PICHA: Jakaya Kikwete, Philip Mangula na John Cheyo wapaa kwenda Zimbabwe

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,551
Rais mstaafu Jakaya Kikwete ameondoka kwenda Harare nchini Zimbabwe kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais mteule wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa.

Rais Kikwete ameondoka leo asubuhi Agosti 26, 2018 kwenda kuhudhuria sherehe hizo zinazofanyika katika uwanja wa michezo wa Taifa Mjini Harare akimwakilisha Rais John Magufuli.
Akizungumza kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Kikwete amesema Tanzania na Zimbabwe zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kindugu.

Amesema katika kipindi ambacho Zimbabwe ilikuwa ikidai uhuru, baadhi ya wananchi wake waliishi Tanzania hasa wanachama wa Chama cha Zanu-PF na kupata mafunzo nchini.

“Baadhi ya wanajeshi wetu wameshiriki pamoja na wanajeshi wa Zimbabwe katika harakati za ukombozi,’’ amesema Kikwete.

Taarifa ya Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu aliyoitoa kuhusu safari hiyo inasema Kikwete ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na mwenyekiti wa UDP, John Cheyo.

Rais Mnangagwa anaapishwa leo kuongoza Taifa la Zimbabwe baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika Julai 30, 2018.

KIKWETE%2BPIC.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais mstaafu Jakaya Kikwete ameondoka kwenda Harare nchini Zimbabwe kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais mteule wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa.
Rais Kikwete ameondoka leo asubuhi Agosti 26, 2018 kwenda kuhudhuria sherehe hizo zinazofanyika katika uwanja wa michezo wa Taifa Mjini Harare akimwakilisha Rais John Magufuli.

Akizungumza kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Kikwete amesema Tanzania na Zimbabwe zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kindugu.
Amesema katika kipindi ambacho Zimbabwe ilikuwa ikidai uhuru, baadhi ya wananchi wake waliishi Tanzania hasa wanachama wa Chama cha Zanu-PF na kupata mafunzo nchini.

“Baadhi ya wanajeshi wetu wameshiriki pamoja na wanajeshi wa Zimbabwe katika harakati za ukombozi,’’ amesema Kikwete.

Taarifa ya Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu aliyoitoa kuhusu safari hiyo inasema Kikwete ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na mwenyekiti wa UDP, John Cheyo.

Rais Mnangagwa anaapishwa leo kuongoza Taifa la Zimbabwe baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika Julai 30, 2018.View attachment 847176

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamechukua nafasi ya Rais,mkewe na mpambe nadhani.
 
Inamaana hiyo ndege inawapeleka mpaka Zimbabwe na kurudi....?

Bila shaka hiyo ni ndege ya Rais...kwa hiyo Cheyo ameteuliwa ili kuonyesha Magufuli ana mahusiano mazuri na wapinzani.
Wakati ni kinyume chake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu cha kushangaza huyo Cheyo ni Mwenyekiti wa Kudumu wa hicho chama na wala sijawahi kusikia uchaguzi wala mkutano Mkuu wa hicho chama wala kumfahamu Katibu Mkuu wake lakini hatusikii makelele ya Lumumba hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli mimi huwa naikubali sana UDP, wanajua kizipiga siasa bila chuki tofauti na CUF na Chadema ninaimani UDP kitakuja kuwa chama kikuu cha Upinzani.

Tutajie na maeneo wanakotokea wenyeviti wa hivyo vyama
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom