Picha: Mnara wa Babel, fumbo linaloishi

Picha: Mnara wa Babel, fumbo linaloishi

Earthmover

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Posts
25,976
Reaction score
25,303
Limebaki kuwa simulizi na hili nalo litakuwa simulizi ilikuwa kishindo na itakuwa kishindo, kiburi na dhambi kwa jumla vinatenganisha watu wasiweze kuelewana wala kuishi pamoja.

Driving+Tour+2013-09-16+013+copy.jpg

Hilo tofali la nyuma mfano wa meza ndo Babel yenyewe, unaweza kufikiri ni majabali HAPANA ni kazi za binadamu.
 
....

Kiburi na dhambi kwa jumla vinatenganisha watu wasiweze kuelewana wala kuishi pamoja.....
 
....Mnara wa Babel ni darasa tosha kwa watawala wenzetu waliliona hilo zamani sana
 
....wamefumba macho hawataki kuona ...wameziba masikio hawataki kusikia
Hakika mnara wa Babeli unaporomoka kwa kasi ya kutisha.

Nitoe mfano mmoja tu kulithibitisha hilo, wakati wabunge wa Sisiem watupu kwenye BMK walipokuwa 'wakinyofoa' kila ibara iliyokuwemo kwenye Rasimu ya Tume ya Warioba, ambayo walikuwa wakiiona tishio kwa azma yao ya kuitawala nchi hii milele, vyama vya upinzani, wanaharakati na umma wa watanzania ulipaza sauti kwa nguvu sana kukemea 'mchezo' wao huo wa hatari wanaoucheza, lakini watawala wetu wakaamua kuziba masikio yao kwa pamba, wakijifanya kelele hizo hawazisikii.

Ilipotangazwa tarehe ya kura ya maoni kuwa tarehe 30 mwezi huu, umma wa watanzania napo ulipaza sana sauti zao kuwa hakuna uwezekano kwa tarehe hiyo iliyotangazwa, kuwezesha kura hiyo ya maoni kupigwa, napo watawala wetu wakajivika upofu, kujifanya hawaoni kelele hizo zinazopazwa.

Hatimaye Mungu wetu mkuu akaamua kuingilia kati kwa kumpa ujasiri mkubwa Jaji Lubuva wa Tume ya uchaguzi na akatangaza hadharani kuwa kura hiyo ya maoni haitapigwa katika tarehe hiyo 30 aliyoitangaza 'mfalme'

Hakika kabisa kwa mfano huo mmoja tu, ni dhahiri kwa sasa kuwa mnara wa Babeli unaporomoka kwa kasi ya kutisha na hitimisho lake litakuwa mwezi Oktoba ya mwaka huu!
 
Tunaukomboa wakati...!
 
Mnara wetu wa babel Tanzania ni katiba mpya. Tulianza vizuri akaja JK akatuchanganya lugha na sasa tumevurugika na kugawanyika. CCM kivyao, wapinzani kivyao, wakristo kivyao, waislamu kivyao na asasi za kiraia kivyao! Matokeo yake mnara(katiba mpya) umesimama kujengwa. Aliyetuvuruga ndimi ni Kikwete ambaye ndiye aliyeanzisha ujenzi wa katiba mpya vizuri, akateua tume ikafanya kazi vizuri na yeye akaisifia sana mpaka dakika ya mwisho. Mjadala wa rasimu ulipoanza akageuza ulimi ghfla na hivyo kuvuruga ujnzi wa katiba mpya. Sasa hivi anajuta kitu kizuri alichokianzisha na kukivuruga kimeleta mgawanyiko mkubwa katika taifa. Kila siku ni matamko kwa kwenda mbele.
 
Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokua wakiujenga wanadamu; Bwana akasema, tazama watu hawa ni taifa moja,na lugha yao ni moja na haya ndio wanayotaka kuyafanya,wala sasa hawatazuiliwa neno wanalo kusudia kulifanya. Haya na tushuke huko tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao! Mungu tuna omba utusikie na hata adui zetu Ccm ukawa chafulie lugha ili wasielewane lugha wao kwa wao!
 
Back
Top Bottom