lowassa aja arumeru na kupokelewa na pikipiki zaidi ya 100, magari zaidi ya 50, mabus na malorry.. watu wanashangilia na kupiga kelele kama lowassa ndo mgombea,huku arumeru hakutoshi, barabara zimefungwa, ameingia kwa aina yake.
lowassa ameingia jukwaani na kukishukuru chama, viongozi wa chama, wabunge, na wananchi woote kwa nafasi aliyopewa. akasema amekuja kumnadi sioi na sio kutoa matusi.
akawakumbusha wameru historia ya jafet aliyepigania arumeru mpaka UN miaka ya 52-54 na kuja kushinda ardhi yao, pamoja na kuingia kwenye chama cha Tanu ambacho sasa ndio ccm na akasisitizia hakuna mtu anaweza kuwadanganya leo wala kubadilisha mawazo yao juu ya ccm kwa walipigania uhuru pamoja.
akaongelea kero za ardhi kwa arumeru na kuwaambia wananchi kuwa 'sasa tatizo la ardhi arumeru limekwisha kama ukimchangua sioi sumari na kwamba rais wetu kikwete ametoa eka 5000 za wananchi kurudishiwa ardhi zao arumeru' na vile vile kusisitizia kuwa wabunge wote wanaomuuunga leo mkono baada ya sioi kuapishwa, atasimamia na kusaidiwa kulimaliza swala la ardhi pamoja na maji. aelezea chanzo cha maji cha arumeru na inavyotumika mpaka monduli.
watalii wamepunguza safari za kuja arusha kutokana na maandamano na ugomvi kila siku, ndizi hazipandi bei kutokana na maandamano ya arusha mjini, upinzani wamekua watu wa fujo badala ya utendaji kazi,na wakipigiwa kura utaenezwa hadi arumeru, wamearibu na kuivunjia heshima mkoa wa arusha na hotel nyingi zinashindwa kuendeshwa kutokana na fujo.
amemaliza sasa ivi na kuondoka, natafuta wapiga picha watume picha..
watu wamemshangilia sana sana, wakina mama wanamlilia kumshika mkono na kumbusu, wengi wanashangilia wakisema 'lowassa ndio mkombozi wetu'
sasa ivi msafara wa sioi unaelekea sehemu nyingine kuendelea na mkapa.
nawakilisha... more updates to come..yoyote mwenye picha asaidie