PICHA: Henry Kilewo na wenzake mahakamani Tabora

Kama huna Mungu basi unashetani na kama huna budi basi una bundi.......umepewa macho na akili za kwendea chunvini tu,Think big
 
Nasikitika tu kwamaana viongozi wetu wa Tz wamepata bahati ya kuona yaliyotokea katika nchi nyingine na wameshindwa kujifunza.Hakika kuna siku ya ambayo kutakua na kilio na kusaga meno.Kinanyika kwa sasa ni kuwatesa viongozi wa CDM kwa kuhakikisha wanakaa mahabusu muda mrefu.sasa ili wakae mahabusu muda mrefu ni lazima wafunguliwe kesi za ugaidi, vinginevyo makosa mengine yana dhamana.Hili inabidi CDM walitafutie ufumbuzi kwani huko tuendako linaweza likafanyika karibia na uchaguzi mkuu,then likaathiri chama kwa kiasi kikubwa.Nafikiri kesi hizi zinaposhindikana inabidi serikali na wale waliohusika wafunguliwe mashtaka kwa kuanzisha kesi za uongo.
 
Ni rahisi kuusema sema hivi, kama mnavyousema na kuanza kuwazoesha Watanzania. Mnausema lakini mnashindwa hata kuuonesha kwenye charge sheet!

Hivi mnaweza kuwaambia wapenda haki, msingi imara wa amani, wauaji (note 'wa') wa Daudi Mwangosi wako wapi? Wauaji wa Msafiri Mbwambo (waliomchinja kinyama) wako wapi? Si walikimbia wakiwa na pingu mkononi mbele ya polisi wenye silaha, wakamnyang'anya bunduki askari mkoja, wengine wakiangalia 'mchezo mzima'. Baadae bunduki eti ikaokotwa ikiwa imetupwa nje ya geti. Wako wapi waliomuua kijana Ally Singano Zona pale Morogoro? Mnaogopa nini kufanya uchunguzi huru?

Waliomteka na kumuua kwa kumtesa vibaya Mbwana Masoud kule Igunga wako wapi? Matukio ni mengi. Mnaogopa hata kufanya uchunguzi huru kwenye tukio la kifo cha kada wenu Yohana Mpinga kule Ndago, Iramba, Singida, badala yake CHADEMA ndiyo wanapigania haki za marehemu yule kwa kudai serikali iwajibike kufanya uchunguzi ili ukweli wa tukio zima la Ndago ujulikane?

Ugaidi, ugaidi! Wanaopaswa kuwa behind bars kwa kesi kama hizi, wanaongoza chama chenu...alisema Shafi Adam Shafi, "Yana mwisho haya..."
mkuu unajitahidi kuwajibu wajinga kwa upendo ingekuwa ni mimi ningewapa za kichwa tu!
 
mhhh. mimi mawazo yangu kwa JOY KIRI... yule dogo anaomba hii kesi iendelee milele au hukumu ikitoka iwe ya kifungo kireeeefu. jamaa akitoka mama kachoshwaaaaaa
 
Mungu tusaidie kutuepusha na Shetani huyu ccm, Wapenda Amani na Haki ya Nchi yetu Tanganyika tunaangamia Baba.
 
Hizi picha tunaomba muzihifadhi vizuri. Huko tuendako hawa akina Kilewo na wengine wanaoteswa sasa na CCM na vibaraka wake watakumbukwa kila mwaka katika sikukuu ya mashujaa.

Hata Mwalimu alikamatwa na wakoloni Waingereza. Lakini kwa vile wao ni wastaarabu, walimtendea kiutu. Hawa wakoloni weusi wa CCM sio wastaarabu; ni watesi wa Watanzania. Kwa sasa, tunatawaliwa kwa nguvu na CCM.

Babu slaa anakula raha ughaibuni huku kina kileo wanashughulikiwa gerezani,hakika kumbukumbu itapendeza tuwekeeni namba za Joy tumsaidie asiteseke na baridi kwani jamaa akirudi atafikia kwa macheni

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
mkuu unajitahidi kuwajibu wajinga kwa upendo ingekuwa ni mimi ningewapa za kichwa tu!

Majibu ya maswali anayo Ben Saanane,akiamua kusema ukweli atawasaidia wanaoteseka magerezani,hebu ongeeni nae awe na huruma hata kidogo mipango yake anayoifanya inawatesa wanyonge

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tumaini Makene, au yeyote mwenye kujua; hivi nini kinaendelea katika hii kesi ya hawa jamaa? Maana wengine tumekuwa mbali na habri kwa kipindi fulani hapa kati.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom