni challange na changamoto watu strong wanapambana nazo na kusonga mbele. Mgano mmeona lipumba, slaa waliondoka lakini watu wanasonga mbele. Watu ka nyinyi ndo wale mkiwa na watoto akiumwa kidogo mnakimbia kwa sababu nyie kwenu challenge ni pigo
 
Ngumu mno kuyaamini uyaandikayo ni ngumu mno...
 
Ujinga ni kufikiri UKAWA ni ya viongozi wa vyama vinavyounda ukawa!

Ukawa ni watanzania wataka mabadiliko tuko zaidi ya million 10...

Endelea na propaganda zako, nahis buku 7 ndo inakuweka mjini.

Wewe kwenye ukawa ni sawa na shabiki wa Azam, anachagiza ushindi ila hana ushawishi wala 'say' tofauti na shabiki wa simba kama 'Mpira pesa' au shabiki wa yanga.
 
afadhari wajiondoe ili na mgombea mwenza wao wamchukue .na uchaguzi usimame uanze upya mwakani kwani nahisi ukifanyika sasa tutachapwa
 
hata huyo lowassa aseme amejiondoa, akengeuke anunuliwe, tutampigia kura kwa sababu haya mabadiliko si ya lowassa ni ya watanzania
 
Mark my word kilichobakia muungano wa CUF na chadema ndani ya UKAWA ni mtu mmoja tu basi ,tena amebakia kiroho ila kisheria ni CDM,tamko rasmi la kutokumuunga mkono rasmi lowasa linakuja linapikwa liko njiani ,hii inatokana na ukiukwaji wa makubaliano wa hali ya juu wa chadema kuendelea kung'ang'ania majimbo ambayo mwanzo walikubaliana waachiwe CUF na NCCR mageuzi,pili kutokua na msaada wowote wa kampeni kutoka kwa mmiliki mpya wa chadema yaani lowasa
Hofu imetanda zaidi vyama hivyo kutokujiweza kisiasa baada ya uchaguzi ,kwani uwakilishi wao wa ubunge na kukosekana kwa uwakilishi wa Rais kunainyima fursa ya kutokupewa nafasi ya kuteuliwa wabunge wa viti maalum bungeni ambayo kimsingi Chadema lazima wateuliwe wengi na kusababisha vyama vya CUF na NCCR kukosa Ruzuku ya kuendeshea vyama vyao
Hongera sana Agent mkuu wa CCM mbowe kwa kuua upinzani Tanzania ,its only a matter of time

Kumekucha tena makamanda.

Itakuwaje na Mzee Duni akiamua kurudi kwao??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom