Pesa imekauka kwaresma

Pesa imekauka kwaresma

pumzihaiuzwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2015
Posts
3,273
Reaction score
3,087
Wanazengo pesa imeyeyuka? Najiuliza funga hii mbona imekua ya kimya sana zile shamra shamra za wasanii, na makampuni mbalimbali nchini za kufuturisha na kutoa vyakula sehemu mbali mbali, za vituo vya yatima na wagonjwa na wasiojiweza mbona mfungo huu wa kwaresma umekua kimya sana wako wapi mabigwa wa kufuturisha hakika mifuko imechanika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Mkuu Pumzi, ni kama umechanganya Madesa.
Kwa kawaida hii Kwaresima inapitaga kimya kimya maana ni kama vile upande huu upo kwenye Maombolezo.
Hizo shughuli zote ulizotaja hapo zinafanyika zaidi kwenye Mwezi ulee wa Upande Mwingine...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hizo mbwembwe sio msimu wake.
Japo kutoa wanatoa ndio maana ya udiakonia
Sio lazima media zimulike.
Ubarikiwe na bwana Yesu kristo
 
Hivi Wakristo nao wana mambo ya kufuturisha/ shamrashamra? Sijawahi kuona/kusikia.
Wanazengo pesa imeyeyuka? Najiuliza funga hii mbona imekua ya kimya sana zile shamra shamra za wasanii, na makampuni mbalimbali nchini za kufuturisha na kutoa vyakula sehemu mbali mbali, za vituo vya yatima na wagonjwa na wasiojiweza mbona mfungo huu wa kwaresma umekua kimya sana wako wapi mabigwa wa kufuturisha hakika mifuko imechanika

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Mkuu Pumzi, ni kama umechanganya Madesa.
Kwa kawaida hii Kwaresima inapitaga kimya kimya maana ni kama vile upande huu upo kwenye Maombolezo.
Hizo shughuli zote ulizotaja hapo zinafanyika zaidi kwenye Mwezi ulee wa Upande Mwingine...!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu lakini najiuliza hata kama ni maombolezo lakini si ni mwezi wa kufanya matendo ya huruma na kutubia makosa nilitegemea kuona shamra hizi kwenye vyombo vya habari lakini hali imekua siyo kabisa ni hivi juzi tu nikiwa kijiwe na washkaji ndio nimejua kuna mfungo nikastaajabu mbona hauna shamrashamra hata sokoni kupo kupo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi hatunaga hizo mbwembwe na ndio maana kipindi cha mfungo wa kwaresima huwezi kukuta watu wamefunga mabaa au mahotel, utaipimaje imani yako kama unawakataza wengine wasio wa imani yako kuendelea na maisha yao ya kawaida........ukifika mfungo wa upande wa pili hapo ndipo unakutana na zile simulizi za wamiliki wa baa na wauza kitimoto wanalalamika kwamba biashara imekuwa mbaya.........hilo ni jambo la kujiuliza sana, tumeambiwa hivi:- mfungapo msiwe kama wale wanafiki wanaojiumbua sura zao na kujipausha midomo.......naomba niishie hapo

komando kinjekitile ngwale
 
Lini kwenye mfjngo huu uliona shmra shamra na huko sokoni uliexpect nini,watu wanunue viazi au,
Umemix ma file

Sent using Brain
 
Sisi hatunaga hizo mbwembwe na ndio maana kipindi cha mfungo wa kwaresima huwezi kukuta watu wamefunga mabaa au mahotel, utaipimaje imani yako kama unawakataza wengine wasio wa imani yako kuendelea na maisha yao ya kawaida........ukifika mfungo wa upande wa pili hapo ndipo unakutana na zile simulizi za wamiliki wa baa na wauza kitimoto wanalalamika kwamba biashara imekuwa mbaya.........hilo ni jambo la kujiuliza sana, tumeambiwa hivi:- mfungapo msiwe kama wale wanafiki wanaojiumbua sura zao na kujipausha midomo.......naomba niishie hapo

komando kinjekitile ngwale
Komando Kinje mzee wa chompwicho upo? 😂😂😂😂
 
Vitu ambavyo huwezi kuvikuta kwaresma
1. Kitimoto kudoda mabuchani,baa,etc
2.kufuturisha mbele za kamera
3.Vyakula kupanda bei ghafla
4. Watu kulindana/kuchunguzana kama wameingia kwa mama lishe,migahawani,hotelini kula kisa kuna mfungo
5.Mtu kupigwa kisa amekutwa anakula iwe hadharan au sirini
6.Hakuna marufuku ya kukaangiza misosi ikanukia sana eti utawatamanisha wenzio walio katika mfungo
7.Hakuna matangazo ya Marufuku ya kula hadharan
 
Back
Top Bottom