Picha: ACT-Wazalendo Waitikisa Songea

Picha: ACT-Wazalendo Waitikisa Songea

Chama cha Act kilikuwa na mkutano, lakin kwa bahati mbaya au kwa kuzamilia mmetuwekea picha tano, ya kwanza mpaka ya tatu sio za leo, ya nne na ya tano ndo za leo hiv kama kweli mnataka kuingia kwenye siasa na sisi tuwa support ya nini kuweka picha za zamani mkachanganya na za leo.

Jaman wana jf wenzangu angalieni picha ya kwanza mpaka ya tatu kisha muangalie ya nne mpaka ya tano kama zinafanana.

My take fanyeni siasa za ushindani sio ushindani wa mitandaoni.

Wewe mtu ebu angalia picha hizo.

Hizo za chini Zitto alipokuwa anapokelewa Songea.Hizo tatu ndio mkutano wenyewe.

Angalia tshirt na kofia alizovaa Zitto; kumbuka Zitto hajawahi kufanya mkutano wowote wa ACT, huu ndio mkutano wa kwanza.

ACT haiendeshi siasa za uongo wala gilba, kinasimamia hoja zinazohusu maisha ya watu na maendeleo yao.
 
Wewe mzee ni wa kupuuzwa tu, tangu nimejiunga na JF sikuwahi kuona hata siku moja unajimu wako ukitimia, daima umekuwa ukijenga hoja kwa mizania ya staki nataka yani mguu ndani mguu nje, mlisema Zitto ni zaidi ya chama sasa hivi huyo nje, chama bado kipo na kinazidi kuchanja mbuga wanafiki mtaendelea kuumbuka mmoja mmoja mpaka tunamaliza uchaguzi October wote mtasambaa humu jukwaani.

Hivi wewe Shardcole and the so called Molemo ni shabiki jina ama Viongozi kweli ndani ya chama? Wakati mwingine nashindwa kuelewa juu ya upeo wenu katika siasa! Hivi kweli inahitaji rocket science kujua kuwa kufukuzwa kwa Zitto na kukua kwa kasi kwa ACT ni tishio kwa CDM ama UKAWA (mnavyojiita) kuliko CCM?

Wanasiasa ama mashabiki wa aina yenu ni janga kubwa katika chama. Ushabiki wa namna hii nimekuwa nikiuona katika chama changu cha CCM japo kwa sasa angalau kimeanza kutii falsafa ya Mwalimu ya "TUJISAHIHISHE" na ndio maana unaona kidogo kuna minyukano ya kukosoana hadharani na vijiadhabu kurejearejea.

Hakika ACT ya Zitto etal, wakizichanga karata zao vizuri, upepo mbaya utaamia kwenu katika sura ileile ambayo CCM ilikumbwa na kusababisha chama chenu kupata baadhi ya Wabunge wasiokuwa na vigezo (sitaki kuwataja).

Wanachama wa CCM huwa awahami kwa mafuriko bali kama hawakupendi watakuangusha huku wakiendelea kuwa wanachama. Hii ni tofauti na vyama vyenu (UKAWA) ambapo ni rahisi Wanachama kukimbia pale upepo unapobadilika. Hii ndio tofauti ya itikadi ya Wanachama wa CCM na wa vyama vyenu, ukitaka kudhibitisha hili angalia Mrema aliondoka na WanaCCM wangapi?

Mnahitaji kukisaidia chama chenu kwa maono na fikra zaidi kuliko ushabiki huu wa "low profile" mnaouonyesha hapa jamvini.

Narudia, Mimi ni Mwanachama wa CCM a.k.a Magamba kama mnavyozoea kutuita kipindi mkielemewa kwa hoja.

Ushauri; Jukwaa hili mbali ya kupata taarifa kwa wakati,pia ni shule ama tanuru la fikra kwetu sote, tulitumie vizuri kusaidia vyama vyetu badala ya udalali usio na macho wala masikio kwa kugeuza vibaya kuwa vizuri ama kukubaliana na ujinga ama upumbavu wa Viongozi wetu.
 
ACT Yangu ni haya:
1.Mkutano wa kwanza leo umekuwa ni wa mafanikio,kazi iendelee nchi nzima sasa.
2.Naomba sana wanachama wa ACT na wafuasi kiujumla,we need to be different,tusiige siasa za matusi,kejeli,mipasho,chuki na uongo hazitatusaidia tuwaachie wanaoziweza.Kiongozi ZZK umekuwa mfano mzuri katika hili naomba uwe unalisema kila utakapopita waTanzania wanahitaji mbadala wa kweli na washaanza kuamini.
3.Lets talk issues,tuzungumze mambo ambayo watanzania yanagusa maisha yao kiujumla,Thats what matters,na hayo ndio yatatufanya tuweze kuirudisha hii nchi katika misingi but with 21st century approach.
4.Tuwe tunalipua mabomu ya ufisadi ya CCM ni jambo zuri lakini we need to go more than that,nashukuru Katibu na mwenyekiti wanalijua hili na walilizungumzia,hata kichaa anaweza kulipua mabomu ya ufisadi,lakini swala ni kwamba wananchi wanataka kujua wewe utafanya nini ukiingia Ikulu?? huko ndiko tunakotakiwa kufocus,tupite kutangaza vision zetu kwa wananchi siasa za chuki tuwaachie wanaoziweza.
5.Moja kati ya sifa kubwa kabisa ya kiongozi ambayo anatakiwa kuwa nayo pamoja na yote ni kutokuwa na Jazba,tunashukuru Mungu hakuna mwenye hilo ndani ya chama chetu,tumuombe Mungu asituletee viongozi wenye hulka hiyo,people have started to believe tusiwaangushe.
6.La mwisho kabisa tupuuzieni kejeli zote,matusi,tutaitwa majina ya kila aina tuvumilie,nashukuru tena viongozi wetu mnalijua hili na tuombe lidumu,nakumbuka katika Bunge la escrow hata ZZK alisema hili kwamba yeye ana Ngozi nyingi wamshambulie tu.Barack Obama aliitwa kila aina ya majina terrorist,muslim,kenyan villager etc alivumilia yeye akawa anahubiri sera tu kilichotokea kitabaki historia.
Aluta Continua
Karibuni ACT-Wazalendo,Tuirudishe Nchi Katika Misingi Yake
 
