Ndege ya kampuni ya Coastal inayofanya safari zake kutokea Dar kwenda kwenye miji na mapori karibu yote yenye airstrips hapa nchini ikiwa imebinuka huko Kiwanja cha ndege cha Arusha baada ya wahudumu wake kukosea namna ya upangaji wa mizigo ndani ya ndege hiyo na pia kutokuweka vifaa maalum vya usalama vya kuzuia kubinuka!
Hili ni tatizo la kuchanganya Uswahili na mambo ya kitaalamu!
hii wala isingefika mbali ingeanguka kwa kushindwa kubalance ikiwa angani
Nimekumbuka mwaka 2003 ndege moja huko US walizidisha mizigo pia waliipanga vibaya
iliporuka ilianguka baada ya dakika chache
soma zaidi hapa Air Midwest Flight 5481 - Wikipedia, the free encyclopedia
Hii ndiyo shida ya waswahili wakishazoea kazi basi wanajifanyia tu bila kuzingatia utaratibu. Walidhani hiyo ni Saibaba wanajaza tu mizigo bila kuipanga kwa utaratibu unaotakikana.
Tumezoea kusikia pilot error, technical prob sasa hii itakuwa porters error....Mazoea na ile pressure ya Arusha airport mida ya saa sita ndivyo vimevimewakamata.....