ilikua hatari aisee!
Hebu tuone waliopitia wenzetu ili tujifunze kitu hapa.
![]()
Inadhaniwa zaidi watu 800,000 walikufa kwenye mauaji haya.
![]()
Maiti zilizagaa mitaani na mbarabarani, kwa wakati huo kila mtu aliangalia nafsi yake tu.
![]()
Nani atamsaidi mwenzake, watoto walipoteza karibia familia nzima.
![]()
Chakula hakuna,na maji yote yalijaa damu za watu.
![]()
Hata kama hatujali kuhusu sisi basi tuwatafakari watoto wetu wataishi ktk mazingira gani.
![]()
Hakuna wa kumsaidia, ni kilio chake kwa mama yake kipenzi.
![]()
![]()
Unabakwa na kisha wanakuua.
![]()
Mitaani utazika ya ndugu yako yupi uache yupi.
![]()
Watoto kuona maiti walishaanza kuzoea.
![]()
Kila sehemu ni maiti tu.
![]()
Ni vilio visivyo na msaada,wapo waliosubiri na wao wauliwe kwa maana ana alichobakisha.
![]()
Wahutu na watutsi wote ni wahamiaji.
![]()
Maiti zilikusanywa na kutupwa kwenye kaburi la pamoja kisha kijiko kinafukia.
![]()
Baadhi ya watu waliobahatika kubaki wamening'iniza picha za wapendwa wao waliokufa.
![]()
Hakuna mwenye tabasamu,ni kumbukumbu mbaya mno maana inasemekana wengine wanawajua waliowauwa ndugu zao ila wameombwa kusameheana ili maisha yaendelee mbele.
Wew unaamin watu wakiandamana ndo kutatokea mauaji ya haraiki?Ni zaidi ya hatari...Ndicho kitu ambacho baadhi wanataka kitokee...wanaandaa maandamano....watu wa nje wanasubiri waone nini kitatokea...nchi jirani huwa wanakimbilia kwetu...yakitokea kama ya Rwanda, sijui tutakwenda wapi...Kenya? Rwanda?, Uganda? Zambia? Malawi?, Msumbiji? DRC?, Burundi? sijui ...au kujitosa baharini?
Kabila lako ni lipi?Hakuna binadamu namuhanya kama mhutu...sitaki hata salamu yake!!
Wew unaamin watu wakiandamana ndo kutatokea mauaji ya haraiki?
Mkuu mbona umejifungia kwenye box?Duh, kazi ipo kweli kweli kwa comments za aina hii...I can just imagine wewe ni mtu wa aina gani kwa kuandika haraik badala ya halaiki...lakini to put things straight hata mauaji yale ya Rwanda hayakuanza kwa ghafula...Yaani watu wanaanza kuuana tu, haiwezekani ikawa hivyo...chuki zilianza kidogo kidogo au pole pole na pengine kwa muda mrefu....Sasa wale wanaoandaa maandamano hapa kwetu wanajenga mazingira mabovu ya mahusiano nchini, chuki ndipo inapoanzia hapo...wewe unadhani katika maandamano hayo yanayoandaliwa fujo zikitokea na watu wengine kupoteza maisha, mali kuporwa majumbani, madukani na kwenye biashara siyo ndiyo misingi ya chuki na ghasia inapoanzia hapo??? Au wewe mwenzetu unaonaje????