Picha: Usahili post ya Mkaguzi msaidizi wa Uhamiaji - Uwanja wa Taifa

HAMTOKI.

Pamba? Kilo moja Tsh 180! Hafu hapo hiyo high quality. Hafu unajua hadi pamba iwr kilo moja ni ujazo gani? Hahaa hah!

Hafu utahitaji kuwekeza pesa ndefu kidogo hapo. Kukod.shamba si.chini ya Hekari 5, madawa, mbegu, vibarua, aaagghh!!!
Kudaaadeki waambie hawa wanadhani kilimo lele mama. Mi nishazika 5.5 million baadae 1.4 million natamani hadi kulia.
 
Hatukati tamaa mkuu
 
Kudaaadeki waambie hawa wanadhani kilimo lele mama. Mi nishazika 5.5 million baadae 1.4 million natamani hadi kulia.

pole sana mkuu! uliingia kwenye kilimo cha aina gani? ulikuwa na vitendea kazi vya kutosha ama tatizo lilikuwa ni nini?
 
Naunga mkono hoja iliyowahi kutolewa na Kiongozi fulani Mstaafu kuwa Ukosefu wa Ajira ni Bomu linalosubiri muda ili lilipuke !!!
 
Mbona hamuongelei wenye ajira zao waliojipeleka kwenye usaili huo, tena wengine wamekubuhu kwenye rushwa.
 
Kila la kheri kwa wote walio ona majina yao, tuna amini haki itatendeka ktk mchujo huu wa mwisho.
 
Nchi imeoza kabisa..Lowassa akisema hili ni bomu watu wanambeza subirini tu kuna siku inakuja watu watakaanga pumbu za hawa viongozi watafune kwa hasira
 
Kuna mtu alisema humu kashukuru hii interview imefanyika shamba la bibi maana kaopoa demu mkali kishenzi.....utaratibu huu uendelee jamani maana ni mzuri
 
UKISTAAJABU YA UHAMIAJI UTAONA YA UTUMISHI..!!

Ck ya (ijumaa) idara ya Uhamiaji ilifanya usaili kwa jumla ya vijana 10,846 ili kupata vijana 70 tu watakaoajiriwa kama Maafisa Uhamiaji wasaidizi. Hii ilikua ni wastani wa 1/156 yaani nafasi moja ya kazi ilishindaniwa na watu 156.

Uwezekano wa kupata nafasi kwa vijana waliojitokeza kufanya usaili (probability) ilikua 0.0064.

Kwa lugha nyingine ni kwamba kila kijana aliyejitokeza kwenye usaili ule uwezekano wa kupata kazi ni asilimia 0.64% na uwezekano wa kukosa ni asilimia 99.36%.

Kwa maneno mengine ni kuwa uwezekano wa kupata kazi ni chini ya asilimia moja (possibility is less than 1%). Rekodi hii ni ya kwanza kutokea duniani.

Kabla ya rekodi hii, nchi iliyokua ikishikilia rekodi ni China. Mwaka jana kiwanda kikubwa zaidi cha nguo duniani kiitwacho China Textile Industry, kilichopo mjini Keqiao, kwenye Kaunti ya Shaoxing jijini Shanghai, kilifanya usaili kwa watu zaidi ya laki moja wakitafuta kuajiri watu 5,000 tu.

[Kiwanda hiki kina wafanyakazi zaidi ya elfu hamsini na vibarua zaidi ya laki 2 wanaofanya kazi kiwandani hapo kila siku].

Kufanya usaili kwa watu laki moja ili kupata waajiriwa 5,000 inamaanisha uwezekano wa kupata kazi kwa kila mtahiniwa (probability) ilikua 0.05.

Kwa lugha nyingine ni kuwa uwezekano wa kupata kazi kwa watahiniwa ulikuwa 5% na uwezekano wa kukosa ulikua 95%.

