PICHA: Mhe Tundu Lissu akiwa hospitalini Nairobi, Kenya anakoendelea kupata matibabu

Ndiyo nasikia vibya sana kwa sababu najali zaidi klk ninyi wanafiki wakubwa, wewe niambie tangu siku ya tuko umetoa msaaada gani kwa Tundu Lisu au Familia yake?
Tutatoa msaada siku mungu wenu wa Lumumba Atakapotiwa uzezeta Na MUNGU halisi,,,na stroke ina mnyemelea mungu wenu wa lumumba kwa uwezo wa Mungu,,,,
 
hakuna namna lissu atatutia courage kusimama nje HT km mvua inanyesha ili tumpe mkono kwa alikuwa akisimamia had roho yake wates wake wakataka kuitoa.

naomba iwe mkosi kwao 2020
 
Hizo ni hasira tu zinawatoka kuona jamaa mzima kweli. Usikute mlikua mnaomba aishie hukohuko. Na pia usikute mlikua mnalishwa propaganda kuwa jamaa hoi sana hatopona. Leo lzm mkameze panadol mshushe homa


Mimi kwangu hakuna tofauti yote sawa tu, kwa maana sijui kwa nini alipigwa risasi labda alistahili huwezi jua!
 
WATESI WAKE WANATETEMEKA,

WATASEMA KILA LUGHA, WATAIMBA KILA PAMBIO.

NI AIBU KUBWA IMEWAPATA.

sasa ombi langu 2020 kama ZAWADI tumpe nchi hii aitawale.

Nilisema sitapiga Kura kwa aliyofanyiwa lissu, ila nimept nguvu Mpya.

Nitasimama nae 2020 km wazo hilo litaafikiwa.
Ameeen, why not!
 
Tanzania,
Tunamhitaji Lissu awe Rais wa Tanzania 2020. Mungu hakika ana Makusudi na Mtu huyu, Watanzania Tumlinde kwa kila hali usiku na Mchana 24/7. Wanaoweza Kumnunulia Armoured Car wafanye hivyo, kama tunataka aishi nasi mpaka 2020, vinginevyo WAPUUZI waliotaka kuutoa Uhai wake, hawafurahishwi kabisa kumuona akiwa hai, watafanya kila njia! Sisi Watanzania Tumlinde Kwa nguvu zetu zote. Watu wa Namna hii hawazaliwi kila siku!! Ni Zawadi tumepewa, tuitunze!!!
Hakuna njia ipitayo fahamu za Mwenyezi Mungu.Nani Umewahi kumsikia duniani akapigwa risasi 11 zikaingia mwilini randomly akabaki hai?.Mungu alitangulia kwenye uwanja wa Dula kumuokoa Lissu.Lissu Mwenyezi Mungu analojambo unalotakiwa kulikamilisha kwa Watanzania,ndiyo maana aliuficha uhai wako mbali sana.
 
Baada ya jana Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kusema kuwa wananchi wataanza kumuona na kusikia sauti ya Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu.

Hii hapa picha yake akioneka na yupo hospitalini, jijini Nairobi.

e549d9c69c5fea4a0d7e4b2fb2646d1a.jpg

Siamini aiseee
 
Charismatic,this is Charismatic

Ni dhahiri sasa tunaweza kusema Tundu Lissu rais wa TLS anapendwa na umma ndani na nje ya nchi kuliko tulivyodhani.

Napitia mitandao ya kijamii naguswa na jinsi maendeleo ya afya ya Lissu yalivyoigusa umma wa Watanzania. Watu wamefarijika watu wameumia watu wameliona tabasamu la Lissu,watu wamemshukuru Mungu kwa ulinzi wake ulivyo mkuu.

Hili ni somo linatakiwa liwafikie wale wote waliokuwa wakimchonganisha Lissu na wananchi. Watu wakubwa na vyeo vyao wanashindwa kujibu hoja za watanzania wanabaki kumshambulia Lissu

Ni vyema kutambua pia maombi makali yanayoendelea. Maombi ya watanzania kuwakabidhi waliomdhuru Lissu kwa Mungu aweze kutoa hukumu inayostahili

Kwa chuki zenu mbichi mmefikia kiwango cha kuwakataza watu kumzungumzia Lissu? Mna Mungu nyinyi?

Mungu aliye juu ametenda kumuokoa baba wa watu mdomoni kwa wauwaji wakubwa mashetani,ameendelea kumsimamia Lissu na anaipika adhabu yenu. Malipo ni hapahapa duniani. Soon tutapata majibu ya malipo kabla mwaka haujaisha
Ashukuriwe Mungu kwa kweli
 
Ukijifanya haumpendi Tundu Lissu unajiingopea., ukifikiri kumchukia Lissu ndio uzalendo, basi unapambana na nguvu ya umma.. Picha 4 tu zimeleta balaa, vipi ikitoka sauti na video!? Mtandao utazimaa..

Hizi picha za Tundu Lissu leo.., hautaki au unataka utaziona tu.., Ukizima data unazikuta kwenye gallery, ukiwasha data unazikuta kwenye timeliness za social media zote.. Habari ni Lissu..

Administrators na moderators wote wa JF na whatsapp groups wametoa alerts za kuvunja kanuni.. Picha za Lissu zitumwe hadi mtumaji atakapochoka mwenyewe..

HURUMA; kwa watu wasiojulikana.., pia kwa wabunge na wanachama wa CCM (Nyalandu excluded), ambao hata hawakutuma mwakilishi Nairobi kumsalimia Lissu tangu anapigwa risasi hadi anaonekana hadharani.. Roho za mauti..

Anyways.., ..., nafikiri, naamini.., ndugu waheshimiwa wabunge (kutoka Kijani—kibichi) watawasilisha pole zao kwa bwana Lissu siku akifanikiwa kurejea bungeni salama... [HASHTAG]#Rohozamauti[/HASHTAG]

Picha zimesambaa kila mahali kama oxygen.., picha zingine kama Pope Francis, Video inatoka muda gani arifuu.. Maana CCM na wasiojulikana hawachelewi kuzikana hizi picha..

Mungu wetu hashindwi hata siku moja.., hakika yeye ni Ebenezer (hata sasa ametusaidia) MUNGU ni mwema kila wakati na kila wakati MUNGU ni mwema
 
Back
Top Bottom