PICHA: Jakaya Kikwete, Philip Mangula na John Cheyo wapaa kwenda Zimbabwe

Rais mstaafu Jakaya Kikwete ameondoka kwenda Harare nchini Zimbabwe kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais mteule wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa.

Rais Kikwete ameondoka leo asubuhi Agosti 26, 2018 kwenda kuhudhuria sherehe hizo zinazofanyika katika uwanja wa michezo wa Taifa Mjini Harare akimwakilisha Rais John Magufuli.
Akizungumza kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Kikwete amesema Tanzania na Zimbabwe zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kindugu.

Amesema katika kipindi ambacho Zimbabwe ilikuwa ikidai uhuru, baadhi ya wananchi wake waliishi Tanzania hasa wanachama wa Chama cha Zanu-PF na kupata mafunzo nchini.

“Baadhi ya wanajeshi wetu wameshiriki pamoja na wanajeshi wa Zimbabwe katika harakati za ukombozi,’’ amesema Kikwete.

Taarifa ya Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu aliyoitoa kuhusu safari hiyo inasema Kikwete ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na mwenyekiti wa UDP, John Cheyo.

Rais Mnangagwa anaapishwa leo kuongoza Taifa la Zimbabwe baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika Julai 30, 2018.

View attachment 847176

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe wamebebwa na ndege rasimi ya mkuu wa kaya?
 
Back
Top Bottom