WanaJF,
Katika hali ambayo imeshtua uongozi wa CHADEMA taifa ni baada ya aliyekuwa mgombea wa makamu wa urais CHADEMA, Babu Duni kuikacha CHADEMA na kutimkia CUF!
Uongozi wa kitaifa wa CHADEMA umekuwa ukifanya vikao vya dharura kumsihi babu Duni abakie CHADEMA ingawa juhudi zao hizo hazikuweza kuzaa matunda na hivyo kufanya babu Duni aitupilie mbali kadi ya CHADEMA.
Pole Mbowe na fisadi Lowassa.
Unashindwa kutolea macho majipu ya serikali yako ya Chama Cha Majipu,unahangaika na Chadema.Uwepo wa Mh.Duni Haji Chadema ni matokeo ya katiba mbovu ya nchi isiyoruhusu muungano wa vyama.Duni haji ili kukidhi matakwa ya kikatiba,ilimlazimu ahame chama chake ili aweze kuwa mgombea mwenza wa Ukawa.
Yeye si wa kwanza,hata makamishna na watumishi wote wa tume ya uchaguzi kabla ya kutekeleza majukumu yao,hula viapo vya kukana uanachama wao wa vyama na kutunza siri.Kiapo hicho hakiondowi ukweli kuwa watumishi hao ni wanachama na wakeleketwa kindakindaki wa vyama vyao.
Uwepo wa Mh.Duni Chadema haukuwa na maana nyingine zaidi ya kutimiza matakwa ya kikatiba ili kuunganisha nguvu ya kupambana na Chama kilicholea majipu kiasi cha majipu hayo kugeuka Kansa inayoutafuna mwili nzima yaani serikali ya CCM.
Ngariba wenu wa majipu naye ni jipu,anapaswa atumbuliwe,hivyo sarakasi za kutumbuana majipu ni maigizo ya kawaida ya Chama cha Majipu.Ufisadi na ubadhirifu wa mali za Umma ni uti wa mgongo wa Serikali ya Chama Cha Majipu(CCM),hivyo kuuondoa uti wa mgongo katika mwili ni sawa na kuuua mwili wote.
Ni watu wa aina yako tu wenyewe uwezo wa fikra unaoishia mwisho wa pua zao,ndiyo wanaoweza kujaribu kuwaghiribu Wadanganyika kwa upumbavu kama huo ili kuwahamisha kwenye mjadara wa kushindwa kwa Serikali ya CCM.
Majipu ya serikali na watendaji wake,ni kielelezo cha mchoko wa CCM katika kutatua changamoto za wananchi,ni uthibitisho wa kauli ya Mh.Kingunge kuwa CCM imeishiwa pumzi.Leo hii ni rahisi kuuhubiri ukweli bila kutumia zana kuwa tangu enzi za Mkapa na mtangulizi wake,Tanzania haikuwa na serikali,badala yake ilikuwa na mkusanyiko wa waharifu wa kiuchumi waliokusanyana pamoja chini ya mwamvuli wa CCM na kupewa ridhaa na wanaccm wapumbavu kwa ujira wa chumi,viberiti,kofia tisheti na kanga ili waweze kupora utajili wetu na kujilimbikizia wao.
CCM na wapumbavu wote waliouweka utawala wa CCM hawawezi kujinasua katika kashifa za majipu yanayoibuka sasa katika sehemu zote za mwili wa serikali.Uzuri wa haya ni kwamba,yanadhihirika wakati ambao waliojivika upambanaji wa ufisadi- Mwakyembe na Sitta,wamewahi kuhudumu kwa nyakati tofauti katika eneo hilo la Bandari lenye majipu sugu.
Uko wapi uadilifu wa Naibu spika,ikiwa alipokuwa akihudumu kuna Mijipu inayotishia kuifunika bahari ya Hindi kwa Usaha?Hiyo ndiyo CCM mliyoipenda wenyewe,chaguo lenu wenyewe na sasa ngoja muisome namba mliyoshirikiana kuiandika wenyewe.
Ni aibu sana kuwa mwanachama wa chama cha majipu.Kuwa mwakilishi uliyetokana na kuchaguliwa na wanamajipu ni fedheha na kielelezo cha kutojitambua.Tunangoja kwa hamu bunge lijalo,tutashuhudia wawakilishi wa mijipu watakavyokuwa wanashindana kupiga kelele za Ndiyooooooo na kupiga meza bungeni,poleni sana wanachama wa majipu na mijipu yenu.