mkuu unajitahidi kuwajibu wajinga kwa upendo ingekuwa ni mimi ningewapa za kichwa tu!Ni rahisi kuusema sema hivi, kama mnavyousema na kuanza kuwazoesha Watanzania. Mnausema lakini mnashindwa hata kuuonesha kwenye charge sheet!
Hivi mnaweza kuwaambia wapenda haki, msingi imara wa amani, wauaji (note 'wa') wa Daudi Mwangosi wako wapi? Wauaji wa Msafiri Mbwambo (waliomchinja kinyama) wako wapi? Si walikimbia wakiwa na pingu mkononi mbele ya polisi wenye silaha, wakamnyang'anya bunduki askari mkoja, wengine wakiangalia 'mchezo mzima'. Baadae bunduki eti ikaokotwa ikiwa imetupwa nje ya geti. Wako wapi waliomuua kijana Ally Singano Zona pale Morogoro? Mnaogopa nini kufanya uchunguzi huru?
Waliomteka na kumuua kwa kumtesa vibaya Mbwana Masoud kule Igunga wako wapi? Matukio ni mengi. Mnaogopa hata kufanya uchunguzi huru kwenye tukio la kifo cha kada wenu Yohana Mpinga kule Ndago, Iramba, Singida, badala yake CHADEMA ndiyo wanapigania haki za marehemu yule kwa kudai serikali iwajibike kufanya uchunguzi ili ukweli wa tukio zima la Ndago ujulikane?
Ugaidi, ugaidi! Wanaopaswa kuwa behind bars kwa kesi kama hizi, wanaongoza chama chenu...alisema Shafi Adam Shafi, "Yana mwisho haya..."
vuta-nkuvute
habari za hapo 'kwenu' lumumba street.
Usilie. Ukilia unampatia nguvu oppressor. Hila zinakabiliwa kwa ujasiri. Moyo kabla ya silaha. Mwalimu nyerere alisema.
Hizi picha tunaomba muzihifadhi vizuri. Huko tuendako hawa akina Kilewo na wengine wanaoteswa sasa na CCM na vibaraka wake watakumbukwa kila mwaka katika sikukuu ya mashujaa.
Hata Mwalimu alikamatwa na wakoloni Waingereza. Lakini kwa vile wao ni wastaarabu, walimtendea kiutu. Hawa wakoloni weusi wa CCM sio wastaarabu; ni watesi wa Watanzania. Kwa sasa, tunatawaliwa kwa nguvu na CCM.
mkuu unajitahidi kuwajibu wajinga kwa upendo ingekuwa ni mimi ningewapa za kichwa tu!