Pete iliyotangatanga

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,761
730,024
Ni habari ya mwaka 1993 Ubungo Kibo mtaa wa Rombo
Wakati ule pale Kibo palikuwa ni kituo maarufu cha kuuzia mikate kwa mabasi ya mikoani na hata magari mengine
Basi kukawa na kijana mmoja mwanachuo wa chuo cha ualimu Nachingwea ambaye aliachiwa nyumba nzima na kaka yake aliyeenda likizo..basi jamaa kila jioni alikuwa anapanda kule Kibo barabarani kununua mkate kwa binti mmoja
Mazoea ya kuuziana mikate yakajenga mahusiano
Binti akawa anaenda mtaa wa Rombo kwa mpenzi wake kila wakati mpaka likizo Inakaribia kwisha , lakini jamaa alimdanganya binti kuwa yeye ni afisa wa shirika la simu TTCL na anaenda Dodoma kikaoni
Binti akampa mshikaji Pete kama zawadi wakaagana jamaa akasepa zake chuoni
Baada ya wiki moja binti akaenda kumwangalia kama mpenzi amerudi (wakati ule simu za mkononi sio kama siku hizi zilimilikiwa na matajiri )kufika pale kamkuta mwenye nyumba na mkewe binti kajitambulisha kuwa anamtaka mwenye nyumba
Ikabidi tu aambiwe ukweli kuwa huyo mwenye nyumba anayemtaka ni mwanachuo tu alikuwa kaachiwa nyumba...binti akasepa kwa uchungu

=============

Baada ya wiki moja yule binti akarudi pale akiwa kavimba uso kisa kapigwa na bwanaake mwingine aliyemvisha Pete lakini yeye akaigawa kwa huyu mwingine
Mawasiliano yakafanyika Nachingwea kwa njia ya barua na ikathibitika ni kweli jamaa aliondoka na Pete ya yule binti
Huku Dar jamaa akawa kawa mbogo kweli anataka Pete yake na alikuwa keshapelekwa mpaka pale nyumbani na yule mwanamke
Kule chuoni jamaa kufika ile Pete akampa mpenzi wake lakini ilipofika February yule mpenzi akapata msiba kwao Ikabidi aende lakini aliporudi chuoni akawa hana ile Pete (ilikuja kujulikana baadae naye alimpa mwanaume kule kijijini)
Huku Dar ilikuwa ishakubaliwa kuwa mpaka likizo ya march Pete haijarudishwa jamaa alipwe pesa

Katika kupatana jamaa alipwe bei gani akaanza kujichanganya jinsi alivyoipata hiyo Pete na thamani yake (ilikuja kujulikana jamaa alipewa na jimama ambalo nalo lilipewa na mkongo mmoja )hakulipwa chochote
Kuja kufuatilia mzunguko wa ile Pete ilikuwa imeshapitia mikono saba ndani ya kipindi kisichozidi miezi minne
Yule mama wa kwanza alipewa na mkongo November 1992 November hiyo hiyo akampa kijana, kufika December kijana akampa mpenzi wake muuza mikate , lakini Dec hiyo hiyo binti akapata mpenzi mwingine 'afisa wa TTCL' akamhonga...!
January afisa mwanachuo akampa mpenzi wake wa chuoni ambaye naye February aliporudi nyumbani akampa mpenzi wake wa huko......
Ni habari ya kweli na nimepata ridhaa ya mlengwa ambaye kwa sasa ni afisa kwenye serikali ya Magu
Kikubwa ni kwamba hizi zawadi tunazopeana kwenye mapenzi nyingine si zawadi bali ni roho zinazotangatanga
 
Nataka nikupe mkufu
Kama huu
1462036386959.jpg
 
Mshana jr jaribu kufanya utafiti humu JF inawezekana imo humu maana kuna watu wanaweza kuleta uzi mpaka mkabaki mnashangaa.
 
Back
Top Bottom