KWELI Picha hii ya mwanaume aliyepanda farasi imetengenezwa

KWELI Picha hii ya mwanaume aliyepanda farasi imetengenezwa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
wakuu, picha hii inanipa mashaka kama ni halisi wana JamiiCheck naomba mnisaidie kujua uhalisia​

1750081210115.png
 
Tunachokijua
Akili Unde (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Aidha teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku na hii ni pindi tu inapotumika kwa nia iliyo njema, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano picha, sauti, na video.

Katika kujenga uwezo wa kumuwezesha kila mmoja kutambua maudhui yaliyotengenezwa kwa teknolojia hiyo ili kuepuka upotoshaji kwa kutumia Picha inayomuonesha mwanaume aliyependa farasi ufuatao ni uchambuzi wa kina kuhusu uhalisia wake.


Uhalisia wa Picha

JamiiCheck imeijiridhisha kuwa Picha hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde. Kwanza picha hiyo inayo mapungufu kadhaa yanayodhihirisha kuwa ni ya kutengenezwa kwani hayarandani na uhalisia.

Sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na Kiganja cha mkono kinachoonekana kujikunja lakini hakioneshi uhalisia wa vidole vyake kuonekana vimejikunja. Mfano mtu akunjapo ngumi na kuegemea juu ya kitu, kidole cha mwisho huonekana kikiwa kimejikunja hali ambayo ni tofauti kwa picha hiyo.

Uwepo wa shanga shingoni ambazo hazina uwiano wa idadi katika ya upande mmoja na mwingine kuizunguka shingo. Upande wa ulio karibu na Mshale namba mbili unaonekana kuwa shanga nne, lakini upande wa pili shanga tano huku zingine zikiwa na muunganiko usio halisi.

Pia kwa kawaida kamba ambayo hutumika kuongoza farasi hutokea upande wa kichwa, lakini katika picha hiyo zinaonekana kutokea upande wa chini wa shingo na kuelekea kiunoni mwa mpanda farasi jambo lisilo la kawaida.

1750319881474-png.3375669
Hii kama sio OG basi itakua ni ya kutengenezwa
 
Picha hii ina uwezekano mkubwa kuwa imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili bandia (AI) au imehaririwa kwa kiwango kikubwa.

Vigezo muhimu vilivyotumika kubaini hilo:

1. Ubora wa Maelezo (Details): Mavazi ya mzee yana maelezo ya kina sana (textures) ambayo ni ya kipekee kwa picha zilizotengenezwa na AI.

Nywele za farasi zinaonekana kama zimechorwa kwa mikono au zimetengenezwa kwa njia isiyo ya kawaida ya upigaji picha.

2. Mwangaza na mwonekano wa ngozi: Ngozi ya mtu aliye kwenye picha ina muonekano laini sana, na kuna utofauti mdogo wa sauti (tone) ya ngozi ambao ni wa kawaida kwenye picha za AI.
3. Mapungufu ya kimantiki au viungo: Huwezi kuona kwa uwazi viungo vya farasi (kama miguu, uso mzima), jambo ambalo mara nyingi huwa kasoro za picha zilizotengenezwa kwa AI ambazo hujaribu kuficha maeneo magumu kuunda.

4. Muktadha wa picha: Picha inaonekana kama imepangwa kisanaa sana (stylistic), kama picha ya filamu au hadithi ya kifalme—aina hii ya muundo hupatikana sana kwenye picha za AI.
 
Picha ya kutengeneza hii ukiangalia shingoni hakuna uwiano wa shangaa alizovaa mpanda farasi, upande mmoja zipo 4 mwingine tano
 
Macho yanaonyesha kasoro zinazodhihirisha kuwa imetengenezwa.
1. Jicho moja linaonekana kutazama tofauti na lingine
2. Mng’ao wa mwanga kwenye mboni hauko sawa kwa macho yote mawili.
3. Maumbo ya macho hayako sawia.
 
Back
Top Bottom