Picha: Athari za mvua Dar zaanza kuleta mafuriko

jaasz

Senior Member
Jan 14, 2016
129
12
bondeni-765x510.jpg

Vijana wakiwa wamekaa nje baada ya nyumba wanazoishi kujaa maji maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam kufuatia mvua zilizonyesha.

Kituo cha daladala za kwenda Gongolamboto cha Suwata Kariakoo kikiwa kimejaa maji hivyo kuleta adha kwa watumiaji kufuatia mvuo hizo.

Dimbwi la maji likiwa mbele ya jengo la Yanga.

Daraja la Jangwani na Kituo cha mabasi ya mwendokasi kikiwa kimezingirwa na maji.

Magari yakipita kwenye dimbwi la maji barabara ya mtaa wa Lindi Ilala.

Moja ya vibanda wanavyoishi wananchi waliobomolewa eneo la Kinondoni Mkwajuni maji yakipita katikati yake jambo ambalo ni hatari kwa watu wanaoishi ndani humo.

Nyumba ikiwa imezingirwa na maji eneo la Mchikichini Ilala kufuatia mvua hiyo iliyonyesha leo

Vijana wakiuangalia Uwanja wa Klabu ya Yanga ulivyojaa maji.
 
Kuwa na uwanja kama huo wa yanga no bora kutokua na uwanja kabisa....eti huo nao no uwanja mpaka na jina kabisa umepewa..yanga mnadhalilisha majina ya watu.
 
Hiyo Darisalama yenu...
Kwanza inanikera tukianza na Trafic Jam, Joto kali na ukiongeza hayo mengineyo....
Kumbe ushirombo pia ni Darisalama kama una pesa aiseeee..
 
Back
Top Bottom