Jumuiya ya kimataifa ililaani kitendo hiki na usaili huu ukaingia kwenye rekodi za dunia kuwa ni usaili wa hovyo zaidi kuwahi kutokea duniani. (The world most ridiculous job interview ever happened).

Taarifa zinasema kuwa haikua haki (it was unfair) kumdahili mtu huku uwezekano wa kupata kazi hiyo ukiwa chini ya asilimia 5%. Ilionekana ni uonevu.

Vyanzo vya habari vilivyopinga usaili huo vinasema, Shirika la kazi duniani (ILO) linapendekeza usaili wa kazi uwape uhakika wa zaidi ya 50% wanaosailiwa.

Hii ina maana kuwa mtu anayefanyiwa usaili wa kazi anapaswa kuwa na uhakika wa angalau 50% wa kupata kazi wakati anapofanyiwa usaili.

Asilimia 50% maana yake ni kuwa idadi ya wasailiwa isizidi mara mbili ya nafasi za kazi zilizopo. Kwa mfano kama nafasi ni 70 unapaswa kufanya usaili kwa watu wasiozidi 140.

Katika nafasi 70, ukisaili watu 140 maana yake ni kwamba kila aliyeitwa kwenye usaili ana uhakika wa kupata kazi wa 50%. Hivi ndivyo ILO wanavyopendekeza. Yani uhakika uwe 50% au zaidi.

Na hivi ndivyo mashirika mengi ya kimataifa yanavyofanya. Kama nafasi ni 3 hata mkiomba 100 uwezekano wa kuitwa kwenye usaili (interview) ni watu 6 tu' ili katika hao 6 wapatikane watatu watakaoajiriwa (sawa na 50% ya waliodahiliwa).

Sasa Idara ya Uhamiaji wakaamua kwa makusudi kuvunja rekodi ya China na kuiweka Tanzania kwenye kilele. Wakati China ikipigiwa kelele kwa kuweka uwiano wa asilimia 5%, Uhamiaji wao wakaenda mbali zaidi kwa kuweka uwiano wa asilimia 0.64%

Hali hii iliwafanya Watanzania wengi kulaani mfumo huu wa usaili uliotumiwa na idara ya UHAMIAJI kwa sababu kuu mbili.

Kwanza ni mfumo wa udhalilishaji. Huwezi kuwakusanya wasomi kwenye uwanja wa mpira kama magunia ya vitunguu ili wafanye usaili wa kazi. Aina hii ya usaili ilikiuka misingi ya utu (it was agaist human dignity).

Pili usaili huu ulizidi kudhoofisha hali ngumu za kiuchumi walizonazo vijana hawa. Gharama za nauli (kwa waliotoka mikoani), malazi na chakula walizotumia ni wizi wa kusadikika uliofanywa na serikali (ya CCM).

Ikiwa kila kijana alitumia wastani wa 150,000/= kama gharama za nauli, malazi na chakula kwa siku alizokaa Dar, ukizidisha kwa watu 10,000 utapata jumla ya shilingi Billion Moja na milioni mia tano (1.5 billlios).

Fedha hizi ni nyingi kuliko fedha zote za miradi ya maendeleo kwenye wizara ya Afrika Mashariki. Ni nyingi kuliko madai ya askari Magereza wote nchini. Askari magereza wanadai jumla ya bilioni 1.2 ikiwa ni malimbikizo ya posho zao mbalimbali, ghamama za uhamisho n.k.

Hebu fikiria vijana wasio na kazi wala chanzo chochote cha mapato unawapora Bilioni moja na milioni mia tano, kwa kisingizio cha kuwaita kwenye usaili.!!!

Tena usaili wenyewe uwezekano wa kupata kazi ni chini ya asilimia moja (1%).!!! Huu mi uhuni na ukatili usioweza kuvumilika. Mbaya zaidi ukatili huu umefanywa kwa makusudi na serikali (ya CCM).

