Philipo Mwakibinga ajiunga na ACT Wazalendo

Philipo Mwakibinga ajiunga na ACT Wazalendo

CHADEMA tunagawana kazi siyo vyeo kama ameshindwa akaondoka akaenda ACT ni haki yake .njaa ni mbaya sana

Kama njaa zilivyowashika Lowassa, Msindai , Masha, Mgeja baada ya kukosa vyeo wakahama
 
Hivi chuo alimaliza??????

alifukuzwa mwaka jana kwa ushawishi wa ccm kisa alikuwa cdm lakini leo anaamua kuhamia act ambapo atazigawa kura za cdm ili kuisaidia ccm anayoipinga kila siku ishinde
 
Kwa hiyo hata akina Said Mkumba, Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Esther Bulaya, James Lembeli, Makongoro Mahanga, Ole Telele na wengineo wamekosea?
Mkuu ndio maana tunasema Chadema hakuna demokrasia,wao huisema CCM lakini wamesahau kuwa wao wamekuwa wakipokea makapi na kuwapa nafasi ya ubunge,na baado sisi tulijua tu haya yatatokea,haiwezekani mtu aliyekijenga chama kwa miaka nenda rudi leo ampishe mtu ambaye hata sera na kanuni za chama hazijui,sidhani kama ingekuwa CCM wangekubali ujinga huo eti leo mtu kakosa nafasi ya kuchaguliwa huko Chadema aje CCM leoleo na apitishwe kugombea nafasi,lazima kwanza akae kwanza ajadiliwe ndio chaguzi nyingine afikiriwe,wakihama makapi CCM hushangilia utadhani ndio wameshinda ,wakiondoka huko kwao hununa eti lengo ni moja ,lengo ni moja basi liwe kwa kutumia njia sahihi na si ujanja ujanja tu,CCM B(waliokatwa) kamwe hawatapeleka ikulu labda wazungumzie UFISADI tena kama walivyofanya hapo nyuma ,kitu ambacho kamwe kwa sasa hakizungumziwi ni kama mwiko sasa kuzungumzia UFISADI huko Chadema na UKAWA yao sasa wamerukia katiba,katiba bila ya kuondoa ufisadi ni sawa na kucheza kigodoro.
 
Malisa Godlisten umenena vizuri!!

Vijana nawashangaa sana sijui kwa nini mnapenda kuchezea fursa kiasi hicho? Kwanza alikuwa ameshatengeneza cv yake vizuri kwamba alitangaza nia ya ubunge, hivyo naamini baada ya miaka 5 chama lazima kingempa nafasi tu hata kama siyo ya ubunge. Sasa huko alikoenda ni kama ametupa 2 akachukua 0! Hivi anafikri UKAWA ikitinga ikulu itaendelea na wakuu wa wilaya wliopo? Wakuu wa mikoa waliopo? Hizi zote jamani ni fursa kwa vijana na bado Rais ana nafasi zake 10 za kuteua wabunge sasa unajuaje kama vyote hivyo Mwakibinga ungekosa hata kimojawapo? Huko alikoenda amepoteza na hatashinda kicho kiti "Ije mvua, lije jua".

Kuna mwingine kule Kasulu naye alikimbilia ACT sasa ngoja tuone kama huo ubunge ataupata tena!!
 
alifukuzwa mwaka jana kwa ushawishi wa ccm kisa alikuwa cdm lakini leo anaamua kuhamia act ambapo atazigawa kura za cdm ili kuisaidia ccm anayoipinga kila siku ishinde

Na bado CDM hawakuona hiyo sacrifice wakamkata???!!!
Acha ahame kumbe. .
 
MOTOCHINI pokea mgeni wenu huyo kiroho safi.
Sisi ukawa mtu akijitoa kwetu na kuja kwenu kiroho safi hatumuiti oil chafu bali tunamuombea heri kwenye safari yake.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo hata akina Said Mkumba, Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Esther Bulaya, James Lembeli, Makongoro Mahanga, Ole Telele na wengineo wamekosea?

Hapo kwa Mgeja, Bulaya, Lembeli hebu sahihisha, hao hawakuondoka kwasababu ya kura za maoni ya chama chenu cha mazingaombwe!
 
We endelea tu kujenga chama mpaka uzeeke wakati kina Said Nkumba wanapitishwa na CC hata bila kupitia kura za maoni.

Huyo Mwakibinga akiwa maarufu tu kupitia ACT,then next election atagombea kupitia CDM bila hata kupitia kura za maoni.

Nyie komaeni kujenga halafu wengine waje wapake rangi kiulaini.

Kama mnagawana majukumu kwa hiyo Slaa mmempangia likizo kwa sasa siyo?

Utakuja kujielewe uzeeni ukiwa huna hata nguvu za kupanda jukwaani.

We endelea na unafiki tu,watu wanapiga pesa.
 
CCM maghufuli ni fisadi wa alivyouza nyumba za serakali.
Ndugu Magufuli aliuza nyumba za Serikali kwa Wananchi na bei nafuu kwasababu ilikuwa ni mali ya Umma. Hazikuuzwa kibiashara na lengo ni kuwapatia watumishi wachache haki miliki ya nyumba hizo. Mie sioni tatizo pale maana walionufaika ni Watanzania na si rahisi tukapata wote.
 
MWAKIBINGA KATIKA CHAMA KIPYA.

ANAYE UNGA MKONO KARIBU ANAYE PUUZA KWAKHERI.

