Picha rasmi ya rais na bango la baraza la mawaziri

BlueBalaa, salama?

Umesalimika kwenye mabomu baada ya mahakama?

Pole kamanda.

Sasa hili la picha za Raisi na Mawaziri vipi tena?

Unatafutia watu ban au? Ngoja nikae kimya, bado napenda kuchangia humu jamvini.
 
Literary Tanzania hakuna raisi..otherwise mambo yasingekuwa shaghalabaghala hivi kama tungekuwa na raisi
 
Hii siyo sehemu ya biashara paleka kwenye thread ya biashara. Kibaya chajitembeza.
 
Picha rasimi ya Diwani (JK), ya kazi gani kwangu mkuu?
Jamaa amepwaya utendaji wake siku hizi kama Diwani wa kata halafu anachakaa ghafla, na bado!


Hapo pekundu panahusika ndiyo maana siku hizi hapendi kupigwa picha.
 
Nini??? watoto wanalala njaa wewe unaniambia picha ya rais na baraza la mawaziri...tena uniambie ninunue?.... Ushindwe na ulegee.
 
Mi sina haraka nazo, nawasiwasi mpaka mwaka huu unaisha ninaweza kuhitaji kununua picha nyingine kwa sababu baadhi ya sura (kama sio zote) zitabadilika.
 
nitake radhi mimi picha ya kikwete na baraza lake ya nini? Ata ukinipa bure siitaki.
mwambie akwauzie watu wantafuta mabox ya kufungia bidhaa lbda watazichukua
sbabau kuweka ndani yako ni kuongeza matatizo na balaa bure
 
Niliwahi kuona katuni moja wananchi watatu wa Uganda, Kenya na Tanzania, wa uganda na kenye walikua wanasifiana kwa maendeleo maraisi wao waliyoleta maendeleo kwenye nchi zao. kwa mshangao yule mbongo alichoona chaweza kua presented katika mjadala ule ni sura ya rais hivyo alisema "WE HAVE A HAND SOME PRESIDENT" so haya ya picha yananifanya niamini tuna raisi muuza sura. tena utaambiwa MABILIONI kadhaa yametumika kutengeneza picha hizi - for what? nonsense!!:target:
 
Raisi muuza sura
 

Attachments

  • Kikwete.jpg
    Kikwete.jpg
    16.5 KB · Views: 42
rais yupi? RA,EL au huyu mgeni aliyekuja juzi?

atakuwa huyu aliyekuja juzi maana nasikia alikuwa ubungo anatest mitambo kama iko fiti kauanza kuzalisha megawati kabla hajamwaga wimo kwa mikogo ili umeme uingie gridi ya taifa ...daaah hakuna nchi ina serikali mbumbumbu kama Tanzania
 
Juzi tulikuwa kwenye hotel moja jijini tukicheck mechi ya Chelsea VS Everton, akaja Dada mmoja anauza KEYHOLDERS zenye picha ya JK. Kuna watu wa makamo watatu nilikaa nao meza moja,maskini Kilichomtokea yule dada .. aliambiwa " toaa,toaa nani anataka MIKOSI?. Kama mnataka tununue labda mtengenezeni za Slaa, siyo huyu..tumemchoka..!"... Siku-comment,Akili kumkichwa.
 
Back
Top Bottom