Mimi naona nina bahati mpwa. Karibu kila kitu ninachotumia hapa ghetto kaninunulia yeye. Pasi, jiko, woofer, viatu ghali sana vya michezo na makorokocho mengineyo yote kanunua yeye. Na cha ajabu ni kwamba huyu binti wala siyo kwamba ana pesa sana hapana. Ni kwamba yeye anajinyima ili mimi nipate.
Binti kama huyu jamani utamfanyia nini mbali na kumkabidhi vyote ulivyonavyo, kumuenzi, kumheshimu na kumpenda kwa moyo wako wote?
By the way mpwa - hata soksi ni zawadi kubwa sana kama imetolewa kwa upendo wa dhati. Labda tu uwe una-deal na mtu ambaye hajitambui na ambaye anadhani kwamba ukubwa wa zawadi ndiyo unaakisi kiwango cha upendo.
Huyu binti hata nikimpa buku au nikimletea kipande cha nanasi basi atashukuru kwa moyo mweupe. Ni burudani sana ukipata mtu anayejielewa mpwa!
Happy Valentines Day (in advance) mpwa! 🙏🏿❤️