Peter Kupaza na mauaji ya Mwivano Mwambashi, nini ilikuwa hatma ya kesi hii?

Mkwaju Ngedere

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
1,046
874
Mwishoni mwa miaka ya 90 kulitokea kesi ya mauaji huko Baraboo Wisconsin iliyomuhusu Peter Kupaza ambaye alituhumiwa kumuua kisha kumchuna ngozi mpwa wake Mwinvano Mwambashi na baadae kuutupa mwili huo katika mto.

Bahati mbaya sikuweza kupata hatma ya kesi hii baada ya mtuhumiwa kukata rufaa na je kwa sasa mtuhimiwa yupo wapi?
 
Mwishoni mwa miaka ya 90 kulitokea kesi ya mauaji huko Baraboo Wisconsin iliyomuhusu PETER KUPAZA ambaye alituhumiwa kumuua kisha kumchuna ngozi mpwa wake MWINVANO MWAMBASHI na baadae kuutupa mwili huo katika mto. Bahati mbaya sikuweza kupata hatma ya kesi hii baada ya mtuhumiwa kukata rufaa na je kwa sasa mtuhimiwa yupo wapi?
Kisa cha Marehemu Mwivano Mwambashi Kupaza
Eneo la tukio....

Ilikuwa ni Julai 30 1999, mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Brenda Dement nchini Marekani aliyekuwa akiishi kwenye mji wa Barabo Wisconsin Kaskazini mwa Marekani, alikuwa Picnic na wanae pamoja na marafiki zake wawili kandokando ya mto Wisconsin, ambapo ndio aligundua mabaki ya mwili wa binadamu yaliyokuwa yamefungwa kwenye mifuko ya nailoni ya kuhifadhia uchafu, maarufu kama mifuko ya Rambo hapa nchini.

Baada ya uchunguzi zaidi mwanamke huyo alikuja kugundua kuwa katika eneo lile ilikuwepo mifuko mingi iliyokuwa na mabaki ya mwili wa binadamu ambao ulikuwa umekatwakatwa kinyama utadhani nyama ya ng’ombe buchani. Polisi walifahamishwa kuhusu kupatikana kwa mabaki yale ya mwili wa binadamu na walipofika kwenye eneo la tukio walichukuwa mabaki yote lakini miguu haikupatikana, ili kwenda kuifanyia uchunguzi zaidi. Uchunguzi wa awali ulithibitisha kwamba yale mabaki yalikuwa ni ya mwanamke mwenye asili ya Afrika ingawa hawakuweza kutambua sura yake kutokana na kichwa chake kuchunwa ngozi yote kiasi cha kutotambulika.

Pamoja na wataalam wa maiti kuyachunguza kwa makini mabaki ya mwili ule, lakini walishindwa kabisa kugundua sababu ya kifo cha mtu yule. Ili kutambua kwamba mwili ule ni wa nani, ilibidi polisi waanze kuchunguza kesi zaidi ya 2,000 za wanawake walioripotiwa kupotea katika jimbo la Wisconsin lakini hakuna mtu yeyote aliyefananishwa na mabaki ya mwili ule. Wakati mabaki yale yanapatikana yalikuwa na siku tatu tangu kutupwa mtoni lakini iliwachukuwa polisi miezi sita kutambua kwamba mwili ule ulikuwa ni wa nani. Na ili kuutambua mwili huo ilibidi polisi waombe msaada kutoka kwenye kitengo maalum cha uchunguzi wa kutumia teknolojia ya kisasa katika kutengeneza taswira kilichopo katika mji wa Milwaukee.

Polisi walituma picha za kichwa cha mwili ule kwenye kitengo hicho, walizoiga kwa kutumia mashine maalum inayotumia compyuta iitwayo Computer Tomography Scan, maarufu kama TC Scan. Jopo la wataalam hao wakiongozwa na mtaalam wa mafuvu ya bianadamu Profesa Robert Crockett walitenegeneza sura nne za mtu mmoja zinazofanana. Muonekano wa sura hizo nne ulipelekwa kwa wataalam wengine walioko katika jimbo la Kentucky ambapo waliiboresha na kuifanya ionekane ni ya msichana aliyekuwa mionekano tofauti tofauti.
Muonekano wa kwanza ulikuwa wa msichana aliyekuwa na nywele ndefu, wa pili ulikuwa ni wa msichana aliye na nywele fupi, wa tatu aliyekuwa amefunga kitambaa kichwani na muonekano wa nne ulikuwa ni wa msichana aliyevaa miwani, Mionekano yote minne ilikuwa imebeba sura ya mtu mmoja.