Mimi nawaambia nyie Vijana hamuwajui ZITTO na Kitila Mkumbo,ndo mwanzo wa mwisho wa zama za CHADEMA hizo! Wapumbavu humu wanasema eti Nyota! Nyota ?! Hao watu wanatumia akili si ushabiki wa kijinga wa vijana wa CHADEMA waliojazana humu Jf.Kwa taarifa yenu hakuna mwanasiasa anayeweza kujenga hoja kwa sasa ndani ya CHADEMA anayeweza kumkaribia ZITTO wala Mkumbo,wengi wenu ni waropokaji tu kama akina Tundu Lissu, Mnyika n.k.

Ukweli ni kwamba kwa muda mrefu CHADEMA imekuwa na siasa za matukio na matusi na si siasa za hoja! Jiulizeni ni kweli CCM imewachosha wengi hapa nchini wakiwemo wazee wetu waasisi aina ya kina Joseph Warioba lakini hata mara moja hawajawahi kuifikiria CHADEMA kama Chama mbadala wa CCM! Ni kwa nini? Wazee hawa wanajua CHADEMA ni mkusanyiko fulani unaoongozwa na remote ya familia tokea Tengeru pale kwa Mzee Mtei kwa maslahi ya Familia hiyo na si Watanzania kama wanavyowadanganya majuha wao!
Unapo ona binti wa mtu makini kama Joseph Warioba anakimbilia kuchukua kadi ACT - Wazalendo ,kwani siku zote hakuona CHADEMA ipo kama chama cha siasa! jua kuna "consultations"!
CHADEMA hacheni kuweweseka,hata wana wa Israel walipoanza safari ya kutoka Misri wengi walijua Musa ndiye atakayewafikisha Nchi ya Ahadi lakini sivyo Musa alifia Njiani! Ni akini Haruni ndo waliwafikisha Kanaani Nchi ya Ahadi!
Leo mnambeza Zitto lakini amini nawaambia Zitto Zuberi Kabwe is a very smart and intelligent politician of our time!
Wakati CHADEMA wamejifunga kwenye ndoa ya Mkeka na CUF,NCCR,NLD ndo Zitto amewasoma na kuwapa big blow!
Kwanza umoja wa UKAWA ni umoja wa mashaka hilo halina ubishi kwa mtu makini.Zitto ameweka TEGO baya kote kwa CCM na UKAWA. Watakaokosa nafasi kote they are likely to join ACT - Wazalendo than any political Party. Kwahiyo msije shangaa baada ya Uchaguzi Mkuu Zitto ndo akawa na turufu ya Kuunda kambi rasmi ya Upinzani Bungeni! Ikitokea hivyo ndo CHADEMA mtawajua CUF ni nani after all mlishawaita Chama cha Mashoga na kejeli nyingi za akina Tundu Lissu za CCM B.
Lingine Tambueni kuwa Zitto hana cha Kupoteza kwa wakati huu anajijenga kama kiongozi makini wa upinzani ajaye hapa Nchini! Baada ya Uchaguzi huu Mkuu Dr. Slaa kwenda lala,John Cheyo kwenda lala,Mrema kwenda lala,Dr. Makaidi kwenda lala,Maalim Seif na Prof.Lipumba kwenda lala! Wanabaki "ring leaders" Zitto Kabwe,James Mbatia na Mbowe! Kati yao who can be trusted ?! Ni obvious kuwa ZITTO ndo anakwenda kuwa Icon wa siasa za upinzani hapa Nchini very soon! Na mwisho kwa sasa hakuna mwanasiasa wa upinzani aliyejijenga Kimataifa na kwa taasisi za ndani kuliko ZittO Zuberi Kabwe! KAMA UNABISHA ACHA MATUSI JENGA HOJA.
 
Wadau nilikuwa kwenye mkutano wa zitto. Ni kweli kwa kiasi fulani kulikuwa na watu . Lakini watu wengi kwa mtazamo walikuwa ni wafuasi wa cdm na ccm. Wengi walikuja kumsikiliza tu. Na baada ya hapo walimsikitikia sana zitto walisema anakwenda kufa kisiasa.
 
Nothing to Loose!!?,Huoni haupo tayari kuwa mshindi ila upo kwa kujaribu bahati yako. "There is no such thing Lucky."
 
Hata mimi nimeshawishika maana mkataa wengi ni Mchawi. Hakuna Chopa wala TOT na umati huu unaashiria makubwa mbeleni.w

Nyie jitekenyeni na mcheke wenyewe msubili hukumu yenu ya usaliti
 
Wadau nilikuwa kwenye mkutano wa zitto. Ni kweli kwa kiasi fulani kulikuwa na watu . Lakini watu wengi kwa mtazamo walikuwa ni wafuasi wa cdm na ccm. Wengi walikuja kumsikiliza tu. Na baada ya hapo walimsikitikia sana zitto walisema anakwenda kufa kisiasa.

Hata siamini kama umefikia hapa.@
 
Nyie mna bishana na maccm ukitaka kuamini kwann mtu aseme km ccm B act iko hv ccm yenyewe siitakuwa tishio maanaake ni ccm anajifanya yuko act kweli nmeamini act ccm B
 
Back
Top Bottom