Picha kibao mitandaoni nini maana yake?

Picha kibao mitandaoni nini maana yake?

Kama ni mke wa mtu na sio mke wako basi haina tatizo. Mumewe hana shida
 
Album siku hizi zimehamia mtandaoni mkuu.. twanga photo
Mimi sikujua kuwa watu wanatunza picha zao humo, si unajua tena sisi wa enzi za mwalimu bado tuko nyuma kiaina kwenye haya ma issue
 
Unazionea wapi mkuu? Kama ni instagram/fb dont follow.
Si unajua tena macho hayana pazia mkuu, nazionaga fb ila zinakuwa nyingi mpaka zinakera mkuu hiyo instagram bado sijajiunga huko kwakweli maana nasikia ndio balaa zaidi.
 
Ni kama vile mwandishi ni ww ila mawazo au habari ni yangu
 
Kila mtu na maisha yake mkuu..kama ambavyo wewe hupendi kuweka picha na ndivyo na sisi tunapenda kuweka picha,so tusipangiane maisha ebooo
 
Mkuu, ninachojiuliza ni kwamba inakuaje wewe unakereka na picha anazopost mtu mwingine kwasababu zake mwenyewe?

Kwanini unawakataza watu kufanya wanayopenda wao kisa wewe hupendi? Kwani mnashea profile?

Nakushauri tu ishi maisha yako kwa style yako binafsi, ukijiuliza sana ya watu wengine utaishia kukereka sanaaaa.
 
Ni uamuzi wao kama hupendi mtu una unfollow...maisha yao pia kila mtu na uhuru wake kwenye account yake inaruhusiwa...na haina tabu.
 
I hear you mkuu! Ila ngoja wenyewe waje....nitakuwa naangalia kwa mbali mashambulizi..ha ha ha
 
Back
Top Bottom