Picha zile zilisambazwa katika majimbo yote ya Marekani ili kuomba msaada kwa mtu yeyote atakayeweza kumtambua mtu mwenye sura ile. Hazikupita siku nyingi mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Shari Goss alikwenda kituo cha polisi na kuwajulisha kwamba zile picha zilizosambazwa zinafanana kabisa na za msichana aitwae Mwivano Mwambashi Kupaza, ambaye alikuwa ni binamu wa mume waliyetalikiana aitwae Peter Kupaza mhamiaji kutoka Afrika Mashariki nchini Tanzania.

Alipoonyeshwa mabaki ya mwili ule, mwanamke yule alizidi kuthibitisha kwamba hata ile mifuko iliyohifadhia yale mabaki ya ule mwili ambayo ni ya duka moja maarufu liitwalo Woodman’s Grocery. Ni duka ambalo Peter Kupaza alikuwa anafanyia manunuzi yake ya kila siku na alikuwa na kawaida ya kuhifadhi ile mifuko.
Mnamo January 31, 2000, polisi walikwenda katika eneo la Middleton kwenye majengo yaliyoko katika barabara ya Pleasant View mahali alipopanga Peter Kupaza ili kumhoji. Kupaza aliwaeleza Polisi kwamba Mwivano alirejea nyumbani nchini Tanzania tangu April 25, 1999.

Alisema ana uhakika kwamba Mwivano alishafika nchini Tanzania baada ya kupiga simu nchini Tanzania na kuzungumza na baba yake Mwivano. Kupaza alizidi kuwaeleza Polisi kwamba Mwivano alipanda basi kuelekea katika Jimbo la Iowa ambapo huko angekutana na mtu aliyemtaja kwa jina la Shadrack ambaye wangesafiri pamoja kurejea nchini Tanzania. Kupaza alikiri kutofahamu ubini wa Shadrack na namna ya kuwasiliana naye, kwani hakuwa na anuani yake na wala namba yake ya simu.

Aliendelea kuwaeleza wapelelezi wa polisi kwamba kabla Mwivano hajaondoka nchini Marekani alikuwa akiishi pale pale katika jiji la Madison, lakini katika eneo jingine akiishi pamoja na rafiki zake wa Kikorea ambao alikuwa akisoma nao, na siku alipoondoka, waliondoka pamoja kupitia katika jimbo la Iowa. Alieleza kwamba, siku Mwivano anaondoka alimpa kiasi cha dola 1,500 kama gharama za usafiri. Awali Kupaza aliwaeleza polisi kwamba Mwivano hakuwahi kufika wala kuishi pale alipokuwa akiishi, lakini baadaye katika mahojiano hayo Kupaza alikiri kwamba Mwivano aliwahi kufika pale nyumbani kwake mara kwa mara.

Alipoonyeshwa zile picha zilizotengenezwa, zenye taswira ya Mwivano ambazo ndizo zilizotambuliwa na mwanamke waliyetalikiana naye, Kupaza alisema hamtambui mtu mwenye sura ile na kwamba sura ile haifanani na ya Mwivano. Historia inaonyesha kwamba Peter Kupaza na Mwivano Mwambashi Kupaza ni mtu na dada yake, kwa maana ya mtoto wa baba mkubwa na mdogo ambao waliishi jirani huko kijijini kwao Usambaani, kabla ya Kupaza hajakutana na aliyekuwa mkewe Shari Goss.

Shari Goss alikuwa ni mwanamke wa kizungu kutoka nchini Marekani aliyekuwa akifanya kazi za Kimishenari kwenye miaka ya 1990, nchini Tanzania kabla ya kukutana na Peter Kupaza na kuanza uhusiano. Baadae Peter Kupaza na Shari Goss waliondoka nchini na kwenda kuishi nchini Marekani mwaka 1993, ambapo walifunga ndoa na kuishi pamoja kama mume na mke katika jimbo la Wisconsin kwenye mji wa Madison. Mnamo January 1997, Mwivano Mwambashi Kupaza alikwenda nchini Marekani na kuungana na kaka yake Peter Kupaza pamoja na mkewe Shari Goss ambapo waliishi pamoja.

