Peter Kibatala akwamisha kesi ya kina Mdee

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Wakili wa CHADEMA, Peter Kibatala safari hii amesababisha kesi ya wabunge 19 wa CHADEMA kuahirishwa hadi mwezi wa 3 mwaka 2023.

=====

Mahakama Kuu imeahirisha kesi iliyofunguliwa na wabunge 19 wakipinga uamuzi wa Chadema kuwafukuza uanachama, baada ya wakili anayewakilisha Chadema, Peter Kibatala kuwa kwenye vikao vya Mahakama Kuu vya usikilizwaji wa kesi za jinai vinavyofanyika mkoani Mwanza.

Akizungumzia hatua hiyo leo Jumanne Desemba 6, wakili anayemwakilisha Halima Mdee na wenzake 18, Edson Kilatu amesema shauri hilo lilikuja Kwa ajili ya usikilizwaji na mahakama hiyo imepanga kusikiliza shauri hilo Machi 6 na 9, 2023.

"Wakili Kibatala aliomba udhuru na kutujulisha pamoja na mahakama yenyewe kutokana na sababu hiyo ya msingi mahakama hili imeridhia ihairishe shauri hili," amesema Kilatu.

Kilatu amesema sasa hivi mahakama inaenda likizo na baada ya likizo hiyo itaanza vikao vya mahakama Kuu vya usikilizwaji wa kesi za jinai hivyo shauri hilo imesogezwa mbele hadi Machi 6 na 9, 2023.

Kesi hiyo ipo mbele ya Jaji, Cyprian Mkeha ambapo Mbunge wa viti maalumu, Jesca Kishoa ataendelea kuhojiwa Machi 6 na 9,2023 na mawakili wa Chadema.

Wabunge hao wanapinga uamuzi huo kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review), wakidai kuwa walifukuzwa isivyo halali kwa kuwa hawakupewa haki ya kusikilzwa, hivyo wanaiomba mahakama hiyo itengue.

Wengine walioitwa kuhojiwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee, aliyekuwa makamu mwenyekiti Bawacha, Hawa Mwaifunga, aliyekuwa Katibu Bawacha, Grace Tendega, na aliyekuwa mweka hazina Bawacha, Ester Matiko; Ester Bulaya na Cecila Pareso.

Mpaka sasa tayari wabunge watano wa Viti Maalumu wamehojiwa na mawakili wa Chadema kuhusiana na ushahidi wao waliowasilisha mahakamani hapo Kwa njia ya kiapo ni Hawa Mwaifunga, Grace Tendega, Nusrati Hanje, Cecilia Pareso na Kishoa.

Chanzo: Mwananchi

Wakili anayeongoza kula hela za Chadema bila kushinda kesi yoyote bwana Peter Kibatala safari hii amesababisha kesi ya wabunge 19 wa Chadema kuahirishwa hadi mwezi wa 3 mwaka 2023, baada ya kushindwa kutokea mahamakani bila sababu zozote za msingi, huku akiendelea kulipwa mshahara na marupurupu mengi kutoka kwenye ruzuku ya chama.

Ikumbukwe ni Peter Kibatala aliyesimamia kesi ya Mbowe ambayo mahakama ilimkuta na kesi ya kujibu kuhusu ugaidi wake.
 
Wakati mdada yule aliposhindwa kutokea mahakamani kwa madai ya kuumwa kiuno ulinyamaza, leo unajitikeza kama konokono aliyelowa mkojo wake mwenyewe.

Pia kumbuka mmoja wa hao covid 19 aliiomba mahakama aiombe Chadema wamalizane nje ya mahakama baada ya kutomjua aliyempendekeza kuwa mbunge!
 
Wakili anayeongoza kula hela za Chadema bila kushinda kesi yoyote bwana Peter Kibatala safari hii amesababisha kesi ya wabunge 19 wa Chadema kuahirishwa hadi mwezi wa 3 mwaka 2023...

Acha kupotosha. Mbona akina Halima Mdee walihairisha kesi Mara nyingi na ulikuwa kimya. Mahakama zinatumika na CCM kurefusha hi kesi mpaka 2025 ili kuendelea kupata mikopo ya wazungu.
 
Chadema hailipwi hata senti moja ya ruzuku. Uwe unashirikisha akili (kama unazo) kabla ya kuropoka. Hao mawakili wenu si ndiyo wameshindwa kesi huko hadi Airbus limelaliwa huko ughaibuni.
 
Acha kupotosha. Mbona akina Halima Mdee walihairisha kesi Mara nyingi na ulikuwa kimya. Mahakama zinatumika na CCM kurefusha hi kesi mpaka 2025 ili kuendelea kupata mikopo ya wazungu.
Kwa nini Kibatala hakwenda leo?
 
Wakili anayeongoza kula hela za Chadema bila kushinda kesi yoyote bwana Peter Kibatala safari hii amesababisha kesi ya wabunge 19 wa Chadema kuahirishwa hadi mwezi wa 3 mwaka 2023, baada ya kushindwa kutokea mahamakani bila sababu zozote za msingi, huku akiendelea kulipwa mshahara na marupurupu mengi kutoka kwenye ruzuku ya chama.

Ikumbukwe ni Peter Kibatala aliyesimamia kesi ya Mbowe ambayo mahakama ilimkuta na kesi ya kujibu kuhusu ugaidi wake.
.View attachment 2437457
Sasa inakuuma nini kama CDM wanaendelea kulipa wakati aashindwa kesi....!!
 
Wakili anayeongoza kula hela za Chadema bila kushinda kesi yoyote bwana Peter Kibatala safari hii amesababisha kesi ya wabunge 19 wa Chadema kuahirishwa hadi mwezi wa 3 mwaka 2023, baada ya kushindwa kutokea mahamakani bila sababu zozote za msingi, huku akiendelea kulipwa mshahara na marupurupu mengi kutoka kwenye ruzuku ya chama.

Ikumbukwe ni Peter Kibatala aliyesimamia kesi ya Mbowe ambayo mahakama ilimkuta na kesi ya kujibu kuhusu ugaidi wake.
.View attachment 2437457

Sijawahi mdharau mtu lakini plies nisamehe bure
 
Hii kesi lazima ifike 2025 au 2024 mwishoni kwa manufaa ya chadema. Ni igizo kama isidingo tuu. Ila litafika mwisho karibia na uchaguzi
 
Back
Top Bottom