Peter Ngumbullu, Mwenyekiti mpya wa Bodi TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Peter Ngumbullu, Mwenyekiti mpya wa Bodi TANESCO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 28, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,872
  Likes Received: 83,350
  Trophy Points: 280
  JK amteua mwenyekiti mpya TANESCO

  na Hamisi Mwesi na Shehe Semtawa
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  RAIS Jakaya Kikwete amemteua Peter Ngumbullu kuwa mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini kuwa uteuzi huo unaanzia Oktoba 27, 2008 hadi Oktoba 26, 2011.

  Taarifa hiyo ilieleza kuwa Ngumbullu amewahi kulitumikia taifa katika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa mkurugenzi mtendaji katika Shirika la Fedha Duniani (IMF) akiwakilisha nchi 21 za Afrika.

  Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha; Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais; Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais; Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo; Naibu Katibu Mkuu na Naibu Katibu wa Tume ya Mipango; Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha; Msaidizi wa Katibu Baraza la Mawaziri; na Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uchumi katika Sekretarieti ya Baraza ya Mawaziri.

  Taarifa hiyo ilieleza kuwa kitaaluma Ngumbullu ana shahada ya uzamili katika uchumi wa maendeleo ya Chuo Kikuu cha Williams, kilichoko nchini Marekani, Diploma katika uchumi ya Chuo Kikuu cha Colorado, nchini Marekani na shahada ya kwanza ya uchumi, uongozi na utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Aidha, taarifa hiyo ilieleza kutokana na uteuzi huo Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja aliwateua wajumbe wa bodi hiyo ambao ni Victor Mwambalaswa, Adollar Mapunda, Agnes Bukuku, Juma Bakari, Vintan Mbiro, Semindu Pawa, Beatus Segeja na Ngosi Mwihava.
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  kwakweli mimi huwa nashindwa kuelewa sababu za msingi za hawa watanzania wenzetu ambao wamelitumikia taifa kwa muda mrefu na kisha kustaafu, kuendelea kuteuliwa kuongoza mashirika ya umma.
  hivi inakuwaje hawa 'watawala' wetu wanashindwa kuwateua watu ambao bado wana nguvu ya kutosha kuweza kuongoza haya mashirika?
  bandugu naomba mwenye kulifahamu hili vizuri anifahamishe.
   
 3. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2008
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Bodi ya wakurugenzi huwa wanavikao vichache tu vya kuangalia na kushauri mwenendo wa utendaji wa shirika husika. na huhitaji wazoefu wachache ambao wengi ni wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali kama wabunge, wizara ya fedha, n.k.
  watu wenye nguvu na wasomi wanahitajika kwenye shirika lenyewe wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, wakurugenzi wa idara na wataalamu ambako kuna day to day activities
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Oct 28, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Jina la Victor Mwambalaswa kama nimewahi kulisikia mahali fulani; I don't remember though..
   
 5. Wakunyuti

  Wakunyuti JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Victor Mwambalaswa ni Mbunge kutokea mkoa wa Mbeya, na very interesting anatokea kwenye Kanisa la kilutheri usharika uleee uliomleta Rostam Kanisani na kuzua balaa...tena ni mzee wa Kanisa kabisa...Sijui huyu jamaa ndiye aliyemleta????
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Recycling at its best!

  Lakini tusisahau methali...better the devil you know than an angel you dont know!
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Huyu Profesa aende vyuoni akagawe taaluma yake
   
 8. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Pamoja na kumkaribisha Rostam Azizi Kanisani,Mzee Victor Kilasile Mwambalaswa ni Mbunge wa Lupa huko Chunya Mbeya.Ni mmoja wa Wabunge waliopo kwenye kamati ya Madini...ambaye kwa namna yoyote kesho (Jumanne) atazungumza kuhusu Tume ya Bomani ya Madini.