Baadae Mwivano alianza kusoma Kiingereza kwenye chuo kiitwacho Wisconsin English Collage, kilichopo katika mji wa Madison. Peter Kupaza na Shari Goss walitalikiana katikati ya mwaka 1997 baada ya Kupaza kumbaka dada yake Mwivano na kumpa ujauzito. Baada ya kutengana Kupaza na Mwivano waliondoka kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi na Shari na kuhamia kwenye eneo lingine. Inasemekana Kupaza alimlazimisha Mwivano kutoa ule ujauzito kwenye kliniki ya Madison ambapo kwa mujibu wa ushahidi uliopatikana kutoka kwenye kliniki hiyo, Mwivano alifanikiwa kuutoa ujauzito huo aliopewa na kaka yake.

Kwa mujibu wa ushahidi uliokusanywa kutoka kwenye kliniki hiyo, ulionesha kwamba Mwivano alijaza fomu maalum ya kutoa mimba sambamba na nakala kivuli (Photocopy) ya viza yake ya kuingia nchini Marekani pamoja na nakala Kivuli nyingine ya leseni ya udereva iliyotolewa katika Jimbo la Wisconsin. Taarifa za kiuchunguzi kutoka kwenye maabara ya kuchunguza alama za vidole ilikuja kuthibitisha kwamba alama za vidole zilizopatikana kwenye fomu za kliniki ambayo Mwivano alitolea mimba zinafanana kabisa na alama za vidole zilizokutwa kwenye mabaki ya mwili uliookotwa ambao ulikuja kuthibitishwa kwamba ni wa Mwivano.

Baada ya Polisi kukusanya ushahidi wote uliopatikana ikiwa ni pamoja na kumhoji Peter Kupaza, Polisi hao walianza kupekua nyumba aliyokuwa akiishi Kupaza kwa kutumia mbwa maalum waliokuwa wakimilikiwa na kampuni iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Canine Solutions International. Mbwa hao wakiwa wanaongozwa na mwanamama aitwae Sandra Anderson waliweza kugundua mabaki ya damu iliyoganda kwenye ukuta wa choo ambapo vipimo vya DNA vilikuja kuthibitisha kwamba damu ile ilikuwa ni ya Mwivano.

Polisi pia walikuta vitu ambavyo vilikuja kuthitishwa na Shari kuwa vilikuwa vikimilikiwa na Mwivano. Vitu hivyo vilikuwa ni Biblia, saa ya mkononi, vito vya dhahabu na nguo, ikiwa ni pamoja na mifuko ya plastiki inayofanana na ile iliyohifadhia mabaki ya mwili wa Mwivano. Kutokana na ushahidi uliopatikana Peter Kupaza alitiwa nguvuni kwa kutuhumiwa kumuuwa dada yake binamu Mwivano Mwambashi Kupaza. Mnamo Juni 18, 2000, Peter Kupaza ambaye alikuwa akitetewa na Wakili aliyetajwa kwa jina la Catherine alifikishwa katika mahakama ya Sauk County na kusomewa mashitaka ya kumuuwa dada yake Mwivano Mwambashi Kupaza na kuukatakata mwili wake na kisha kuutupa katika mto wa Wisconsin.

Mahakamani hapo walikuwepo pia wazazi wa Mwivano, ambao walisafiri wakitokea nchini Tanzania ili kusikiliza shauri hilo. Baada ya kusomewa mashitaka hayo ya mauaji ya dada yake, Kupaza alikanusha katakata kumuuwa dada yake, huku machozi yakimtoka alisema “Mwivano ni dada yangu, Mwivano ni dada yangu wa damu, ni sehemu ya familia yangu, kamwe sikumuuwa, ninakanusha kabisa kutenda kosa hilo”
Ukweli ni kwamba kesi hiyo ilivuta hisia za watu wengi waishio katika mji wa Madisoni ikiwemo jamii ya Watanzania waishio katika mji huo, hivyo mahakama ilikuwa ikifurika sana kila siku kesi hii ilipokuwa ikisikilizwa na wahudhuriaji wengi walikuwa wakitokwa na machozi kwa kuhuzunishwa na unyama aliotendewa Mwivano Kupaza binti mbichi wa miaka 25.

Kesi hiyo ambayo iliendeshwa kwa kutegemea zaidi ushahidi wa kimazingira, iliendelea kusikilizwa kwa upande wa mashitaka kuleta mashahidi wake. Akitoa ushahidi wake pale mahakamani, aliyekuwa mke wa Peter Kupaza Bi Shari Goss aliiambia mahakama hiyo kwamba Kupaza alipokwenda nchini Marekani hakuwa na fedha za kujikimu na katika kipindi chote alichoishi naye hakuwahi kuwa na kazi hadi mwaka 1997, Mwivano alipowasili nchini Marekani na kuishi nao.Shari aliendelea kusema kwamba kuanzia mwaka 1997 ndipo kupaza alianza kufanya kazi.

Lakini wafanyakazi wenzie walipohojiwa walisema kwamba Kupaza hakuwahi kuajiriwa bali alikuwa kibarua wa kufanya kazi maalum( Part-time job) Hiyo ilikuwa ni katika kukanusha madai ya Kupaza kwamba alimpa Mwivano kiasi cha dola zipatazo 1,500 kama nauli ya kurejea nchini Tanzania.

Alipoulizwa kwamba aliwezaje kuweka akiba ya kiasi hicho cha fedha, wakati hakuwa na historia ya kuwa na kipato kinachofikia kiasi hicho, Kupaza alisema kuwa fedha hizo alikuwa akijiwekea kidogo kidogo nyumbani na sio benki. Hata hivyo kulikuwa na wasi wasi mwingine, kwani mwaka 1998 baada ya kutalikiana na Shari Goss Kupaza alishindwa kulipia gharama za gari alilokuwa amelikodisha kwa matumizi yake binafsi. Inasemekana Kupaza alishindwa kulipia gharama za kukodi gari kutokana na ukosefu wa fedha uliotokana na yeye kutokuwa na ajira ya kudumu.

Kutokana na sababu hiyo ya ukosefu wa ajira ya kudumu, Kupaza pia alikosa hata fedha za kulipia gharama za talaka mahakamani. Katika fomu ya mahakama Kupaza aliandikisha Thamani zake zote , lakini hakuandikisha kiasi chochote cha fedha alichoweka akiba nyumbani, ingawa alimuandikisha Mwivano kama mtegemezi wake katika fomu hiyo.

Akiendelea kutoa ushahidi wake Shari aliielezea mahakama kuhusu tabia ya unyanyasaji aliyokuwa nayo mumewe huyo mpaka wakatalikiana. Pia alielezea historia ya Kupaza aliyokuwa nayo kijijini kwao huko Sambaani nchini Tanzania ya kupenda kuchinja mifugo waliyokuwa nayo pale nyumbani kwao. Shari aliongeza kusema, “Kupaza alikuwa na utaalam wa kutumia kisu kwa uhodari wa hali ya juu wakati wa kuchinja mifugo.”

Pia alibainisha kuwa Kupaza alikuwa ni katili sana kwa wanyama. Naye baba wa marehemu Mwivano, mzee Mwambashi Kupaza akitoa ushahidi wake, alisema kwamba hakuwahi kuwasiliana na mwanae Mwivano tangu Juni 1998, na pia hakuwahi kuwasiliana na Peter Kupaza kwa zaidi ya miaka miwili nyuma. Hata hivyo na yeye pia aliungana na Shari Goss kuthibitisha kwamba Peter Kupaza alikuwa anajua vizuri sana kutumia kisu wakati wa kuchinja mifugo kule kijijini kwao ambapo mzee Mwambashi alikiri kwamba kuchinja mifugo wanayofuga pale kijijini kwao ni sehemu ya mila na desturi zao.

Shahidi mwingine aliyeitwa alikuwa ni Shadrack Msengi, ambaye alikuwa ni Mtanzania anaeishi katika Jimbo la Iowa. Huyu ndiye aliyetajwa na Kupaza kwamba, Mwivano alikwenda Iowa ili kuungana naye ili wasafiri pamoja kurejea nchini Tanzania. Katika ushahidi wake, Shadrack Msengi alikiri kuwafahamu Peter Kupaza na Mwivano ambao alisoma nao shule moja nchini Tanzania, lakini alikanusha kuwasiliana na Mwivano tangu alipowasili nchini Marekani.

Pia Shadrack alisema kwamba hakuona kama kulikuwa na sababu ya Mwivano kusafiri kwenda Iowa kabla ya kusafiri kwenda nchini Tanzania. Shahidi mwingine binti wa Kitanzania aishiye nchini Marekani aitwae Faith Mmanywa, rafiki wa karibu wa Kupaza ambaye nae kama Kupaza alihamia nchini Marekani akitokea nchini Tanzania mwaka 1998, akitoa ushahhidi wake alisema, mnamo Septemba 1999 (Baada ya mwili wa Mwivano kuwa umeshapatikana lakini ukiwa bado haujatambuliwa) Kupaza alimpigia simu na kumweleza kwamba Mwivano amesharudi nchini Tanzania na asingeweza kurejea nchini Marekani tena.

Kupaza aliendelea kumweleza Bi Mmanywa kwamba sababu ya yeye kumpigia simu ni kutaka kumjulisha kuwa Mwivano amerejea nchini Tanzania na kwamba amemuachia jukumu zito la kujiandaa kuoa siku yoyote. Jukumu lingine alilolieleza Kupaza ni lile la kumshawishi Bi Mmanywa ahamie katika Jimbo la Wisconsin. Pia Kupaza alimjulisha Bi Mmanywa kwamba, kwa mujibu wa taarifa alizopata kutoka nyumbani nchini Tanzania ni kwamba Mwivano alikuwa amejiunga na shule ya uuguzi nchini Tanzania. Awali katika mahojiano na polisi, Kupaza alisema kwamba ana uhakika mwivano yupo nchini Tanzania kwa sababu alipiga simu na kuongea na baba yake Mwivano, kitu ambacho baba yake mwivano alikanusha pale mahakamani.

Alipoulizwa ni kwa nini aliwadanganya polisi kuhusu kuthibitisha kwamba aliongea na baba yake mwivano kwa simu na kujulishwa kuwa Mwivano yuko nchini Tanzania wakati haikuwa kweli? Akijibu swali hilo Kupaza alidai kwamba alilazimika kuwadanganya polisi kwa sababu alihofia kuwa Mwivano angeshtakiwa kwa kuwepo nchini Marekani kinyume cha sheria kwa sababu Viza yake ilikwisha muda wake.

Lakini hata hivyo Kupaza alishindwa kutoa sababu ya kumdanganya Mmanywa kuhusu Mwivano kurejea nchini Tanzania. Katika utetezi wake Kupaza alisema kuwa alimweleza Bi Mmanywa kwamba Mwivano alikuwa ameomba na kukubaliwa kujiunga na chuo cha uuguzi nchini Tanzania kabla hajaenda nchini Marekani na kwamba huenda angerejea nchini Tanzania kujiunga na masomo ya uuguzi.

Lakini hata hivyo hakukanusha madai ya Mmanywa kwamba yeye Kupaza alipata taarifa za Mwivano kuwa ameshajiunga na Chuo cha uuguzi nchini Tanzania kutoka kwa baba yake Mwivano mzee Mwambashi Kupaza. Shahidi mwingine aliyetoa ushahidi wake katika kesi hiyo ni Brenda Dement, mama aliyeona mabaki ya mwili wa marehemu Mwivano kule mtoni. Akiongozwa na mwendesha mashitaka Bi Rhoda Ricciard, Brenda alisema kwamba, siku ya tukio alikwenda Picnic yeye na watoto wake watatu, pamoja na rafiki zake wawili, ndipo walipogundua mabaki ya mwili wa binadamu yakiwa kwenye mifuko ya takataka.

Hata hivyo Brenda alibainisha kwamba katika eneo hilo alikuwepo mtu mmoja mweupe (Mzungu) aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 au anayekaribia miaka 50 ambaye alikuwa akirandaranda katika eneo hilo, lakini akionekana kama mtu mwenye wasiwasi hivi. Baada ya wao kugundua kuwepo kwa mabaki ya mwili wa binadamu katika eneo lile, mtu yule aliwafuata na kuwashauri wawajulishe polisi.

Baadae mtu yule alitoweka mahali pale akiwa ndani ya gari dogo jeupe aina ya Van, kabla ya polisi kufika kwenye eneo la tukio. Huo ukawa ni utata mwingine, kwani Kupaza alikuwa ni mwafrika mweusi. Hata hivyo mwanasheria wa Mahakama ya Sauk Patricia Barett, aliukataa ushahidi ule unaohusu mtu mweupe (Mzungu) kuonekana katika eneo la tukio.

Lakini mwendesha mashitaka Rhoda Ricciard alisema kwamba upande wa utetezi unaruhusiwa kuibua ushahidi ambao huenda ukabainisha kwamba watu wengine walihusika na mauaji yale. Katika utetezi wake mwingine Kupaza aliiambia mahakama kuwa haoni sababu ya yeye kushitakiwa kwa kosa la kumuuwa dada yake Mwivano, kwa sababu wataalam waliochunguza mwili wa marehemu wameshindwa kuthibitisha sababu za kifo cha Mwivano.

Mnamo Juni 21, 2000 Jopo la washauri wa mahakama ya Sauk walitumia takribani saa 9 kufanya majumuisho ya ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa mashitaka vikiwemo vielelezo vya mifuko iliyohifadhia mabaki ya mwili wa Mwivano na ule wa alama za vidole, ambapo walikubaliana na upande wa mashitaka kwamba peter Kupaza alimuuwa dada yake Mwivano Mwambashi Kupaza mnamo Julai 1999.

Katika majumuisho hayo jopo la washauri wa mahakama hiyo walizingatia ushahidi ufuatao;Kielelezo cha kwanza kinaonesha kwamba Kupaza alidanganya kwenye fomu yake ya kuomba kazi katika kampuni nyingine mnamo Juni 1999, miezi miwili baada ya Mwivano kusemekana ameondoka mjini Madison kuelekea Iowa, ambapo Kupaza alijaza jina la Mwivano katika fomu hiyo akimtaja kama ni mtu ambaye kampuni inaweza kuwasiliana naye iwapo itatokea dharura inayomhusu yeye Kupaza. Hata hivyo anuani ya mwivano iliyojazwa kwenye fomu hizo ilikuwa siyo sahihi.

Taarifa hizo za kupaza, kwenye fomu ya kuomba ajira zilichukuliwa na mahakama kama ni za uongo. Pili mabaki ya mwili wa Mwivano yalikutwa kandoni mwa mto Wisconsin, ambapo inasemekana Kupaza anaufahamu vizuri sana mto huo, kwani mfanyakazi mmoja aliyekuwa akifanya kazi na Kupaza, aliieleza mahakama katika ushahidi wake kwamba wakati fulani aliwahi kuzungumzia mto huo na Kupaza. Katika maelezo yake mfanyakazi huyo alimnukuu Kupaza akiulezea mto huo kuwa ni mzuri sana lakini ni hatari pia.

Tatu mabaki ya mwili wa Mwivano yalikuwa yamekatwakatwa kwa umahiri mkubwa na kulikuwa na muonekano uliionesha kwamba aliyeukatakata mwili ule alikuwa na utaalam wa kufanya kazi buchani, utaalam ambao inasemekana Kupaza anao kutokana na ushahidi uliotolewa na Shari Goss pamoja na baba yake Mwivano mzee Mwambashi Kupaza kuwa Peter kupaza alikuwa na uzoefu ya kuchinja wanyama kutokana na mazingira aliyokulia kule kijijini kwao Sambaani nchini Tanzania ambapo tabia ya kujichinjia mifugo majumbani ni jambo la kawaida.

Nne Kupaza alikuwa amejitengenezea kalenda yake mwenyewe ambapo alikuwa amejipangia majukumu ambayo alikuwa ameyagawa kwa wiki. Katika kalenda hiyo kulikuwa na maneno matatu ambayo yaliandikwa kwa lugha inayotumika nchini Tanzania, lakini hata hivyo Lugha hiyo haikutajwa pale mahakamani.

Kalenda hiyo ilikuwa na neno “Bodo” neno ambalo lilitafsiriwa na baba yake Mwivano, Mzee Mwambashi Kupaza baada ya kuombwa kufanya hivyo na mahakama, kuwa lina maana ya kuangukia kitu au kuwa juu ya kitu ambacho kinaanguka.

Neno la pili lilikuwa ni “Mushingwa”Hili nalo lilitafsiriwa kama siku iliyotengwa (Chosen day) au siku maalum iliyotengwa (Special chosen day)

Neno la mwisho lilikuwa ni “Fanya kazi”, neno hili liliandikwa kwa lugha ya Kiswahili kama lilivyosomwa pale mahakamani. Maneno yote hayo yaliandikwa katika kalenda hiyo yalidhihirisha kwamba Kupaza alikuwana jambo la siri alilokuwa amelifanya na hakutaka mtu mwingine afahamu.

