Pete iliyotangatanga

Pete iliyotangatanga

69a0f5577c598f7d7bd12be8411f405b.jpg
hizi Pete za namna hii hata ukiokota usiichukue
 
Mimi nimekuelewa vizuri sana..hiyo imeshakuwa roho yako ya pili na siku likitokea la kutokea (sikuombei mabaya )nayo itapotea mazima na isipopotea italeta shida sana kwa watakao kuwa nayo

Inawezekana ikawa ivyo ila sitaki kuliwekea maanani
 
69a0f5577c598f7d7bd12be8411f405b.jpg
hizi Pete za namna hii hata ukiokota usiichukue
Nimesikia juzi kwenye redio akihojiwa Ben Pol naye anayo yake ya fuvu akasema ni urembo tu.
.
.
.
Nikajiulizaaaaaaaa tangu lini fuvu likawa urembo siku hizi!?? #kuigaNIkubaya
 
Nimesikia juzi kwenye redio akihojiwa Ben Pol naye anayo yake ya fuvu akasema ni urembo tu.
.
.
.
Nikajiulizaaaaaaaa tangu lini fuvu likawa urembo siku hizi!?? #kuigaNIkubaya
Inawezekana kabisa hajui maana yake au anajua ila anaficha ukweli ila kwa vyovyote ile Pete ya fuvu si kitu cha kawaida au urembo hata kidogo
 
Pete ni mamlaka; ndio maana wafalme wana pete; au kiongoz yeyote anaweza kuwa na pete ya uongoz huo. Kuna pete za ndoa uchumba na mengineyo. Mpendao pete vidolen muwe makin na pete za urembo mnaweza beba majini humo lasivyo muwe mnaziombea. Hatq kuna hiz pete za miguun nazo tunaita urembo lakin unabeba had majin humo mdan; kuna vikuku pia. Sikatai msichana kujiremba sababu ni vizur pia. Lakin tujifunze kuombea hivyo vitu. Naongea ninajua ninachosema hapa na nina uhakika; tuwe makin sana unaweza jikuta kila cku ugomv hauish ndan ya nyumba au rlshp hazidumu kumbe una kitu umebeba ambacho kina leta yote hayo.watu mwaweza bisha sababu hayajawakuta ila yakikukuta mtajua nn namaanisha. Hii dunia ya sasa ni kuwa makin na kila kitu si hivyo tu vya hapo juu; na vingine vyote. Mungu atulinde hich kizaz
 
Inawezekana mwana jf mmoja anayo humu!huku ni kuleta mahaba kwa uji wa matanga huku.


Mshana! Ngoja kwanza....

Hebu ongea na huyo jamaa afunguke hiyo Pete ikoje
kama hana picha basi chukua maelezo alafu yaweke ktk picha hata kwa kuchora kisha itupie hapa

kuna Pete moja hapa home hata sielewi elewi jinsi nilivyoipata
 
Mshana! Ngoja kwanza....

Hebu ongea na huyo jamaa afunguke hiyo Pete ikoje
kama hana picha basi chukua maelezo alafu yaweke ktk picha hata kwa kuchora kisha itupie hapa

kuna Pete moja hapa home hata sielewi elewi jinsi nilivyoipata
Nawasiliana naye kupata zile barua..kwa picha itakuwa ngumu by then tech haikuwa so advanced
 
Ni habari ya mwaka 1993 Ubungo Kibo mtaa wa Rombo
Wakati ule pale Kibo palikuwa ni kituo maarufu cha kuuzia mikate kwa mabasi ya mikoani na hata magari mengine
Basi kukawa na kijana mmoja mwanachuo wa chuo cha ualimu Nachingwea ambaye aliachiwa nyumba nzima na kaka yake aliyeenda likizo..basi jamaa kila jioni alikuwa anapanda kule Kibo barabarani kununua mkate kwa binti mmoja
Mazoea ya kuuziana mikate yakajenga mahusiano
Binti akawa anaenda mtaa wa Rombo kwa mpenzi wake kila wakati mpaka likizo Inakaribia kwisha , lakini jamaa alimdanganya binti kuwa yeye ni afisa wa shirika la simu TTCL na anaenda Dodoma kikaoni
Binti akampa mshikaji Pete kama zawadi wakaagana jamaa akasepa zake chuoni
Baada ya wiki moja binti akaenda kumwangalia kama mpenzi amerudi (wakati ule simu za mkononi sio kama siku hizi zilimilikiwa na matajiri )kufika pale kamkuta mwenye nyumba na mkewe binti kajitambulisha kuwa anamtaka mwenye nyumba
Ikabidi tu aambiwe ukweli kuwa huyo mwenye nyumba anayemtaka ni mwanachuo tu alikuwa kaachiwa nyumba...binti akasepa kwa uchungu

=============

Baada ya wiki moja yule binti akarudi pale akiwa kavimba uso kisa kapigwa na bwanaake mwingine aliyemvisha Pete lakini yeye akaigawa kwa huyu mwingine
Mawasiliano yakafanyika Nachingwea kwa njia ya barua na ikathibitika ni kweli jamaa aliondoka na Pete ya yule binti
Huku Dar jamaa akawa kawa mbogo kweli anataka Pete yake na alikuwa keshapelekwa mpaka pale nyumbani na yule mwanamke
Kule chuoni jamaa kufika ile Pete akampa mpenzi wake lakini ilipofika February yule mpenzi akapata msiba kwao Ikabidi aende lakini aliporudi chuoni akawa hana ile Pete (ilikuja kujulikana baadae naye alimpa mwanaume kule kijijini)
Huku Dar ilikuwa ishakubaliwa kuwa mpaka likizo ya march Pete haijarudishwa jamaa alipwe pesa

Katika kupatana jamaa alipwe bei gani akaanza kujichanganya jinsi alivyoipata hiyo Pete na thamani yake (ilikuja kujulikana jamaa alipewa na jimama ambalo nalo lilipewa na mkongo mmoja )hakulipwa chochote
Kuja kufuatilia mzunguko wa ile Pete ilikuwa imeshapitia mikono saba ndani ya kipindi kisichozidi miezi minne
Yule mama wa kwanza alipewa na mkongo November 1992 November hiyo hiyo akampa kijana, kufika December kijana akampa mpenzi wake muuza mikate , lakini Dec hiyo hiyo binti akapata mpenzi mwingine 'afisa wa TTCL' akamhonga...!
January afisa mwanachuo akampa mpenzi wake wa chuoni ambaye naye February aliporudi nyumbani akampa mpenzi wake wa huko......
Ni habari ya kweli na nimepata ridhaa ya mlengwa ambaye kwa sasa ni afisa kwenye serikali ya Magu
Kikubwa ni kwamba hizi zawadi tunazopeana kwenye mapenzi nyingine si zawadi bali ni roho zinazotangatanga

Nilitegemea kusikia Mazara ya Pete Ila sijasikia
 
Back
Top Bottom