Mauaji ya Kimbari Rwanda

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
214
229
Anaandika Mo Mlimwengu.

Yule bwana aliyesema mwenda bure si mkaa bure kuna kitu alikiona. Mgagaa na upwa siku zote huwa hali wali mkavu. Mlimwengu mimi nikaona itakuwa dhambi kubwa kwangu kufika Rwanda na nisifike kwenye eneo ambalo kuna historia ya mauaji ya kimbari.

Wakati nafika eneo la tukio nilifurahi mwenyewe nikajiona kama mtalii maana pale kulikuwa na raia wa mataifa mbalimbali ambao wanafika kupata historia. Nilipofika eneo la tukio sasa wakati naingia kwenye jumba la makumbusho nilijikuta furaha inakata bali inakuwa simanzi kutokana na historia iliyopo hapo. Tukiwa ndani ya jengo hilo niliona raia mbalimbali wakifuatilia historia ile wakati mapaji yao ya uso yamejaa machozi.

Mlimwengu mimi nilikuwa makini kupata historia kamili dhidi ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Historia inaanza wale wanyarwanda wakati wanatawaliwa na mjerumani walikuta jamii zao zinatawaliwa na wafalme wa kitusi na baada ya vita ya pili wakatawaliwa na wabelgiji. Sasa wabelgiji walitumia watawala wale wa kifalme kuwatawala wanyarwanda wenzao. Mbelgiji aliwagawa ikaonekana kama jamii ya watusi wao ni bora kuliko wahutu. Hii sumu ikatengenezwa na kutengenezwa na wao wakaibeba.

Baada ya kupata uhuru wanyarwanda walitengenezewa kadi ambazo ni kadi za kitaifa zilikuwa zinaonyesha huyu ni mtusi au ni mhutu. Wakati sumu inatenegenezwa kumbuka wahutu walikuwa wengi na wao walionekana kama ni jamii yenye kudharaulika na na jamii zingine. Shaaban Robert aliwahi kusema ipo siku mawe yatasema kitu. Sasa jamii ya wahutu ikaanza kupata elimu na kuanza kudai haki yao ya kuheshimiwa na kuchukua nafasi za juu kwenye uongozi wa serikali yao.

Mara paah timbwili likaanza 7 April 1994 na lilikuja kuisha baada ya siku 100. Kitu kibaya inakadiriwa watu zaidi ya laki nane walipoteza maisha, haikuishia hapo watu zaidi ya milioni mbili walikuwa wakimbizi kwenye mataifa jirani na Rwanda, haijashia hapo wanawake zaidi ya laki mbili na nusu walibakwa na haikuishia hapo na wengine waliweza kupata maambukizi ya UKimwi. Kumbuka hawa watu ni jamii moja wanaongea lugha moja lakini kuna sumu ikapandikizwa kwamba huyu ni mhutu na huyu ni mtusi wakaanza kuuana. Wengi walipata ulemavu wa kudumu, familia zilitengana na watoto wengi walibaki yatima. Jamani vita ni mbaya isikie tu kwa wengine.

Tunaposema maridhiano ya kitaifa lazima tusimame kwelikweli. Wasijitokeze watu wakatugawa kwa makabila yetu wakatugawa kwa dini zetu wakatugawa kwa rangi zetu. Rwanda walikuwa ni ndugu kabisa wengine walikuwa wameoana lakini pale chuki ilipopandikizwa waliuana kinyama pasipokujali huyu ni jirani yangu au ni ndugu yangu.

Leo hii Rwanda wameishasahau hicho kitu leo hii hakuna mtusi wala mhutu ila kuna mtu anaitwa Mnyarwanda na huo ndio utaifa wenyewe. Mungu ibariki Afrika na Mungu wabariki watu wake.

Mohamed Ismail Rwabukoba
Katibu Hamasa wa Vijana na Chipukizi UVCCM (W) Muleba.

#mlimwengumimi
#mauajiyakimbari
#afrikakwanza

20230715_185102.jpg
 
View attachment 2697841

Naona una bwabwaja ebu tuoneshe safu nzima ya uongozi, jeshi, wafanyabiashara wakubwa na position muhimu nani wapo?
ungenambia burundi ningekuelewa
 
Aisee inauma sana.
Mauaji ya kikatili dhidi ya wanawake na watoto..kuna watu wamelala makaburini, lakini wameteseka mno kabla ya mauti kuwafika.
 
Back
Top Bottom