Philipo Mwakibinga ajiunga na ACT Wazalendo

Philipo Mwakibinga ajiunga na ACT Wazalendo

MWAKIBINGA KATIKA CHAMA KIPYA.

ANAYE UNGA MKONO KARIBU ANAYE PUUZA KWAKHERI.

Kama Mwakibinga nina maamuzi yangu na siendeshwi na hisia bali naendeshwa na dhamira yangu.

Nimepata marafiki wengi sihofu kuwapoteza kwa kusimamia ninacho kifia.

Nilijiunga na chadema mwaka 2009/01/23. Nikiwa kidato cha sita. Baada ya hapo niliendelea kuhakikisha chadema inaenea vyuo vikuu vya dodoma nilifanikiwa kueneza chadema lakini nimefukuzwa chuo zaidi ya mara mbili niliamini kwenye ukombozi na msimamo wa CHADEMA. Nimetumika sana sana katika chama hichi.
Nimekua afisa mafunzo Taifa.
Nimekua mwenyekiti chadema UDOM.
Nimekua Mjumbe wa kamati tendaji ya jimbo la lupa chunya chadema.
Nimekua mratibu wa vijana bavicha chadema chunya.
Nimekua mjumbe katika kamati ya ufundi ya chadema nyanda za juu kusini.
Nimetumikia idara ya usalama ya CHADEMA kazi maalumu chini ya Rwakatale sijui hata kama Mbowe anajua labda Dr slaa.

Pamoja na hayo yote nakumbuka nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya chadema ni msingi kanada ya nyanda za juu kusini nikashinda Mbowe akasema nina hakili sana sifahi kuwa mwenyekiti ila niwe makamu nika kataa.

Niligombea bavicha taifa mbowe akaja usiku wa manane kumsafisha patrobas katambi wagombea wengine tuka hujumiwa.

Nimegombea ubunge chunya kila taarifa ilionesha uchaguzi haukuwa wa halali lakini amekatwa wa kwanza. Amepewa kasaka aliye ongoza jimbo kwa miaka 15 akashindwa 2005 akahamia chadema kabla hajazoea kahamia cuf kabla hajazoea kahamia ccm tena.
Nimejenga chunya kwa juhudi na mahalifa lakini siku ya siku analetwa KASAKA HATA KADI YA CHADEMA HANA.

Nimeitwa na viongozi wa chama nikaambiwa ni mwachie KASAKA lakini aliyeshika nafasi ya kwanza hajaitwa hata kuambiwa kama kumuheshimu tu MIRAJI HUSSEIN KAONEWA.

Huu ni udhalilishaji nimevumilia lakini leo mchana kata ya chokaa yaani nyumbani kabisa ambapo kuna makaburi ya babu na bibi mgombea aliye chukua nafasi ya kwanza kachukua na form karudisha lakini viongozi wa jimbo wame pora form ya mzee kabuje kwa mtendaji msimamizi wa uchaguzi mtendaji karipoti polisi lakini inaonekana agizo la kufukuzwa mzee kabuje limetoka juu yaani mkoa kanda na taifa.

Mbowe kauza jimbo letu kwa kasaka,
Kaamua na kuuza kata yetu No! Sitaki kuona chunya ina ujumiwa mimi chunya kwanza chama baadaye.

Nita hakikisha chunya ina kombolewa na nitapambana hadi nife siwezi kurudi nyuma

NINA MSIMAMO NA NIKO TAYARI KUUFIA. KAMA KUNA MTU YUPO TAYARI KUPOTEZA URAFIKI WANGU NAYE KWASABABU YA KUONANA NA KUACHANA CHADEMA BASI SEPA.

MWAKIBINGA NI YULE YULE NA SASA TUKUTANE CHUNYA MAHALI NILIPO ZALIWA.
HUJUMU KILA KITU ILA SIYO CHUNYA HAISEE

ACT WAZALENDO NDIYO CHAMA CHANGU KWASASA.
Mwakibinga II
0758 910403

Chagadema wahuni hao-mwenye akili na asiyekuwa opportunist hawez kukaa Chagadema. kadi yangu ni ya mwaka 2001 lkn mwaka 2009 niliichana
 
Kwa hiyo hata akina Said Mkumba, Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Esther Bulaya, James Lembeli, Makongoro Mahanga, Ole Telele na wengineo wamekosea?

