Picha ya kuhuzunisha sana

Picha ya kuhuzunisha sana

Sema wanafanana sana nywele zao kipili pili kinacho vutia
 
Huyu bint huyo ni mama ake mzazi ila baadae huyu bint alichukuliwa na familia nyingine yenye uwezo lkn huyo mama kila mara alikuwa akimpelekea mwanae zawadi, bint alisomeshwa hadi kufikia elimu ya chuo kikuu na akapata mchumba ambae alikuwa na pesa, bint alipompeleka kwao kumtambulisha alimtambulisha kuwa wale walio mlea ndio wazazi wake lkn wakiwa katikati ya utambulisho mara huyo mama yake mzazi akafika na kumkimbilia mtoto wake lkn bint akutaka ifahamike hivyo akamkataa na yule mama akatolewa nje na sherehe ikaendelea. Lkn baadae waliporudi mjini yule kijana alirudi tena kule mkoani bila kumjulisha yule bint na akafanya uchunguzi na kugundua kwamba yule ndie mama mzazi wa mchumba wake. Siku ya send off/harusi yule mama katikati ya sherehe akatokeza tena akiwa na mfuko wa chakula mkononi na kumfata yule bint pale mbele lkn bint akawa anapiga kelele na kumkimbia ndipo yule kijana akamshika mke wake na kuomba mic toka kwa MC ndipo alipowaomba wahudhuriaji kumsikiliza, ndipo alipowaeleza watu kwamba huyu hapa mnae muona ndiye mama mzazi wa mke wake, Yaani ndiye mama mzaa chema. Na akamshika mkono mke wake na kumueleza kuwa anafahamu kwamba huyo ndie mama yake mzazi na siku alipogundua hivyo ilisababisha ampende sana mke wake. Akamfuata mama mkwe wake akamkumbatia kisha akapokea ule mfuko na kukitoa kile chakula na kukaa high table na kuanza kula pamoja na mke wake.
 
Mbona kama anakabidhiwa yai la mbuni kwenye hiyo jamii ina maana gani hawa nadhani niile jamii ya kibushman kwa kiafrica nimesahau wanaitwa kinanani
 
Inasemekana huyo binti alitupwa na mama yake mzazi akaokotwa na kulelewa na huyo bibi ambaye Inasemekana ni chizi
Kila jambo na sababu zake huwenda kuna kitu kikubwa aliepushiwa,na kuna jambo zuri anaandaliwa Mungu hana choyo
 
Mimi hainihuzunisha ila inanifurahisha kwan maisha ya binti yameokolewa! Au kwanini unataka tuhuzunike?
 
Mimi hainihuzunisha ila inanifurahisha kwan maisha ya binti yameokolewa! Au kwanini unataka tuhuzunike?
Hapana sikutaka mhuzunike[emoji31] [emoji31] [emoji31]
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Pale ilipopatikana ile habari ni page ya simulizi za kutunga, na mimi naamini kwamba siyo 100% yale maelezo

sasa ebu lete habari za uhakika,
Rejea page 5 #49 nimeweka picha kamili mkuu.
Ni msichana wa miaka 14 akipewa yai la Mbuni na bibi yake huko Namibia
 
Rejea page 5 #49 nimeweka picha kamili mkuu.
Ni msichana wa miaka 14 akipewa yai la Mbuni na bibi yake huko Namibia
page za kitabu gani?
make kama ni JF page za device yako haziwezi kufanana na zangu, isitoshe huo ni mpangilio tu, ziwe ndefu au fupi,
tuachane na hilo, habari ulizoweka hapa zina maelezo mafupi hayo uliyosema, hazina link ya ushahidi.
jf huwa ni mtandao usio na ubabaishaji
 
Yaani vichaa kwa watoto wao wako makini sana kuna kichaa alikua akipita kwetu Na mtoto wake mgongoni mtoto mazuri very healthy Na ukitaka kugombana nae ulizia chochote kuhusu mtoto wake....
 
Back
Top Bottom