Hakika mnara wa Babeli unaporomoka kwa kasi ya kutisha.
Nitoe mfano mmoja tu kulithibitisha hilo, wakati wabunge wa Sisiem watupu kwenye BMK walipokuwa 'wakinyofoa' kila ibara iliyokuwemo kwenye Rasimu ya Tume ya Warioba, ambayo walikuwa wakiiona tishio kwa azma yao ya kuitawala nchi hii milele, vyama vya upinzani, wanaharakati na umma wa watanzania ulipaza sauti kwa nguvu sana kukemea 'mchezo' wao huo wa hatari wanaoucheza, lakini watawala wetu wakaamua kuziba masikio yao kwa pamba, wakijifanya kelele hizo hawazisikii.
Ilipotangazwa tarehe ya kura ya maoni kuwa tarehe 30 mwezi huu, umma wa watanzania napo ulipaza sana sauti zao kuwa hakuna uwezekano kwa tarehe hiyo iliyotangazwa, kuwezesha kura hiyo ya maoni kupigwa, napo watawala wetu wakajivika upofu, kujifanya hawaoni kelele hizo zinazopazwa.
Hatimaye Mungu wetu mkuu akaamua kuingilia kati kwa kumpa ujasiri mkubwa Jaji Lubuva wa Tume ya uchaguzi na akatangaza hadharani kuwa kura hiyo ya maoni haitapigwa katika tarehe hiyo 30 aliyoitangaza 'mfalme'
Hakika kabisa kwa mfano huo mmoja tu, ni dhahiri kwa sasa kuwa mnara wa Babeli unaporomoka kwa kasi ya kutisha na hitimisho lake litakuwa mwezi Oktoba ya mwaka huu!