Pf3

believer

JF-Expert Member
Dec 22, 2012
615
250
Hizi ni fomu za polisi zinazohusu kutoa taarifa polisi kwanza inapotokea ajali,ili ukatibiwe au kupokelewa hospitali kwa matibabu.Wote tunatambua kua ajali ni jambo la dharura na hata jinsi ya kulishughulikia linahitaji uharaka na umakini,ningeshauri hizi fomu ziwekwe mahospitalini na afisa wa polisi awepo hospitalini kusaidia yale ambayo yanamlazimu mtu aliyepata ajali kwenda polisi kuchukua fomu ya PF3 ili apokelewe hospitalini,jeshi la polisi wekeni maafisa wenu hata mmoja mmoja kwa shift kila hospitali za wilaya tunusuru majeruhi wetu kama ambavyo mnafanya katika mashule ya msingi.
cc kakajambazi
 
illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,275
2,000
kweli pf3 ni tatizo lakini kwa kukurekebisha tu hizi form sio maalum kwa ajili ya ajili pekee bali kwa majeruhi wa aina yote, umuhimu wake ni kukusanya upelelezi wa awali kujua chanzo kisa cha majeruhi binafsi niliwahi kuona mtu kagongwa na gari baada ya kupelekwa hosipitali wakasema ameanguka kwenye mnazi wazo lako ni zuri
 
nimekupata mkuu,imagine inabidi mtu adanganye tukio vinginevyo mtu amefika hospitalini akiwa majeruhi anaambiwa kachukue PF3.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom