[PICHA] CHADEMA Ndani ya Shinyanga

Anapoona umati huo ndipo anapopatwa na kwikwi na kudai chadema wanataka kumpindua.
Hakuna wa kumpindua. Anajipindua yeye mwenyewe kwa kutojali matatizo ya wananchi na badala yake kuendekeza mambo ya anasa kama vile safari za mara kwa mara za nje zisizo na tija kwa taifa. Kweli chadema imeshika pabaya. Cuf nao utakuja kuwasikia sasa hivi wanaibeza chadema. Nccr na vyama vibaraka vingine hali kadhalika.
Chadema ndio chama tawala vilivyobaki ni vya upinzani.
Go chadema, go.
 
the truth shall remain there,c cri we a fed up tumechoka jamani nauli juu,mabomu tuu,umeme huu ,c cri rais zuzu na imetosha jamani lol tumechoka
 
hapana jamani...kwa hizi picha ninavyoona mwanza ilikuwa zaidi......
Tuangalie na Ratio ya population katika mkoa. Mwanza is more populated so its obvious watazidi shinyanga. But all in all response ni kubwa sana na ndiyo inayomtisha jamaa.
 
Kuna kama kaukweli flani hapo,wengi naona bado wana machungu ya 2010.
 
pipoooz..
nimekumbuka ule wimbo,
chadema 2napanda, 2napanda milimaa, ccm itashuka, itashuka mazimaa
 
hivi anawaongoza wanani jk kama wote hao hawamkubali?
jana alilialia aonewe huruma kama vile mtoto kumbe kubwa fisadi
 
Wananchi wamechoka na uongozi wa CCM. Hii inadhihilisha kuwa wengi waliipigia CDM isipokuwa waliibiwa kura zao. Otherwise ni swali gumu kulijibu ni ni kinachohamasisha kujitoa kwa watu hao!
 
Mungu awalinde na kila hila za mwovu na adui,ili mapambano yaendelee na hatimaye kupata ushindi wa haki.
Kikwete amepwaya kaiga kulihutubia Taifa kila mwezi lakini hana hoja za maana bali hofu,kulalamika sasa hivi anatafuta alindwe ili aendelee kubali ikulu,kwa umati huu sijui ni nani alimpigia kura
 
Tatizo la ushabiki wa kofia na t-shirt na vigelegele vya pilau na elfu 5 na usafiri wa bure kwenye kampeni wakajua watz wote tiyari wanaipenda ccm, kumbe walipenda na kutamani mabadiliko na si maisha magumu kila kukicha na ahadi za ahera zisizotimilika hadi ufe. Uongo na udhalimu hufika kikomo. Watu miwa wanalima wenyewe sukari wanakosa, shule wanajenga wenyewe watoto wao hawashindi, kodi wanalipa hazileti tija! Nyumba ujenge mwenyewe halafu ulale nje mwingine afaidi!
 
Back
Top Bottom