Kama Mwakibinga nina maamuzi yangu na siendeshwi na hisia bali naendeshwa na dhamira yangu.

Nimepata marafiki wengi sihofu kuwapoteza kwa kusimamia ninacho kifia.

Nilijiunga na chadema mwaka 2009/01/23. Nikiwa kidato cha sita. Baada ya hapo niliendelea kuhakikisha chadema inaenea vyuo vikuu vya dodoma nilifanikiwa kueneza chadema lakini nimefukuzwa chuo zaidi ya mara mbili niliamini kwenye ukombozi na msimamo wa CHADEMA. Nimetumika sana sana katika chama hichi.
Nimekua afisa mafunzo Taifa.
Nimekua mwenyekiti chadema UDOM.
Nimekua Mjumbe wa kamati tendaji ya jimbo la lupa chunya chadema.
Nimekua mratibu wa vijana bavicha chadema chunya.
Nimekua mjumbe katika kamati ya ufundi ya chadema nyanda za juu kusini.
Nimetumikia idara ya usalama ya CHADEMA kazi maalumu chini ya Rwakatale sijui hata kama Mbowe anajua labda Dr slaa.

Pamoja na hayo yote nakumbuka nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya chadema ni msingi kanada ya nyanda za juu kusini nikashinda Mbowe akasema nina hakili sana sifahi kuwa mwenyekiti ila niwe makamu nika kataa.

Niligombea bavicha taifa mbowe akaja usiku wa manane kumsafisha patrobas katambi wagombea wengine tuka hujumiwa.

Nimegombea ubunge chunya kila taarifa ilionesha uchaguzi haukuwa wa halali lakini amekatwa wa kwanza. Amepewa kasaka aliye ongoza jimbo kwa miaka 15 akashindwa 2005 akahamia chadema kabla hajazoea kahamia cuf kabla hajazoea kahamia ccm tena.
Nimejenga chunya kwa juhudi na mahalifa lakini siku ya siku analetwa KASAKA HATA KADI YA CHADEMA HANA.

Nimeitwa na viongozi wa chama nikaambiwa ni mwachie KASAKA lakini aliyeshika nafasi ya kwanza hajaitwa hata kuambiwa kama kumuheshimu tu MIRAJI HUSSEIN KAONEWA.

Huu ni udhalilishaji nimevumilia lakini leo mchana kata ya chokaa yaani nyumbani kabisa ambapo kuna makaburi ya babu na bibi mgombea aliye chukua nafasi ya kwanza kachukua na form karudisha lakini viongozi wa jimbo wame pora form ya mzee kabuje kwa mtendaji msimamizi wa uchaguzi mtendaji karipoti polisi lakini inaonekana agizo la kufukuzwa mzee kabuje limetoka juu yaani mkoa kanda na taifa.

Mbowe kauza jimbo letu kwa kasaka,
Kaamua na kuuza kata yetu No! Sitaki kuona chunya ina ujumiwa mimi chunya kwanza chama baadaye.

Nita hakikisha chunya ina kombolewa na nitapambana hadi nife siwezi kurudi nyuma

NINA MSIMAMO NA NIKO TAYARI KUUFIA. KAMA KUNA MTU YUPO TAYARI KUPOTEZA URAFIKI WANGU NAYE KWASABABU YA KUONANA NA KUACHANA CHADEMA BASI SEPA.

MWAKIBINGA NI YULE YULE NA SASA TUKUTANE CHUNYA MAHALI NILIPO ZALIWA.
HUJUMU KILA KITU ILA SIYO CHUNYA HAISEE

ACT WAZALENDO NDIYO CHAMA CHANGU KWASASA.
Mwakibinga II
0758 910403
 
Mtoa mada umechekesha kweli, hivi unafikiri hakuna anayetaka zile milioni 250 pale bungeni, unafikiri hakuna anayetaka yale marupurupu ya vikao pale bungeni. Yaani kwa ufupi unaoona wanaama kutuka chama kimoja kwenda kingine malengo yao huwa hasa ni maisha yao binafsi na siyo chama wala wananchi. Tanzania ni shamba la bibi hili na ndio maana unaona watu wako tayari kutumia mabilioni ya shilingi ili waweze kuingia madarakani kwani wanajua kabisa atapata faida tu baadae. Hamka kijana hata wewe kama unajiona bado una uwezo tafuta chako mapema. Kwani katika hali ya kawaida vijana wengi ambao huwa wanatumika tu kwenye vyama, lakini Mapapa yenyewe yapo.
 
Nimeona kwenye fb page yake.Nimekatishwa sana tamaa na kijana huyu niliyemwamini kama mpambanaji.Sawa ni maamuzi yake.Najua atashibdwa na baadaye atarudi tena CHADEMA!!
 
Kwani Kuna tofauti gani ya waliohama CCM kwenda CDM... That's politics... Mbona wewe inauma wakati Kuna wengi Wamepigwa Chini CCM wamekimbilia CDM, na Kuna wengi zaidi wataendelea kuhama,
 
Atakapo dondokea pua asisahau kupitia shauri hizi
 
Nimeona kwenye fb page yake.Nimekatishwa sana tamaa na kijana huyu niliyemwamini kama mpambanaji.Sawa ni maamuzi yake.Najua atashibdwa na baadaye atarudi tena CHADEMA!!

Mchumia tumbo
 
Back
Top Bottom