Wewe situnakujua unalipwa kwa kutetea ccm. Sisi tumeichoka kaka hiyo ccm yako.
 
mkuu lizaboni wote hao uliowataja hakuna atayeshinda hata mmoja; bulaya ni ndoto kumshinda wasira na lembeli hawezi kumshinda kishimba so wote naona wamekul wa chuya

Labda kwa rushwa vinginevyo wanachukua majimbo wasira mwepesi juzi kwenye kura za maoni ananyonga mikono wagombea wenzake yamekuwa.masumbwi?
 
mkuu lizaboni wote hao uliowataja hakuna atayeshinda hata mmoja; bulaya ni ndoto kumshinda wasira na lembeli hawezi kumshinda kishimba so wote naona wamekul wa chuya

we lazima utakuwa mgonjwa wasira hana chake kwa bulaya
 
Mwakibinga anajua fika kwamba hatashinda na ACT. Ila anachofanya ni kwamba kwa kuwa CDM wamemtosa basi sasa tukose wote yaani kugawa jimbo kwa CCM
 
Hao wamepatia sana maana wanasaidia kuliondoa liCCM madarakani. kukosea ni kama alivyofanya Mwakibinga. kupunguza au kutaka kupunguza kura za kuliondoa liCCM madarakani

Maisha ya kiasa yanapatikana hata nje ya CHADEMA.
Mwache dogo atekeleze haki yake ya kidemokrasia.
Kukatwa na kuhama ndo habari ya mjini.
 
Ni vyema kuwa na hoja pambanuzi kuliko malumbano yasiyo na muafaka, ACT WAZALENDO ni chama pekee pinzani ambacho kinachukua nafasi ya chadema kama chama bora pinzani ambacho hakijawahi kutokea tz,cdm imepoteza mvuto kwa wasomi kwa kuwa hawahitaji kurubuniwa na pesa za EL,hivyo basi tutashuhudia mwaka huu cdm/ukawa wakishika nafasi ya tatu....!!!!! WEKA NA HILI KWENYE KUMBUKUMBU!!!!
 
Kwa hiyo hata akina Said Mkumba, Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Esther Bulaya, James Lembeli, Makongoro Mahanga, Ole Telele na wengineo wamekosea?

kweli kaka, mtu ni mwema akiingia chadema, na akitoka ni mbaya..... chadema hakuna demokrasia aiseee
 
Atakuwa ameona haki haitendeki ukiona hivyo.

hahahahahaha kumtoa whatsap ndo umemkomoa au niaje? poor idea kabisa... tatzo lenu wana ukawa mnawadanganya watanzania kua mna demokrasia ya ukweli lakin kiukweli hamna demokrasia yoyote angalia lowassa alivopitishwa kimabavu.... kingne msijione nyie wakamilifu kupita kias, mtu akihama vyama vngne kwenda chadema anainekana mwema lakin wanaohama chadema kwenda vyama vingne wasaliti na wanatumika huo ni upuuzi.. mkubaliane na hali kua tumeshawajua.
 
Malisa Godlisten

Mwema ni anayeingia chadema tu anayetoka anatumika na amenunuliwa.... kwa hyo kama kuunganisha nguvu kama kakatwa kwann muwapokee hao waliokatwa na ccm ambao wameshindwa kura za maoni.... chadema na ukawa ikulu muisahau aisee
 
Last edited by a moderator:
Mwakibinga kazi yote aliyotufanyia Udom ameizika kwa siku moja, hopeless kabisa mwakibinga. Tumemwondoa whatsap groups zote za ukawa wa leo akajiunge ya act.

Kama mlijua amefanya kazi ya maana kwa nini mlimkata?
 
Unajidanganya sana kwani Lembeli na Bulaya wanasubiri kuapishwa kwa hali ilivyo majimboni kwao.

Umesikiliza taarifa za vyombo vya habari kuhusu kinachoendelea Bunda kuhusiana na swala la kulazisha Easther Bulaya agombee na kuwakata Makamanda waliosoteshwa na Wassira (+Bulaya) long time lina gharama zake
 
Hivi huyo dogo chuo kilimshinda ..ubunge ataweza kweli?

Arudi kwanza shule !

Tusimsakame sana dogo.
Mbona tunao wabunge wetu wengi hawana degree?
Elimu ya dogo na ya baadhi ya viongozi kadhaa waandamizi wa chama vianendana. Kuwa na degree ni changamoto. Kilichomkosesha ni ukamanda na amekatwa...
dah
 
Sio kosa lako mtoa mada! Maana inaonesha unapenda sana angebaki kwako!! bali ni tamaa usioijua athari kwa wanaohama na kubaki katika chama!
 
Back
Top Bottom