Elections 2010 PICHA: Kikwete alivyofunika jana huko Mwanza

hata the comedy walipokuja mwanza watu walijaa zaidi ya hapa! hakuna jipya mbona? klazimisha mvuto? imekula kwao ccm
 
Ebu cheki umma ulivyo kubali yaani CHADEMA kuitoa CCM madarakani ni sawa na kuku kuzaa ndama na ng'ombe kutanga mayai....

hata id amin aliokuwa powerful hakuamni anaikimbia nchi yake wa miguu yake mwenyee, wamejaa amekuja wenyewe? wapo hapo kwa last resp
 
Hii ni pamoja na kuwalazimisha waajiri wote kuhakikisha wafanyakazi wao wanaenda kwenye mkutano huo la siyo biashara zao zitapigwa panga na kupoteza ajira kwa viongozi wa uma

Jamani hayo malori ni watu wenyewe ndo walijipanga na kuyakodi ili kwenda msikiliza raisi wao mpendwa. Kwani kuna shida gani kupanda malori???

Mi sioni hiyo kama ni sababu ya msingi.

JK anapendwa jamani...
 
Watu wameandaliwa kutoka mikoa jirani hawa.......

Mh hapana mkuu, kwa nini wahangaike na watu wa kutoka mikoa jirani wakati kuna lundo la watu Mwanza mjini? Gharama yote ya nini wakati wa Mwanza wanapatikana kwa buku 5 tu?
 
lets 31 oct, ng'ombe atakavyotaga, simply mkuyu utakavyoangushwa na panga! chadema ndiyo mpango mzima!
 
Tuseme kweli hata pamoja na malori bado JK anamvuto na yeye....

Acha utani bana!
Ile picha aliyoitumia kwenye mabango ni ya miaka mingi iliyopita, unajua ule mvuto wa mwaka 2005 umeisha kabisa! Juzi hapa nilimuona live, kachakaa kiasi, as compared to 2005.
 
Mh hapana mkuu, kwa nini wahangaike na watu wa kutoka mikoa jirani wakati kuna lundo la watu Mwanza mjini? Gharama yote ya nini wakati wa Mwanza wanapatikana kwa buku 5 tu?

HAKUNA UWONGO MBAYA KAMA KUJIDANGANYA MWENYEWE!!!!!! Tehetehe!!! Yaani hii inanikumbusha vituko vya MR. BEAN anapojitumia mwenyewe kadi za krismas ili naye aonekane wamo wakati hakuna hat jirani anaye mjali.
 
umatiwawananchikatikamkutanowakampeniuwanjawasaharajijiniMwanza2.jpg

NyomiiliyomlakiJKuwanjawaSaharajijiniMwanzawakatiwamkutanowakampeni.jpg

MsaniiBushokeakitumbuizauwanjawaSaharajijiniMwanza.jpg

NyomiiliyomlakiJKuwanjawaSaharajijiniMwanzawakatiwamkutanowakampeni2.jpg

NyomiiliyomlakiJKuwanjawaSaharajijiniMwanzawakatiwamkutanowakampeni7.jpg

wanasikiliza mziki tu hamna jingine
 
Tuseme kweli hata pamoja na malori bado JK anamvuto na yeye....

Mwanakijiji, kumbuka Kikwete ni Rais tayari. Kwa kuwa kwake Rais tu, ni sababu tosha ya watu kwenda kumuona na kumskiliza. Kumbuka mbwembwe zake za uingiaji kwenye viwanja vya kampeni, msafara wake na vitu kama hivyo. Wapo ambao wanakwenda kwenye mkutano kwa kuwa tu wanataka kuona hayo. Nakumbuka mwaka 1995, nilikuwa upande wa Mrema, lakini tulipoambiwa mgombea wa CCM anakuja kila mtu alikuwa na hamu ya kwenda kuona namna ambavyo alikuwa anasindikzwa na mapikipiki ving'ora na vitu kama hivyo. Na ukumbuke kwamba kila anakokwenda nchini ana mabalozi, wajumbe wa nyumba mia, na viongozi mbalimbali wa chama ambao wanakuwa wamemuandalia mkutano in advance.

Slaa hana hivi vitu, watu wanaokuja kwa Slaa ni wale tu wenye mapenzi mema na Slaa. Lakini wanaokuja kwa Kikwete si lazima kwamba wote wanampenda. Naamini ni baadhi tu wanaohudhuria mikutano ya Kikwete ndo wanampenda, lakini idadi kubwa imesukumwa na bongo flava na hayo mengine niliyoyataja hapo juu.
 
Jamani hayo malori ni watu wenyewe ndo walijipanga na kuyakodi ili kwenda msikiliza raisi wao mpendwa. Kwani kuna shida gani kupanda malori???

Mi sioni hiyo kama ni sababu ya msingi.

JK anapendwa jamani...

Kwenye vyombo vya moto, magari ya kawaida, mabasi tunaambiwa na wanausalama tufunge mikanda. Leo hii watu wanarusiwa kupanda malori na wanausalama wapo. Nchi ya hovyohovyo!!
 
ni lazima awe na mvuto maana kila mtu bado anamshangaa je kwa nini ameshindwa kuachia ngazi mwenyewe ?anataka hadi atolewe na wananchi,kwa hiyo usione ajabu wananchi wanataka kumwona kwa mara ya mwisho mwisho.:sad:
Tuseme kweli hata pamoja na malori bado JK anamvuto na yeye....
 
Ni aibu kwa rais wa nchi aliye madarakani kwa miaka mitano kuanza kulinganisha na kupima uwezo wake na idadi ya watu wanaohudhuria.
 
Back
Top Bottom