Ni rahisi kuusema sema hivi, kama mnavyousema na kuanza kuwazoesha Watanzania. Mnausema lakini mnashindwa hata kuuonesha kwenye charge sheet!
Hivi mnaweza kuwaambia wapenda haki, msingi imara wa amani, wauaji (note 'wa') wa Daudi Mwangosi wako wapi? Wauaji wa Msafiri Mbwambo (waliomchinja kinyama) wako wapi? Si walikimbia wakiwa na pingu mkononi mbele ya polisi wenye silaha, wakamnyang'anya bunduki askari mkoja, wengine wakiangalia 'mchezo mzima'. Baadae bunduki eti ikaokotwa ikiwa imetupwa nje ya geti. Wako wapi waliomuua kijana Ally Singano Zona pale Morogoro? Mnaogopa nini kufanya uchunguzi huru?
Waliomteka na kumuua kwa kumtesa vibaya Mbwana Masoud kule Igunga wako wapi? Matukio ni mengi. Mnaogopa hata kufanya uchunguzi huru kwenye tukio la kifo cha kada wenu Yohana Mpinga kule Ndago, Iramba, Singida, badala yake CHADEMA ndiyo wanapigania haki za marehemu yule kwa kudai serikali iwajibike kufanya uchunguzi ili ukweli wa tukio zima la Ndago ujulikane?
Ugaidi, ugaidi! Wanaopaswa kuwa behind bars kwa kesi kama hizi, wanaongoza chama chenu...alisema Shafi Adam Shafi, "Yana mwisho haya..."