Philipo Mwakibinga ajiunga na ACT Wazalendo

Philipo Mwakibinga ajiunga na ACT Wazalendo

mkuu lizaboni wote hao uliowataja hakuna atayeshinda hata mmoja; bulaya ni ndoto kumshinda wasira na lembeli hawezi kumshinda kishimba so wote naona wamekul wa chuya

Unajidanganya sana kwani Lembeli na Bulaya wanasubiri kuapishwa kwa hali ilivyo majimboni kwao.
 
Ana haki ya kufanya alivyofanya kwani kamati kuu imetekwa na watu wa lowasa.
Walichokifanya mvomero hatutakaa tuwasahau kwa kumkata kijana wetu aliyekipingania chama hata kuhatarisha maisha yake ndugu MATOKEO ODENI MANYETA.

Tumewasusia mgombea wao;
Kwa hali hiyo mgombea wa ccm atatangaza ushindi saa mbili asubuhi.
 
Hahahaaaa...mwakibinga bana!
Kila la kheri bana..nakumbuka siku ileeee unaongoza nyimbo za mgomo UDOM (2010)..ila chunga sana, ukikosa ubunge..siasa ndo utapotea hivyo, istoshe hata zile platform za migomo wameshakubana..sjui umaalufu utaupatia wapi tena. Anyways..i like him, ana msimamo! Anafaa kuwa mbunge..akomae!
 
Kwa hiyo hata akina Said Mkumba, Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Esther Bulaya, James Lembeli, Makongoro Mahanga, Ole Telele na wengineo wamekosea?

Hawakukosea maana wameshuka kwenye gari bovu na kupanda zima!
 
haki yake bana akiny kuku kany akiny....a ba.ta dooh..proUKAWA tulizeni mzuka ndio siasa mamvi kaharibu kila kitu yaani hamna namna yakujinasua kujustify mtu kuhamia chama kingine..kifupi muwe wa pole tu..
 
mkuu lizaboni wote hao uliowataja hakuna atayeshinda hata mmoja; bulaya ni ndoto kumshinda wasira na lembeli hawezi kumshinda kishimba so wote naona wamekul wa chuya

Kishimba wa Imalaseko !? Kansigo
 
Last edited by a moderator:
Kila mtu anauhuru Wa kuchagua chama anachoona ni sahihi kwake

Kila la kheri mwanaharakati wa Udom mwakibinga

Viva CDM
 
Malisa Godlisten

sijaona logic.. mbona wale wa c.c.m wakihama kuja chadema hamsemi wamekose ila kwa mwakibinga kwenda kwa wazalendo unasema amekosea??? ukosefu huo upo upande mmoja tu wa chama hapa tanzania???
 
Last edited by a moderator:
Malisa Godlisten

Huko moshi nako hamkani hali si shwari,ndesamburo analazimisha mambo,anaripoti kubenea na gazeti lake



Philemon-Ndesamburo-620x308.jpg



Ndesamburo aivuruga Chadema | MwanaHALISI Online
 
Last edited by a moderator:
Hivi huyo dogo chuo kilimshinda ..ubunge ataweza kweli?

Arudi kwanza shule !
 
Aliyekua kada wa CHADEMA Philipo Mwakibinga amejiunga na chama cha ACT Wazalendo baada ya kushindwa kwenye kura za maoni huko jimbo la Lupa-Chunya. Sasa Mwakibinga atagombea ubunge jimbo hilo kupitia chama cha ACT.

Kwa maoni yangu Mwakibinga amekosea. Najua ni haki yake kujiunga na chama chochote cha siasa, najua pia ni haki yake kugombea ubunge. Lakini si kwa namna alivyofanya.

Nilitegemea Mwakibinga kama ilivyo kwangu na vijana wengine wa CHADEMA waliotangaza nia lakini hawakupitishwa, angetulia na kukisaidia CHADEMA kuiondoa serikali dhalimu ya CCM madarakani. Lakini ameamua kuondoka ili akatimize azma yake ya ubunge nje ya CHADEMA.

Nilimsoma Mwakibinga kwny group moja akisema "Huu ndio muda sahihi wa yeye kuwatumikia wananchi kama mbunge". Bila shaka alikuwa sahihi kuwaza hivyo. Lakini lazima aelewe kuwa CCM kuondoka madarakani ni muhimu zaidi kuliko yeye kuwa mbunge.

So angetulia ashirikiane na mgombea wa CHADEMA aliyepitishwa jimbo la Lupa ili chama kishinde. Ushindi wa CHADEMA Jimbo la Lupa ungekua ushindi kwa Mwakibinga pia. Chadema hatugawani vyeo tunagawana majukumu. Si lazima wote tuwe viongozi mwaka huu.

Mbona Julius S. Mtatiro alipokosa fursa Segerea hakuonesha kukereka? Hata alipoulizwa alijibu kwa hekima kuwa atamuunga mkono mgombea yeyote atakayepitishwa Segerea. Hii kilikua kiwango cha juu zaidi cha "matured politics".

Ni vizuri vijana tukajiandaa kisaikolojia tunapoamua kugombea nafasi za kisiasa. Tunaweza kuamini sisi ni bora zaidi ya wengine, tuna uwezo zaidi ya wagombea wengine lakini lazima tuheshimu maamuzi ya wananchi. Wakimpitisha mtu mwingine tofauti na sisi tusikasirike. Tumpe ushirikiano ili mradi awe amepitishwa kwa haki.

Pia ni muhimu tuelewe kuwa nafasi za kisiasa si ajira. Tusitegemee kufanya siasa kama sehemu ya ajira yetu. Ni muhimu wagombea wawe na ajira zao au njia zao nyingine za kuwaingizia kipato wakati wanagombea. Ili wasipopata nafasi wasione ndio mwisho wa maisha. Wasije kudhani hamna maisha nje ya siasa.

By the way namtakia kila la heri Mwakibinga huko alikoenda. Namtakia heri ktk mbio zake za ubunge jimbo la Lupa kupitia ACT (japo hatashinda). Pia nimtake ajiandae kisaikolojia kupokea matokeo ya ushindi wa CHADEMA jioni ya tar.25 October.!

ALL THE BEST MWAKIBINGA. Mwanajeshi mmoja akifa vitani, sio mwisho wa mapigano. Vita vinaendelea. Umetuacha vitani, tutapambana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha CCM inaondoka madarakani. VIVA CHADEMA, VIVA UKAWA.!

View attachment 278559

Well said brother.. Tatizo vijn wengi hushindwa kutofautisha harakti zao na nfasi za kisiasa.. Siasa hubadikika gafla na yapasa hujiandae vyema kisaikolojia..kakosea.. Namfaham uyo jamaa angekuja kuwa potential saaana mbeleni.. Muda utatoa majibu. Tuombe uzima

Tatizo moja la vijana wanaochipukia wananaona Siasa ni kama ajira, Kumbe ni sehemu za harakati za jamii.

Tatizo ni Madaraka.

be genuine wakuu!!

hata EL anataka madaraka tu! mwache aende
 
Mwakibinga kazi yote aliyotufanyia Udom ameizika kwa siku moja, hopeless kabisa mwakibinga. Tumemwondoa whatsap groups zote za ukawa wa leo akajiunge ya act.

Miye mwenyewe amenisikitisha sana kazi zote alizozifanya kupigania haki za watu mbalimbali anaamua kuisaidia ccm ishinde kwa kuwagawa wapiga kura wa Cdm chama ambacho kimemtesa sana ktk harakati zake za kupigania ukombozi wa nchi hii,tumuache aende tu lakini nafsi yake itamsuta huko mbeleni
 
Back
Top Bottom