Personalities: Aina za mtu kwenye mtu na mahusiano na jamii.

The Alchemist

Senior Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
177
Reaction score
148
Mwanadamu ni kiumbe wa tabia (a creature of habit). Huwa kile ambacho hukifanya kwa muda. Kila anachofanya huwa. Leo nizungumzie Kwa ufupi personalities za mtu kulingana na mazingira na madhara ya kutokumwona mtu katika tabia anayotaka kuonekana anayo.

1) Personality ya mtu mwenyewe: Hii ni yeye akiwa mwenyewe. Personality hii ni exclusive domain ya mtu mwenyewe na akuna mtu mwingine yeyote anaifahamu. Kuna tabia ama utu anaokuwa nao ambao kwa hali ya kawaida hawezi kabisa kuuonyesha mbele ya mtu mwingine yeyote.

2) Personality ya mtu na watu wa karibu sana. Familia, marafiki wa karibu sana na mke au mume. Hii personality mtu anaionyesha tuu akiwa na watu wa karibu sana na mara nyingi hii huwa ndio tabia halisi ya mtu husika ama hujenga kwa kiasi kikubwa tabia ya mtu husika. Katika Personality hii, jamii ambayo haipo kwenye makundi tajwa, haiwezi kabisa kukutana nayo.

3) Personality ya Mtu na marafiki wa kawaida/Jamii. Hapa mtu huishu picha ambayo kimsingi hutaka jamii nzima imtambue kama ivyo. Mara nyingi personality hii ime-hariri sana tabia za mtu ili aweze ku-coform na norms za eneo husika/watu husika. Hapa ndio reputation ama sifa ya mtu hujengwa. Hapa huwa na vita sana kuijenga na vita zaidi kama mhusika ni public figure.

Personality na mahusiano.

Kwa kila personality aliyo nayo mtu, hutaka aonekane ivyo na kundi husika na asiyemwona hivyo huwa adui yake. Kama yupo na familia ama watu wa karibu, asingependa kabisa wajue personality yake akiwa na marafiki na mwanafamilia atakayetaka kukomalia na kufahamu basi utengeneza chuki ama uadui wa kiwango fulani, kadhalika, personality yake akiwa na marafiki ama personality yake akiwa mwenyewe, ataki kabisa ifikie uma kwa ujumla.

Kadhalika, mtu ambaye anataka kujulikana kama mtu wa wanawake atagombana ama kumkaripia yule atakayemwona kuwa ni domo zege.
Ama ni mtu wa wanawake kweli ama siyo ila bado atataka kuonekana namna anavyotaka kuonekana.

Kadhalika, wengine utaka kuonekana wasomi, wanajua kupika sana, watu wa Mungu, Ibada na madhabahu, wanamziki wakali wakati kiuhalisia hawana hizi karama ama tabia.

Kwenye kitabu cha How to Make Friends and Influence People, Dale Carnegie anashauri kwamba ili kuongeza ushawishi kwa mtu ama jamii, kutengeneza marafiki ni lazima umwona kila mtu namna anavyotaka kuonekana. Hii ni weakness kubwa sana kwa watu. Ni window ya kuingia kwenye moyo wa mtu, window ya kutolewa pia. See a persona for who he want to be seen.

Aidha, kutokumwona mtu namna na vile ambavyo mtu husika anataka kuonekana unajihakikishia uadui mkubwa na mtu husika na moja kwa moja unapoteza ushawishi wako kwake.

Wewe ni tabia gani ambayo usingependa jamii ifahamu, personality gani unapenda kutambulika nayo kwa jamii? Marafiki? Wewe mwenyewe?

Tujadili.

I am The Alchemist
 
Ahsante.
somo nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom