Peter Kibatala: We need a Police to Police the Police

Kwani humu Jamiiforums, Jeshi la Polisi halina Special thread kama TRA, TANESCO AU DAWASA?
 
Kwani humu Jamiiforums, Jeshi la Polisi halina Special thread kama TRA, TANESCO AU DAWASA?
Hawana ubavu huo wa kuweka thread ya namna hii humu. Wanajijua walivyo, usifikiri kwamba hawaifahamu 'image' yao jinsi ilivyo.
Wao wenyewe mtu binafsi mmoja mmoja Wana account zao humu, Mambo yote yanayojadiliwa humu mitandaoni wanayaona na kuyasoma.
 
Elimu,elimu,elimu,elimu,elimu,ilimu,ilimu,ilimu.

Kwenye Qur'an tukufu hata huko MWENYEZI MUNGU alitukumbusha juu ya elimu na kusisitiza ikiwezekana tukaifuate hata uchina
 
Elimu,elimu,elimu,elimu,elimu,ilimu,ilimu,ilimu.

Kwenye Qur'an tukufu hata huko MWENYEZI MUNGU alitukumbusha juu ya elimu na kusisitiza ikiwezekana tukaifuate hata uchina
Mbali na Elimu, lakini pia Katiba na Sheria zilizopo nazo ni tatizo lingine. Sheria zilizopo ni kandamizi kwa Raia na zinawapa kinga Polisi wasiweze kuwajibishwa kisheria hata pale wanapofanya makosa makubwa ya jinai Kama kuua watu kiholela.
 
Mmmh police gan mwenye Masters? PhD?

Aaah wee hapanaa.
Wapo wengi sana huwa wanajiongeza wakiwa makazini, Wapo wengine smart sana hata Darasani mfano Commishner Jerali Thobias Andengeye wakati RCO Morogoro tulikuwa tunasoma naye masters alikuwa kipanga, Baadae akapanda, akawa RPC mara full commishner wa HR polisi mara nikamona general wa zima moto nasikia sasahivi mkuu wa mkoa, sijui ki utendaji jeshini yukoje lakini darasani alikuwa mkali sana
 
Nipe jina la polisi mmoja tu ambaye ana cheo cha PhD.

Yaani polisi anayeitwa Afande Dokta...
 
Itafahamika baada ya ku-surrender hizo simu!

Ni ujinga tu. Ni sawa na mgonjwa aliyekatika kidole cha mguuni halafu daktari anasema mgonjwa apimwe haja kubwa.

Vioja vya polisi vinajulikana. Manji alituhumiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya, halafu walimpeleka kupima mkojo.

Polisi wakitaka kukutengenezea kesi ya uwongo ndiyo huwa wanahangaika na vitu visivyo na uhusiano. Haitashangaza ukasikia kuwa watuhumiwa wamepatikana na msokoto wa bangi.
 

Ukiwa mgonjwa wa akili, unaropoka chochote. Eti Kibatala huwa anahonga majaji!! Waombe ndugu wakusindikize hospitali.
 

Kelele nyingi but no content. Mtu yeyote mwenye akili timamu, mwelewa, mkweli wa nafsi na mzalendo wa kweli, ataungana na Kibatala. Kwa sababu anachoongelea Kibatala ni kupanua uwigo wa haki.

Ndani ya jeshi la polisi, kama zilivyo taasisi nyingine, kuna waovu. Kuna polisi ni majambazi, wala rushwa na watengenezaji wa kesi za kubumba, hawa hawawezi kudhibitiwa na polisi wenzao, kinahitajika chombo kingine, kama ambavyo baadhi ya mataifa wamefanya.
 
Nakumbuka mwaka 1996 pale Tunduma , ujambazi ulikua unafanywa na polis. Mitaa ilikua inafungwa saa nne usiku. Waliletwa polis Toka makao makuu kuja kukomesha matukio ya uhalifu, polis kadhaa walidakwa.
Kule Njombe kuna mwaka mmoja, polisi aliuawa kwa rungu, na mlinzi wa kampuni kwenye tukio la wizi.

Polisi alikuwa kwenye lindo la bank usiku. Usiku huo akiwa na smg akaongozana na majambazi mpaka Kibena, karibia kilometa 10 toka eneo lake la kazi. Walipofika eneo la uhalifu, polisi yule alipiga risasi, mlinzi akakimbia. Majambazi yakaendelea kufungua mashine waliyokusudia. Kwa kuwa mashine ilikuwa kubwa, iliwachukua muda mrefu. Polisi akijua hakuna mlinzi, akabaki amesimama akitazama majambazi yanavyofungua mashine. Mlinzi wa kampuni alimnyemelea kwa nyuma, akamtandika yule polisi jambazi rungu moja la mpingo, akaanguka na kufa palepale, majambazi yakakimbia yakiacha kila kitu. Polisi wakamkamata yule mlinzi lakini kelele za wananchi na jitihada za kampuni, wakalazimika kumwachia, na kampuni ikamzawadia mlinzi jasiri aliyeua polisi jambazi.

Mjaka ya nyuma, nikiwa naishi Chuo kikuu UDSM kulikuwa na matukio mengi ya vibaka waliokuwa wakihusishwa na baadhi ya polisi. Likitokea tu tukio, polisi wanakuja mara moja, wanaanza kuorodhesha vitu vilivyoibiwa. Wewe unadhani wanachukua hizo taarifa kusaidia uchunguzi, kumbe wanataka kujua vitu vilivyoibiwa ili wasidanganywe kwenye mgao.
 

Prof. Tibaijuka alisema kuwa alimwambia Lowasa wakati anahamia upinzani kuwa, hajui kuwa mfumo wetu wa Tanzania hauruhusu mtu kuwa Rais kutoka chama kingine chochote zaidi ya CCM? Lowasa akamjibu kuwa anajua, lakini amechoka kunyanyaswa.

Kwa hiyo unachokisema kina ukweli kwa sehemu kubwa.
 

Hakuna mahali au taasisi ambayo inakuwa na watu wote walio safi. Kilicho tofauti ni kwamba kuna nchi ambazo kuna waovu lakini waovu wanaadhibiwa vikali kiasi cha kupunguza idadi ya watu waovu.

Lakini zipo nchi, kama Tanzania, waovu wenye madaraka au mamlaka ndani ya Serikali, kuna wakati badala ya kuadhibiwa, wanatukuzwa. Fikiria mawaziri ambao ni mafisadi, taasisi na wizara zao zinatajwa kwa ufisadi mkubwa, tena kwa vielelezo, hakuna anayeadhibiwa, na kuna wakati wanapandishwa vyeo au kuhamishwa wizara.
 
Tafsiri ya kutumia akili ni ipi? Nguvu hutumika baada ya akili

Akili ndiyo humwongoza mwanadamu atumie nguvu wapi, atumie wakati gani, atumie kwa kiwango gani. Ukiwa huna akili unatumia tu nguvu, nguvu zako zinaweza kuwa chanzo cha uharibifu.
 
Changamoto ya chombo chetu cha Polisi ni kufanyakazi kwa kupokea maelekezo toka juu!
 
Nipe jina la polisi mmoja tu ambaye ana cheo cha PhD.

Yaani polisi anayeitwa Afande Dokta...
Wapo wengi sana sana mkuu , mimi nimesoma na dr mangu ifm, na kulikuwa na phd kama 4 nimesoma nao wote walikuwa mapolisi, nenda pale oysterbay kuna ocd alitokea mbweni nae ni phd , kiufupi ni wengi mno sema kwa nature ya kazi yao huwezi kuwaona kwenye media wakijikweza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…