Kwa kujumuisha ushahidi wote uliotolewa mahakamani hapo, mnamo Juni 23, 2000 , Peter Kupaza aliyekuwa na umri wa miaka 40 wakati huo, alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani na alipewa uwezekano wa Parole akishatumikia kifungo cha miaka 31 gerezani na kuonesha nidhamu katika kipindi chote atakachokuwa gerezani.

Baada ya hukumu ile kutolewa wazazi wa marehemu Mwivano waliridhia mtoto wao mpendwa kuzikwa nchini marekani, ambapo mazishi yake yalifanyika Juni 21, 2000, siku ya Jumapili saa 8 mchana katika makaburi ya Westby ikiwa ni siku moja baada ya Peter Kupaza kuhukumiwa na takribani mwaka mmoja tangu mwivano alipouawa.

Katika mazishi hayo, kitengo cha ulinzi wa amani (Sheriff Department) cha Sauk County kilipeleka kikosi cha askari wa heshima ili mkuongoza mazishi hayo. Mara baada ya mazishi, Shari Goss ambaye ndiye aliyekuwa mwenyeji wa wazazi wa marehemu Mwivano katika kipindi chote cha kesi ya Kupaza, aliungana na waumini wa kanisa lake pamoja na wafanyakazi wa mahakama ya Sauk County, kuwapa pole wazazi wa Mwivano ikiwa ni pamoja na kutoa fedha walizochanga ili kuwapa wazazi hao kama rambi rambi zao.

Wazazi wa Mwivano walitoa shukrani zao kwa watu wote waliowasaidia, tangu walipofika nchini Marekani mpaka shauri la mtoto wao lilipokwisha, kisha wakarejea nchini Tanzania. Naye Peter Kupaza kwa upande wake alikata rufaa ambayo ilitupwa mwaka 2003, na kuamriwa aendelee kutumikia kifungo chake. Hata hivyo mwaka mmoja baadae, yaani mwaka 2004, Peter Kupaza alikata rufaa nyingine akituhumu ushahidi wa mbwa wa kunusa walioongozwa na mwanamama Sandra Anderson, kuwa haukuwa ni wa kuaminika. Kwani Sandra alikiri katika mahakama ya Michigan kwamba alipandikiza vielelezo vya ushahidi katika kesi nyingine. Hivyo Kupaza alituhumu kwamba huenda na kwenye kesi yake Sandra alipandikiza Vielelezo vya ushahidi pia.
Rufaa yake hiyo nayo ilitupwa mnamo Mei 25, 2006.
 
image.jpeg

Muuaji Peter Kupaza
 
Leo katika pitapita zangu humu, nakutana na hii habari japo kwa ufupi kuhusu mauaji haya ya mtanzania huyu alieuwawa kikatili huko Marekani.

Nakumbuka hii habari huko udogoni nilipata kuisikia tu japo sikuitilia maanani sababu labda nilikua mdogo na sikuelewa chochote kama mtu mzima.

Hivyo leo kukutana na habari hii Ikanipelekea kwenda katika vyanzo mbalimbali kusoma zaidi kuhusu hii habari,
niseme tu ni habari ya kusikitisha sana kama sio ya kuogopesha. Naomba kuuliza kwa wale waliomfahamu huyu Peter Kupaza hakua na matatizo ya akili kweli

Vyanzo mbalimbali na comments mbalimbali katika blogs zinasema huyu Peter Kupaza alikua akimfanyia ukatili wa kijinsia(rape), dada yake huyo. Ila mwisho wa siku sheria ilifuata mkondo wake na kuhukumiwa maisha gerezani, sijajua huyu bwana kama bado yupo hai au la, kuna comment moja katika blog moja mwaka 2007 mdau anasema jamaa "anafanywa" na masela wa huko jela na amekua shoga na alipoonekana alikua akitembea kama mwanamke. What goes around ...

Wadau mnaojua hii stori mtatueleza zaidi.

Kupaza Mwivano.jpg
Kupaza.jpg
 
Hii stori ipo youtube ni Video kabisa ikielezea jinsi mwili wake ulivyookotwa na ulivyofanyika uchunguzi mpaka akapatikana Muuaji pia
 
Hapo juu pameandikwa "mauaji ya xxxxx" halafu ndani kuna swali la "kama yupo hai au amekufa" saitan kabisa
 
Back
Top Bottom