Ndugu wana jamiiforums. kichwa cha habari kinajieleza vizuri. Tuna shida katika kujenga hoja, ila tuko vizuri katika kutoa maoni. Na hii ndiyo concern yangu katika post hii. Watu wengine, kwa mfano, wakitoa maoni yao kuhusu jambo fulani, wanataka uwaamini kwa asilimia 100 kwa hilo jambo wanalokwambia. Kwa mfano
Ukiuliza wana uhakika gani na jambo hilo, most likely watauliza: "kwa hiyo huniamini?" Lakini wewe ulitaka tu ku'verify' akupe vyanzo vya taarifa yake ili na wewe uweze kutafuta ukweli kuhusu jambo uliloambiwa.
Lakini matokeo yake, unakuta unaingia mgogoro na mtu wako wa karibu kwa kudhani humwamini, na unaanza kusikia habari ofisini au sehemu nyingine kwamba "huyo ni mtu mkubwa hukupaswa kumuuliza a'verify' taarifa anazokupa." By the way, mimi kwa mfumo wangu wa elimu nilioupitia siku za huko nyuma, nimeweza kukubali kanuni ya Rene Descartes. Alikuwa French Mathematician, scientist and philosopher.
Hivyo, the likelihood ni kwamba mtu akisema jambo fulani mbele yangu, lazima niulize "how do you know?" Lengo sitaki kulishwa matangopori. Je, na wewe ulishawahi kukabiliana na situation kama yangu, na je wewe huwa unafanyaje Concretely, mtu hawezi kuja kwangu na kuniambia "mkeo anachepuka" nikamwamini.
Ingawa inaweza kunisaidia kuchunguza kwanza kabla ya kuamini hivyo kwa sababu kuna mambo mengi nilishaamini ambayo si kweli, na kuna baadhi sikuamini na yakawa kweli. Kwa hiyo, ndiyo maana kwangu verification ni jambo muhimu sana.