Pesa 8 zenye nguvu Afrika

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Nguvu ya pesa hutambulika kwa vitu vingi ikiwemo upatikanaji na uzalishaji wake ( supply and demand ), nguvu za soko ndani ya nchi, mfumko wa bei na soko la ubadilishwaji pesa.

Dola ya marekani huchukuliwa kuwa pesa yenye nguvu zaidi duniani hivyo katika upimaji wa pesa nyingine, tunaitumia kujua nguvu ya pesa nyingine.

1. Dinar ya Libya
Hii ndio pesa yenye nguvu zaidi afrika ukiangalia thamani yake dhidi ya dola ya marekani na nguvu yake ya kununua (purchasing power)
1$ = 1.38 dinar za Libya


2. Dinari ya Tunisia
Hii ni pesa ya pili kwa afrika
1$ = 3.05 Tunisian Dinari.


3. Cedis ya Ghana
Ghana ni nchi pekee ya afrika magharibi ambayo ipo kweny nane bora ya nchi nane zenye pesa yenye nguvu afrika

1$ = 5.50 Ghana cedis


4. Dinar ya Morocco
1$ = 9.55 Moroccan dinar


5. Pula ya Botswana
Pesa ya Botswana inaitwa pula. Iliwekwa ili kuichukua nafasi ya Rand ya Afrika ya Kusini

$ 1 = 10.60 pula

6. Kwacha ya Zambia
Hii ni pesa ya Zambia ambayo ilichokua nafasi ya Paundi ya Zambia.
$ 1 = 11.98 kwacha

7. Lilangeni ya Swazi
$ 1 = 13.99 lilangeni



8. The South African Rands
South African rand ilichukua nafasi ya South African pound.

$ 1 = 14.18 rands
 
Hakuna Nchi kwa upande wa fedha yake naikubali Kama Zambia. Sijui wametumia Effort gani kubadii kutoka Kuwa pesa ya thamani ya Chini mpaka ubora huo.
Maana Kwacha ilikuwa mara mia kabisa TZS.
Lakini toka akamate Nchi Lungu, Mambo yanaenda Mswano kwa Ustable wa Currency yao. Tanzania CCM ndiyo Shida.
 
Kwacha tangu lini ? Hii mbona Kali sababu fedha yao ilijuwa ovyo sana kulinganisha na Shilingi ya Tanzania
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazambia walifuta sifuri kadhaa kutoka kwenye Kwacha yao.

Hilo linakuonesha kwamba, thamani ya pesa haina maana ya uchumi mzuri.

Hata sisi tunaweza kuondoa sifuri tatu kwenye shilingi yetu, dola moja ya kimarekani iwe shilingi mbili na ushee.

Tunaweza kufanya hilo leo.

Lakini, hilo halitamaanisha kuwa uchumi wetu utaimarika mara elfu.
 
Kwacha imekuwaje na thamani kubwa cku izi? Wanatumia mechanism gn?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama KENYA haimo ni maajabu ya SENENE?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…