Lakini wakati hayo yote yakiendelea kuna kioja kingine kikubwa kimetokea. Lakini hakijasikika sana labda kwa kuwa kila mtu alikua "busy" na kioja cha idara ya UHAMIAJI.

Kioja chenyewe ni hiki. Menejimenti ya utumishi wa umma ilitangaza nafasi za kazi. Vijana zaidi ya 4,000 wakaomba nafasi mbalimbali zilizotangazwa.

Wote wakaitwa kwenye usaili. Usaili wenyewe ulikua juz (jumamosi) pale chuo cha Mwl.Nyerere Kigamboni.

Hakuna aliyedhani kama UTUMISHI wangeweza kurudia makosa ya UHAMIAJI. Lakini kilichotokea ni kinyume chake. Idadi ya watu haikua kubwa sana kama ile ya Uhamiaji lakini nafasi zilikua chache zaidi ya zile za Uhamiaji.

Kwa mfano nafasi ya maafisa maendeleo ya Jamii (Community Dev.Officers) iliombwa na watu 716, walioshiriki usaili jana ni watu 564. Lakini nafasi za kazi (vacancy) kwa maafisa maendeleo ya jamii zilikua mbili tu.

Hii inamaanisha kuwa vijana wote 564 waliofanya usaili jana kwenye nafasi ya maafisa maendeleo ya jamii, walikua wanapigania nafasi mbili tu za ajira.

Huu ni uwiano wa 0.35% au 1/282. Yani kati ya watu 282 waliofanya usaili ataajiriwa mmoja, halafu mwingine mmoja atapatikana kati ya 282 waliosalia.

Hii ni sawa na kusema vijana wote walioshiriki usaili huu kwenye nafasi tajwa hapo juu wana uhakika wa kupata ajira kwa 0.35% na uhakika wa kukosa ni 99.65%.

Hiki ni kiwango cha juu zaidi ukilinganisha na kile cha UHAMIJAJI ambako uhakika wa kupata ajira ulikua angalau 0.64% na kukosa 99.36%.

Hii inamaanisha kuwa UTUMISHI wamevunja rekodi ya dunia iliyowekwa na idara Uhamiaji. Kwa lugha rahisi ni kuwa Uhamiaji walishikilia rekodi kwa siku moja tu kisha Utumishi wakaivunja.

Hivyo basi napenda kuchukua fursa hii kutangaza kuwa Menejimenti ya UTUMISHI WA UMMA nchini Tanzania kwa sasa ndiyo inayoshikilia rekodi ya dunia ya kufanya usaili wa kazi wa hovyo kuliko usaili mwingine wowote uliopata kutokea duniani (The world most ridiculous job interview).

Hongera idara ya Utumushi kwa kupata nafasi hiyo. Pongezi kwa mama Hawa Ghasia na serikali nzima (ya CCM) kwa kutekeleza vema Ilani ya chama chenu. Ama kweli ukistaajabu ya UHAMIAJI utayaona ya UTUMISHI.
 
tatizo ni kwamba! kwanini wasinge fanya short list inayo endana na uhalisia. kama walitaka watu 70. Wangeita watu 350 tu. ila wanalao jambo kufanya vile. Sio mbaya watu waliweza kujenga mahusiano ya future husbands and wife. wafanye vijana wetu wapate wachumba wenye degree hewa.
 
Jamaa hao ni vichwa maji kweli,kusoma hawawez hata picha bas?????
Test yenyewe walikopi na kupest,c jui kama majukumu yao wanayajua,wao ni ufuska na rushwa.
Ila ipo siku........
 
Mimi upande wangu nimewashangaa sana uhamiaji mbona ule mtihani test iliofanywa ni copy ya mtihani ambao ulifanya na walioomba kazi nigeria ina maana wameshidwa kutunga mtihani its astonish !!!
 
Watu ni wengi sana na bado wanazidi kuja, kama ni mechi basi ni sawa na wale wanaoingia katika mechi za simba/yanga wanapocheza na timu za mikoani.

