PICHA na Maelezo: Yaliyojili Mkutano wa Nape na Mwigulu hapa Igunga

So Nape na vijana wake ni kama wamelaaniwa vile. Wanapingana na picha hata za mkutano wao wenyewe!!! Ukisikia kukimbia kivuli ndiko huku. Sasa Zomba anabisha nini, si alete picha zake toka studio yao ya Lumumba?

Asubuhi ya leo tarehe 9 Sept. akiwa Star TV Nape amekana polisi kuhusika na uuaji wa marehemu Mwangosi, pamoja na ushahidi wa picha za mnato, video, mashuhuda na kwa baadhi ya polisi. Hatutawaacha safari hii bali ni mpaka kieleweke kwa ukweli kujulikana na haki kutendeka.
 
Nape alikatazwa kwenda IGUNGA kibali amekipata wapi leo aliambiwa anavuruga uchaguzi

nashindwa kuamini kuwa kweli hizi ni kauli za viongozi wa juu wa chama tawala !! Kama wanajiamini kushinda kwa nini wanakata rufaa ???
 
mbona huyu inaonesha ndo alikuwa anaenda kwenye mkutano mana hapo si mazingira ya uwanja wa mkutano, mbona hajatuonesha huyo mwigulu na nape! na mbona picha ya juu kabisa kwenye jukwaa kuna mtu m1 nape na mwigulu hawapo, embu tujaribuni kuzifikiria hizi picha, hata kama tunawakosoa hawa jamaa tusije tukawa na sisi vichwa maji bure kwa mjinga mmoja kutuweke vitu ambavyo haviendani na ukweli! mbona picha za kushikiana bastola tumezipata hii ya wao kuhutubia hatuioni?

na zaidi huyo dada hapo mbele anaelekea ndo anakwenda kutafuta riziki yake kwenye huo mkutano kutokana na hizo bidhaa zake kwenye mkokoteni. mkuu INTELLEGENCIA ya wana jf haiko kimajungu majungu wala ki mabwepande mabwepande aisee!

Una maana hilo basi lilikuwa kwenye mkutano wa nape, una makengeza wewe, huyo mdada anaenda kuuza biskuti kwenye hilo basi lilosimama stendi, kama vipi hama mabwepande, halafu usitutishie kwa matusi ili tukuunge mkono.

Huhitaji picha ya nape wala mwigulu jukwaani kuamini wamepigwa doro!!
 
Rest in Peace Chama Cha Mapinduzi. My sincrere gratitudes to Nape na Mwigulu for facilitating this. Keep it up!!
 
attachment.php

attachment.php

watu waliohudhuria

attachment.php

attachment.php

Watu wakiondoka kwenye mkutano baada ya Mwigulu kutoa maneno yasiyofaa juu ya Dr. Slaa

attachment.php

Moja ya malori yaliyotumika kukusanyia watu kutoka vijijini likisubiri abiria mkutano ukiisha

Leo Mwigulu na Nape waliitisha mkutano Igunga na kutoa hutuba kwa wananchi, wameongea mengi ambayo hayakuwa na tija kwa wanachi wa Igunga na Taifa labda yalikuwa na tija kwa Chama.

Wamesema mengi lakini naorodhesha machache aliyozungumza Mh. Mwigulu:

1. Dr. Slaa ni mzinzi na alimpa mimba mtoto wa shule (baada ya kauli hii watu wengi waliondoka kwenye mkutano)
2. Wakialikwa sehemu watu wenye ndoa Dr. Slaa hatahudhuria
3. Kale kazee (Dr. slaa) kanakula kwa kutembea tembea
4. Yule mzee (Dr. slaa) wazee wenzake wamebaki majumbani wanalea wajukuu yeye kuzurura tu
5. CDM wanategemea mtaji wa mauaji katika mikutano yao ?????????
6. Hata kama uchaguzi ukirudiwa igunga lazima washinde kwani timu ni ile ile ya ushindi
7. Lengo la CDM kukata Rufaa ilikuwa ili Kafumu hasiweze kutekeleza Ilani ya CCM
8. Aliuliza wananchi eti kunakosa hata moja Kafumu kalifanya hadi kuvuliwa ubunge ( Walikaa kimya)
9. Kafumu hakufanya kosa lolote - eti kosa nyie kupewa chakula, eti kosa nyie kujengewa daraja
10. Mnamshangilia Dr. slaa wakati ameikimbia Familia
11. Mnamshangilia Kasulumbai mnajua historia yake anakotoka, Akimwangalia tu mtoto wako anakufa.

Jamani hayo ndiyo maneno ya Mwigulu, naomba tuchangie yanatija na mstakabari wa taifa hili?

Nawasilisha

Mkuu weka na picha ya jukwaani ili nifurahie kumwona Nape na Mwigulu wa zero class economist!!! Poor him, na 2015 hapati kitu!!! Zile taarabu siku hizi kwenye kampeni SSM mnapotea, be objective wazee.
 
Kwani huo mkutano ulianza saa ngapi na kumalizika saa ngapi, kwa vile thread yako umepost saa 16:53. Kama umeweza kupiga picha za watu mkutanoni, kwa nini hukuweza kupiga picha za viongozi waliokuwa wanahutubia huo mkutano ili kutoa taswira chanya. Kama hizo ndizo picha za kilele cha mkutano, basi CCM wana kazi ya ziada kushinda hilo jimbo. Kama umechagua tu sehemu ya kupiga picha ili waonekane kama hawakuwa na watu, ujumbe wako hautakuwa tofauti na kauli za watu wa CCM. Mimi nafikiri kufanya kampeni za kisiasa za uongo kama CCM kutawafanya watu wasione tofauti yoyote katika vyama.
 
Hawajui kukosa adabu vile ni kuijenga CDM bila ya wenyewe kujitambua. Nape alibariki huu upuuzi bila shaka! na JK je?
 
Kumbe mnamwongelea huyu Lameck Madelu Mkumbo also know as Mwingulu Nchemba mchumi pekee Tanzania daraja la kwanza!Ngoja tusiosoma tusiwajadilidi wasomi.
 
nadhani mda sio mrefu midomo yao itaenda upande kabisa kwa kuongea uongo na madhambi wanayoficha kuhusu chama chao
Mungu alivo mwema anazidi kuwaanika na mwishowe adhabu yao itakuwa hapa hapa duniani.
 
Ndugu yangu Gobless Lema yuko wapi,huu ukomo wa M4C utamuua njaa jamaa.
 
Back
Top Bottom