Kafaulu na hana maumivu tena kinachotuumiza sisi ni hizi disturbing images za mwili uharibikao! Na kwanini mwisho wake ukawa hivi
Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
Daaah! Umenifanya nimtafute msichana niliyezaa nae, ila nimeumia sana baada ya kukuta hapatikani
Huyu binti amejifungua mwezi wa tano na mtoto kafanana na mimi pia ni mtoto wa kiume sasa mtoto ndo kwanza ana miezi miwili
Nimezinguana nae baada ya mvutano wa kumtoa saba(nilishawahi kukutumia PM kuhusu hili)na kwa bahati mbaya sikuweza kwenda na toka ajifungue sijawahi kwenda kumuona mwanangu, hii yote ni baada ya kuzinguana sana baadae Binti akaamua kuniblock ili nikimpigia simu nisimpate kaona hiyo haitoshi akam block mpaka Dada yangu nae akiwa akipiga simu anaambiwa namba inatumika.
Sasa siku nikampigia kwa namba yangu tofauti simu ikaita na akapokea akanijibu jeuri weeeee baadae tukaanza kuchat akaendelea kunijibu jeuri na mimi kwa hasira nikawa namjibu jeuri(nahisi hili ndilo kosa nililofanya maana siku zote huwa najizuia kutumia hasira) Mwisho akaniambia nisimpigie simu nami nikamjibu "SITAKUPIGIA"(kwa hasira)
Sasa leo nilipoona hii post yako imenibidi nitengue kauli (maana mimi mara nyingi nikisema kitu huwa nafanya kweli) nisije nikasababisha maafa bure na kusema ukweli huyu msichana bado nampenda na nilishatoa mpaka POSA kwao ninasubiriwa ni mimi tu niamue ndoa ni lini
Kuhusu huu mtifuano mpaka ndugu zake wanajua na wameshanichukulia kwamba mimi ni mkorofi maana kila msg niliyokuwa nikimtumia alikuwa akiwaonyesha ndugu zake na mbaya zaidi ndugu zake hawakuwahi kumuuliza,"imekuwaje mpaka yeye akutumie msg kama hizo?" Yaani alichokuwa anakifanya yeye ni kunifanya mimi nionekane mbaya tu basi.
Na mimi nikachukulia anafanya hivyo sababu hana mpango na mimi
Nikaamua kumwambia Dada kwamba huyu mwanamke sina tena mpango wa kumuoa na nikamwambia na huyo binti mwenyewe kwamba,"kuanzia sasa sina mpango na wewe maana siwezi kuishi na mwanamke jeuri na hata wifi yako nishamwambia"
Basi kuanzia hapo hakuna mawasiliano,
Yaani mkuu mpaka hapa ninavyoandika mwezi uliopita nilitaka kumtumia pesa ya matumizi ya mtoto ila nikashindwa maana alishasema nisimpigie simu na akili zake zilivyo mbovu naweza kumtumia kisha akanirudishia pesa yangu(alishawahi kufanya hivyo akiwa mjamzito)
Nikapata wazo nitume kwenye namba ya mama yake ila naye ameshatoa kauli zilizozidi kunivuruga kwa Dada yangu, hivyo nikaghairi
Kuna Dada yake nae pia alishawahi kunitukana hivyo nikaapa kutompigia simu milele(na iwapo nitampigia simu nafsi itanisuta pia naona kinachozidi kuwapa jeuri ni kwa sababu yule mtoto ni Damu yangu hivyo wanajua lazima nitawatafuta)
Hivi sasa hapa najishauri kwenda kwao ila ninamtumia Dada yangu awapigie simu kwanza ili nikienda nimkute huyo mzazi mwenzangu
Maana hata kama sitamuoa na kwa kuwa ameshasema nisimpigie simu(sa hivi namba yake ya simu haipatikani kabisaaa) ila nataka nimfungulie biashara yoyote ile itakayomwezesha aweze kupata pesa ya kumuhudumia mtoto huku na mimi nikiendelea kuwajibika kama mzazi
Pia nataka nikaonane na Baba yake mzazi maana ndiye aliyepokea posa
NB;
Waweza nishauri kama kuna njia mbadala tofauti na hiyo niliyofikiria, pia waweza nifungulia thread kama hautojali ili na wadau wengine wachangie maana nimefunguka hapa baada ya kuona huyo mtoto aliyenyongwa hivyo na mimi nahofia nisije kusababisha maafa kwa kiumbe kisicho na hatia