Philipo Mwakibinga ajiunga na ACT Wazalendo

Philipo Mwakibinga ajiunga na ACT Wazalendo

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
202
Reaction score
1,588
Aliyekua kada wa CHADEMA Philipo Mwakibinga amejiunga na chama cha ACT Wazalendo baada ya kushindwa kwenye kura za maoni huko jimbo la Lupa-Chunya. Sasa Mwakibinga atagombea ubunge jimbo hilo kupitia chama cha ACT.

Kwa maoni yangu Mwakibinga amekosea. Najua ni haki yake kujiunga na chama chochote cha siasa, najua pia ni haki yake kugombea ubunge. Lakini si kwa namna alivyofanya.

Nilitegemea Mwakibinga kama ilivyo kwangu na vijana wengine wa CHADEMA waliotangaza nia lakini hawakupitishwa, angetulia na kukisaidia CHADEMA kuiondoa serikali dhalimu ya CCM madarakani. Lakini ameamua kuondoka ili akatimize azma yake ya ubunge nje ya CHADEMA.

Nilimsoma Mwakibinga kwny group moja akisema "Huu ndio muda sahihi wa yeye kuwatumikia wananchi kama mbunge". Bila shaka alikuwa sahihi kuwaza hivyo. Lakini lazima aelewe kuwa CCM kuondoka madarakani ni muhimu zaidi kuliko yeye kuwa mbunge.

So angetulia ashirikiane na mgombea wa CHADEMA aliyepitishwa jimbo la Lupa ili chama kishinde. Ushindi wa CHADEMA Jimbo la Lupa ungekua ushindi kwa Mwakibinga pia. Chadema hatugawani vyeo tunagawana majukumu. Si lazima wote tuwe viongozi mwaka huu.

Mbona Julius S. Mtatiro alipokosa fursa Segerea hakuonesha kukereka? Hata alipoulizwa alijibu kwa hekima kuwa atamuunga mkono mgombea yeyote atakayepitishwa Segerea. Hii kilikua kiwango cha juu zaidi cha "matured politics".

Ni vizuri vijana tukajiandaa kisaikolojia tunapoamua kugombea nafasi za kisiasa. Tunaweza kuamini sisi ni bora zaidi ya wengine, tuna uwezo zaidi ya wagombea wengine lakini lazima tuheshimu maamuzi ya wananchi. Wakimpitisha mtu mwingine tofauti na sisi tusikasirike. Tumpe ushirikiano ili mradi awe amepitishwa kwa haki.

Pia ni muhimu tuelewe kuwa nafasi za kisiasa si ajira. Tusitegemee kufanya siasa kama sehemu ya ajira yetu. Ni muhimu wagombea wawe na ajira zao au njia zao nyingine za kuwaingizia kipato wakati wanagombea. Ili wasipopata nafasi wasione ndio mwisho wa maisha. Wasije kudhani hamna maisha nje ya siasa.

By the way namtakia kila la heri Mwakibinga huko alikoenda. Namtakia heri ktk mbio zake za ubunge jimbo la Lupa kupitia ACT (japo hatashinda). Pia nimtake ajiandae kisaikolojia kupokea matokeo ya ushindi wa CHADEMA jioni ya tar.25 October.!

ALL THE BEST MWAKIBINGA. Mwanajeshi mmoja akifa vitani, sio mwisho wa mapigano. Vita vinaendelea. Umetuacha vitani, tutapambana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha CCM inaondoka madarakani. VIVA CHADEMA, VIVA UKAWA.!

11201494_886615841430109_2664872540388598777_n.jpg
 
Well said brother.. Tatizo vijn wengi hushindwa kutofautisha harakti zao na nfasi za kisiasa.. Siasa hubadikika gafla na yapasa hujiandae vyema kisaikolojia..kakosea.. Namfaham uyo jamaa angekuja kuwa potential saaana mbeleni.. Muda utatoa majibu. Tuombe uzima
 
kwa hiyo hata akina said mkumba, hamisi mgeja, mgana msindai, esther bulaya, james lembeli, makongoro mahanga, ole telele na wengineo wamekosea?

mkuu lizaboni wote hao uliowataja hakuna atayeshinda hata mmoja; bulaya ni ndoto kumshinda wasira na lembeli hawezi kumshinda kishimba so wote naona wamekul wa chuya
 
Bora basi angeenda CCM kama ana ubavu lakini huko alikoenda nina shaka kama atafanikiwa. Hicho chama ni bado kichanga sana kinashindwa hata kumpata mgombea wa Urais wakati kwenye vyama vingine watu wanagombana na kususa kwa sababui tu wameenguliwa kwenye nafasi ya kuwa wagombea wa Urais.
 
Kwa hiyo hata akina Said Mkumba, Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Esther Bulaya, James Lembeli, Makongoro Mahanga, Ole Telele na wengineo wamekosea?
nampalapala... Jitahidi kujenga hoja ushabiki tupa kulee..

Acha kijana uokoke.. Njoo ukawa usichelewe
 
mkuu lizaboni wote hao uliowataja hakuna atayeshinda hata mmoja; bulaya ni ndoto kumshinda wasira na lembeli hawezi kumshinda kishimba so wote naona wamekul wa chuya

Mmh walewale.... Hakujakucha bado?... Amka
 
Tatizo moja la vijana wanaochipukia wananaona Siasa ni kama ajira, Kumbe ni sehemu za harakati za jamii.

Tatizo ni Madaraka.
 
CHADEMA tunagawana kazi siyo vyeo kama ameshindwa akaondoka akaenda ACT ni haki yake .njaa ni mbaya sana
 
Kwa hiyo hata akina Said Mkumba, Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Esther Bulaya, James Lembeli, Makongoro Mahanga, Ole Telele na wengineo wamekosea?

Hao wamepatia sana maana wanasaidia kuliondoa liCCM madarakani. kukosea ni kama alivyofanya Mwakibinga. kupunguza au kutaka kupunguza kura za kuliondoa liCCM madarakani
 
Kwa hiyo hata akina Said Mkumba, Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Esther Bulaya, James Lembeli, Makongoro Mahanga, Ole Telele na wengineo wamekosea?

esther Bulaya tayari ni mbunge anasubiri kuapishwa tu pamoja na mwenzake lembeli! Huyo dogo ni kama maji sasa kutaka kupanda mlima
 
Vipi hawa wengine walioshinda kwenye majmbo yao lakini wamekatwa unawazungumziaje walizike tu?

Huoni kwamba hawajatendewa haki?

Na wana wajibu wa kujaribu mahali pengine kama akivyofanya Lowassa?
 
Bora basi angeenda CCM kama ana ubavu lakini huko alikoenda nina shaka kama atafanikiwa. Hicho chama ni bado kichanga sana kinashindwa hata kumpata mgombea wa Urais wakati kwenye vyama vingine watu wanagombana na kususa kwa sababui tu wameenguliwa kwenye nafasi ya kuwa wagombea wa Urais.

Nibora kukosa mgombea kuliko kuweka fisadi...
 
Bora basi angeenda CCM kama ana ubavu lakini huko alikoenda nina shaka kama atafanikiwa. Hicho chama ni bado kichanga sana kinashindwa hata kumpata mgombea wa Urais wakati kwenye vyama vingine watu wanagombana na kususa kwa sababui tu wameenguliwa kwenye nafasi ya kuwa wagombea wa Urais.
Kamanda usimpangie Philipo Mwakibinga ni mtu mzima ana maamuzi yake.
 
Back
Top Bottom