Ulinzi naona ni jukumu la askari magereza.

Hii nimetumiwa sijui kama ni kweli?

Matokeo ya Usaili wa nafasi za Konstebo wa Uhamiaji yaliyotolewa katika magazeti ya tarehe 23 Julai, 2014 yameonesha kuwa katika Idara hiyo watanzania wengine mbali ya watoto au ndugu wa wafanyakazi wa Idara hiyo hawawezi kupata ajiya ndani ya Idara hiyo ya Serikali. Majina ya wengi walioitwa kazini ni watoto au ndugu wa wafanyakazi wa idara hiyo.

  1. Abdulhaq Amin Mandemla – Mtoto wa afisa Uhamiaji Amin Mandemla
  2. Alphonce Kishe – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Aleluya Kishe
  3. Asha Burhani Idd – Ndugu ya Afisa Uhamiaji Tatu Burhani Idd
  4. Beatrice Temba – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Joseph Kasike
  5. Geofrey Justine Mhagama – Ndugu ya Afisa Uhamiaji Rose Mhagama
  6. Iginga Daniel Mgendi – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Daniel Mgendi
  7. Issack Michael Makwinya – mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Makwinya
  8. John Alfred Mungulu – mtoto wa Afisa Uhamiaji Alfred Mungulu
  9. Joseph A. Milambo - mtoto wa Karani wa Uhamiaji Milambo
  10. Michael J. Choma – mtoto wa Afisa Uhamiaji John Choma
  11. Shimba H Zakayo – mtoto wa Afisa Uhamiaji Zakayo Mchele
  12. Upendo E. Mgonja - mtoto wa Afisa Uhamiaji Mgonja
  13. Vaileth A. Kidesu – mtoto wa Afisa Uhamiaji Adam Kidesu
  14. Elizabeth Edward – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Edward Martin
  15. Ester Mahirane – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Mahirane
  16. Basil Lucian John – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Dismas Lucian
  17. Frank E Kajura- Ndugu wa Afisa Uhamiaji Kajura
  18. Jacob P. Ulungi – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Magnus Ulungi
  19. Janeth John Milinga – Ndugu wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Milinga
  20. Janeth R Lukuwi – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Eliza Lukuwi
  21. Joseph N. Yondani – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Mary Yondani
  22. Leila khatib Irovya - Mtoto wa Afisa Uhamiaji Abbas Irovya
  23. Lucian F. Mlula – ndugu wa Afisa Uhamiaji Dismas Mlula
  24. Neema Kasian Lukosi- Ndugu wa Afisa Uhamiaji Zubeda Abbas
  25. Pendo D. Gambadu – ndugu wa Afisa Uhamiaji Gambadu
  26. Paschalia E. Mwenda – ndugu wa Martin Edward mwenda
  27. Theresia Ernest Kalunde – Mtoto wa Ernest Kalunde
  28. Veronica G Vitalis – Mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Vitalis Mlay
  29. Victor G. Mlay- Mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Vitalis Mlay
  30. Catherine J. Mapunda- mtoto wa Afisa Lucy Mapunda

Hii ni sampuli tu yaani nimeorodhesha moja ya tatu tu kwani zaidi ya asilimia tisini ni watoto na ndugu wa Maafisa Uhamiaji.
Nadhani ingekuwa vyema wasingekuwa wanatangaza nafasi hizi bali wawe wanagawiana ndani kwa ndani.
Alamsiki.
 
Wadanganyika tumekwisha jamani. Afadhali kuishi Gaza tukajua moja.
 
aisee hatari mi nakumbuka siku moj niko tamisemi dar pale kina ktu nlikiona nkasema nchii km huna mtu imekula kwako
 
Huku sina ndugu narudi kijini nisubiri urithi wa familia. Lasivyo tutaishia kuwa nyumba kumi na kuokota vyuma chakavu
 
Back
Top Bottom