  Victor Mwambalaswa kama Wabunge wengi ni Mbunge Mfanyabiashara,ukitaka rekodi zake zaidi Muangalie alipokuwa Kampuni ya sigara yeye na rafiki yake Mzee Katunda.Kwa mtazamo wangu nafikiri amechaguliwa kwenye Ujumbe wa Bodi ya Tanesco kutokana na Ujumbe wake wa Kamati ya Bunge ya Madini na Nishati.
   
 9. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2008
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Inawezekana ila pia hata spika wetu Mzee Sita nae ni mzee wa kanisa wa usharika huo huo so yote yanawezekana!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mbunge Mwambalaswa, kuwemo humu ni safi sana, maana huyu hana mchezo ni mpiganaji hodari sana wa haki za wananchi.
   
 11. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  adollar mapunda si alikuwa posta na simu?
   
 12. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hapa ndipo tunapokosea. Bodi ndiyo msimamizi mkuu wa menejimenti. Ukiweka mambumbumbu kama mimi ndiyo umeliwa. Kawaida yetu ilikuwa hapa ni mahali pa ulaji hasa ukiangalia kuwa Mkurugenzi Mkuu anawajibika kwa Rais na si kwa bodi! Hawa walitakiwa kuwa ndiyo wawakilishi wetu katika kuangalia mwenendo mzima wa menejimenti. Si mahali pa kuweka wenye uzoefu wachache hata kidogo.
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ndiye huyohuyo. Kwa sasa yuko kwenye bodi kadhaa za mashirika ya UMMA ikwemo DAWASCO, MUHIMBILI na sasa TANESCO!
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  hata mimi hapa ndipo pananipa ukakasi wa kukubaliana na teuzi mbalimbali.
  mimi nadhani suala si uzoefu tu, muhimu zaidi ni uadilifu.wasiwasi wangu hawa wastaafu huwa hawana nguvu/jeuri ya kusimamia maslahi ya wananchi kwa kuwa wanakuwa wanatekeleza matakwa ya waliowateua kwa kudhani kwamba hiyo ni 'favour' ambayo ni adimu kuipata tena ukiwa umestaafu.
  kwa namna moja ama nyingine wanajiona kama vile hawana cha kupoteza.
  kwa mtazamo wangu hawa wateuliwa waliostaafu hawaleti tija iliyokusudiwa.
  nadhani ifike mahali sasa hawa wazee wetu wapumzike waendelee kula pensheni zao na watoe ushauri wao pale watakapohitajika, vijana wenye uwezo, nguvu na maarifa wapewe nafasi waongoze mashirika ya umma, naamini ufanisi utakuwa mkubwa sana.Mbona baba wa taifa alikamata madaraka ya nchi hii akiwa kijana mdogo lakini hadi leo tunakubaliana na mambo mengi mazuri aliyoifanyia nchi yetu.Na kuna vijana wengi tu ambao wlionyesha ufanisi katika kazi zao akiwemo Salim Ahmed Salim, Malecela na wengine wengi tu.
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  heshima yako mkuu,
  inawezekana kweli mwambalaswa ni mpiganaji wa kweli wa haki za wananchi.
  tafadhali naomba unifahamishe ni kwa namna gani amewapigania wananchi wa lupa/chunya au watanzania kwa ujumla wake.
  je historia yake inasomekaje huko kwenye biashara zake na huko kwenye kampuni ya sigara inaposemekana alipata kufanya kazi. je tokea amekuwa mbunge amefanya nini cha kufikia kupongezwa au kuitwa mpiganaji wa haki za wananchi?ni hayo tu mkuu.
   
 16. B

  Boma Senior Member

  #16
  Nov 2, 2008
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 190
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Ukweli ni kwamba Mh Mwambalaswa alikuwa mla rushwa mkuu huko sigara na ana mali nyingi alizopata kwa murungula, pia mpaka sasa ni mfanyakazi wa sigara, analipwa mshahara na marupurupu mengine manono sana.

  ukiangalia kwa undani utaona anavi-element vya ufisadi ndani ya damu yake, pesa ndiyo kaweka mbele.
   
Loading...